Jamhuri, Morogoro: Mtibwa FC 0 -1 Simba SC, Ligi Kuu Soka Tanzania Bara

kirerenya

JF-Expert Member
Joined
Aug 27, 2013
Posts
1,696
Reaction score
2,253
Leo ni kivumbi cha ligi kuu soka Tanzania bara ambapo mnyama simba atashuka dimbani kuumana na Mtibwa Sugar.

Ni mechi inayotarajiwa kuwa na ushindani wa kipekee kwani Mtibwa wamekuwa wanazikazia timu kubwa za Dar ikiwemo Simba, Azam na Yanga.

Katika mechi iliyopita ambapo Simba walikuwa nyumbani, Mtibwa iliikazia Simba baada ya kuifunga goli la mapema. Goli lililodumu mpaka dk 90. Simba ilifanikiwa kuchomoa kupitia faul iliyopigwa na mshambuliaje wake mahiri Emmanuel Arnold Okwi kutoka Uganda na kufanya mpira kumalizika kwa sare ya 1-1.

Leo mtibwa wapo uwanja wao wa nyumbani Jamhuri Morogoro na wanawakaribisha wekundu hawa wa msimbazi ambao ni vinara wa ligi kuu kwa sasa. Japo mechi iliyopita kati ya Simba na Njombe mji, simba iliibuka na ushindi wa 2-0.

Kitendawili kinabaki, Mnyama huyu mkali kabisa mwituni atafanikiwa kuwararua wakata miwa hawa na kuzitafuna miwa?



Kikosi cha Mtibwa Sugar

Benedict Tinoc, Kibwana Shomary, Hassan Mganga, Hassan Isihaka, Dickson Daudi, Shabani Nditi, Salum Kihimbwa, Henry Joseph, Stamil Mbonde, Hassan Dilunga, Ismail Mhesa

Kikosi cha akiba

Shaban Kado, Cassian Ponera, Saleh Khamis, Ally Makarani, Ayoub Semtawa, Haruna Chanongo, Hussein Javu



Hiki hapa kikosi kamili cha Simba
Aishi Manula; Shomary Kapombe, Asante Kwasi, Paul Bukaba, Yusufu Mlipili; Jonas Mkude, Mzamiru Yassin, Nicholas Gyan, Shiza Ramadhani; John Bocco, Emmanuel Okwi

Kikosi cha akiba
Said Nduda, Mohamed Hussein, Haruna Niyonzima, Mwinyi Kazimoto, Said Ndemla, Rashid Juma, Laudit Mavugo

Wachezaji wameshaingia uwanjani
Muda wowote mpira utaanza

0'Mpira umeanza hapa dimba la Jamhuri.

1'Bocco anafika langoni kwa mtibwa na kutaka kumtoka kipa, hatimaye kipa anautoa mpira nje.

02'Kipa wa mpira yupo chini anagangwa. Kipa wa akiba anapasha

03'Shomari Kapombe anapiga shuti kali, linatoka nje kidogo ya lango

06'Mtibwa wanafanya shambulizi kali kwenye lango la simba ila wanadhibitiwa na mabeki

07'Mtibwa wameamka baada ya kukoswakoswa na simba, wanaishambulia simba

09'Faul inapigwa kuelekea simba

10'Simba sasa wanaliandama lango la mtibwa

14'Mtibwa wanapiga kona ya kwanza.

16'Okwi anapiga shuti kali golini, lakini kipa anaokoa

18'Timu zote zinashambuliana kwa zamu.

23'Goooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooo
Emmanuel Okwi anapokea pasi kutoka kwa John Raphael Bocco na kuitundika nyavuni huku akiindikia Simba goli la kwanza. Simba 1, Mtibwa 0

27'Mtibwa wanafanya counter attack ila wanadhibitiwa.

28'Mtibwa wanapiga kona, Hasan Dilunga anapiga kichwa na inakuwa ni goal kick

30' Mtibwa wanapiga faul, inapigwa kichwa inakuwa ni kona. Kona inadhibitiwa.

