Jamhuri Kihwelu ‘Julio’ atangaza kuachana na soka

Jamhuri Kihwelu ‘Julio’ atangaza kuachana na soka

Kurzweil

JF-Expert Member
Joined
May 25, 2011
Posts
6,621
Reaction score
8,411
Kocha mkuu wa Mwadui FC Jamhuri Kihwelu ‘Julio’ ametangaza rasmi kuacha kufundisha soka la Tanzania kutokana na maamuzi mabovu katika baadhi ya michezo ligi kuu Tanzania bara.

“Kuanzia leo na kuendelea, sitaki tena mpira. Najiuzulu mpira moja kwa moja sitaki kwasababu mpira wa Tanzania unachezwa kwa siasa sana. Mpira unachezwa kwa ajili ya kufurahisha watu hata wasiokuwa na uwezo waonekane wanajua, hiki kitu kinaumiza sana”, amesema Julio baada ya mchezo kati ya Mbeya City vs Mwadui uliomalizika kwa vijana wa Julio kulala kwa bao 1-0 ugenini.

“Nimeshafundisha mpira Qatar, Yemen na Dubai lakini sijawahi kufeli lakini kuna kundi la watu wanajua huyu ukimfanyia hivi unamharibia ni kuharibu mpira wetu ndio maana vilabu vyetu vikienda kwenye mashindano ya kimataifa havifanyi vizuri.”

“Kwahiyo kuanzia sasahivi natangaza sitaki kuwa kocha wa mpira wa Tanzania tena labda nikipenda niwe naenda kuangalia mpira lakini kinyume cha hapo sitaki mpira kwasababu tunakoelekea siko. Kuna watu watasikitika kutoka kwangu kwenye mpira lakini kwa kipindi hiki bora nipumzike nifanye kazi nyingine kwanza, mawashuru watanzania wote waliokuwa karibu na Julio.”
 
Daahhh na ule mchezo je kauwacha pia....
1475485729965.jpg
 
Kwani refa aliyechezesha ni yule wa yanga wa goli LA mkono,mchezaji wa 12 wa yanga
 
jamhuri-kihwelo.jpg

julio.jpg
Kocha wa klabu ya Mwadui FC ya Shinyanga Jamhuri Kiwelu Julio jioni ya Oktoba 2 2016 alitangaza maamuzi ya kuwashtusha walio wengi, hiyo ni baada ya mchezo wake wa ugenini kati ya Mwadui FC dhidi ya Mbeya City kumalizika kwa kupoteza kwa goli 1-0.

Julio baada ya mchezo huo uliochezwa katika uwanja wa Sokoine Mbeya alitangaza kuachana na soka la Tanzania, hiyo inatokana na kutoendelea kuridhishwa na uwezo wa waamuzi wa soka wa Tanzania, kwani katika mchezo dhidi ya Mbeya City amekiri kuwa walifungwa kihalali lakini muamuzi alionesha kuwawekea vikwazo wasisawazishe.
"Natumia nguvu nyingi kufundisha, kampuni inatumia pesa nyingi kugharamia timu, tunasafiri safari ndefu halafu mwisho wa siku waamuzi wanafanya upendeleo wa wazi wazi",alisema Julio.

“Mchezaji wetu anapambana hadi anapata mpira kwenda kufunga refa badala yake anatoa faulo kwao kwenye timu ya adui kusema kweli kimeniuma sana, kwa hiyo nitangaze rasmi kuanzia sasa hivi na kuendelea mimi sitaki kuwa kocha wa mpira wa miguu katika soka la Tanzania tena”.
Chanzo: Malunde blog
 
Fanya mishe zingine Julio,Ili maisha yasonge,wakuu yule msema ovyo wa Yanga Jerry Muro kapotea,hata kutoa maoni binafsi Kama yeye sijamsikia!,au sasa anafanya kazi kwa Mdosi Manji nini?
 
Acha,kwani si ulikuwa unafanya kwa ajili ya maisha yako na familia yako kwa ujumla.
 
Asiondoke buana

Mi napendaga tu vijembe vyake

Kuhusu kuwa kocha bora sina uhakika
 
Hoja yake ni ya msingi sana,kuhusu hawa waamuzi wa soka.

Miaka ile golikipa maarufu Juma Pondamali alikuwa anawapa vichwa sana hawa waamuzi.
 
Julio kuwa mkweli kwamba ulifanya makosa kwenye usajili wa Wachezaji. Hivyo wajibika kuliko kuhamisha zingo la lawama kwa Maamuzi.
Umefanya uamuzi mzuri kuliko ungesubiri ufukuzwe. Umejitambua na umejiuzuru kulinda heshima yako.
Kwa upande mwingine huo ni uhaini na unastahili ushitakiwe Kwa kosa la uhaini. Usajili mbovu ufanye mwenyewe kisha ukimbie uwanja wa mapambano?! China unapigwa risasi. Hata hivyo rudisha fedha za usajili ulizozitumia vibaya.
 
Back
Top Bottom