31'Jonas Mkude na Dilunga wanaonyeshwa kadi za njano kwa kutaka kupigana uwanjani

34'Mtibwa wanafanya kila jitihada ili kubadili matokeo, wamekuwa wanajaribu mashuti mengi kwenye lango la simba.

35'Simba wanapata kona ya kwanza na inapigwa na Mzamiru. Kona haijazaa matunda.

37'Kona ya nne kwa upande wa mtibwa inadhibitiwa ila almanusra wapate goli. Kona ya tano inapigwa lakini pia inadhibitiwa. Imekuwa ni kashkash kwenye lango la Simba hapa.

39'Kipa wa simba Aishi Manula ameumia anagangwa

40' Mpira unaendelea na kama kawaida ni kushambuliana kwa zamu.

42'Mtibwa sasa ni kushambulia lango la simba mara kwa mara wakitafuta goli la kusawazisha.

43'Mpira unaendelea baada ya kusimama kwa muda kutokana mchezaji wa Mtibwa kugangwa.

45'Mtibwa wanapiga faul

45+2' Okwi anawachachafya mabeki wa Mtibwa na kuachia shuti moja matata sana lakini golikipa anafanikiwa kulinyaka

45+3'Golikipa wa Mtibwa alikuwa chini na alikuwa anagangwa ila kwa sasa yuko fiti na mpira unachezeshwa fair play.

Mpira ni Mapumziko

45'Kipindi cha pili kimeanza
Okwi anafanya shambulizi ila anadhibitiwa

46'Mtibwa wanarudisha mashambulizi kwenye lango la simba.

47'Mzamiru anawekwa chini, faul inapigwa kwenda mtibwa

50'John Bocco anaachia shuti moja, kipa analiokoa na kusababisha kona
Kona inapigwa na Bocco anaipiga kichwa ila goli linakataliwa.

53'Mtibwa wanajibu mashambulizi na wanawakosakosa simba.

54'Simba nao wanafanya mashambulizi

56'Mtibwa sasa wanaishambulia simba kwa kasi

57'Bocco anapiga mshuti mkali ila unambabatiza mtu.

59'Faul kuelekea Mtibwa inapigwa lakini simba wanapiga kichwa inatoka nje

60'Faul inapigwa kwenda simba, ni karibu kabisa na goli

63'Anatoka Stamili Mbonde, anaingia Husein Javu

64'Anaingia Salim Mbonde, anatoka Mzamiru Yassin

68'Mtibwa wanafanya shambulizi hapa ila Javu anapiga nje

70'Mpira ni kushambuliana kwa zamu

72'Anatoka Hassan Dilunga anaingia Ayoub Semtawa kwa upande wa Mtibwa.

74'mpira ni faul inapigwa kuelekea mtibwa

76'Anaingia Haruna Niyonzima , anatoka Nicolaus Gyan

79'Simba wanaonekana kurudi nyuma. Ni kona kwa upande wa Mtibwa. Kona inatoka nje.

81'Faul inapigwa ila inakuwa ni goal kick

84' Mtibwa wanawabana simba kwenye lango
Mtibwa wanaachia shuti la kushtukiza ila kipa wa simba anadaka.

87'Asante kwasi analala chini baada ya kuzidiwa na maumivu, anatolewa nje.

88'Mtibwa wanaendelea kuwashambulia Simba

90'Simba wanafanya shambulizi la kushtukiza.

90+2'Haruna chanongo anaonyeshwa kadi ya njano kwa kubishana na mwamuzi.

90+3 Haruna Chanongo anapiga shuti na linatoka ila linatoka nje

Mpira umekwisha
 
Na cha mtibwa je?


kila laheri wakata miwa.kila la heri tobiasi kifaru.
 
Mashabiki wa simba na wadau mbalimbali wa soka wamiminika uwanjani
 
Ila Dakika Izi Mtibwa Wanacheza

Na Mvua Inanyesha Hatari.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…