Jamhuri ya Chile | República de Chile

Jamhuri ya Chile | República de Chile

isajorsergio

Platinum Member
Joined
Apr 22, 2018
Posts
4,143
Reaction score
6,560
Jamhuri ya Chile | Republic of Chile au República de Chile

Chile
ni taifa linalopatikana bara la Amerika Kusini likiwa na mipaka baina ya Ajentina, Bolivia, Peru, milima ya Andes na bahari ya Pasifiki.

Chile.jpg

Bendera ya Jamhuri ya Chile

Taifa hili lenye ukubwa wa Kilomita za mraba 756,950 sawa na maili za mraba 292,260 ni nyumbani kwa watu takribani millioni 19,121,776 kufikia Julai 14, 2020.

Kauli kuu ya taifa (Motto) ni “Kwa Haki au Nguvu” | “Por la razón o la fuerza”. Lugha rasmi ni Kihispaniola, pesa rasmi ni Peso ya Chile (CLP), Peso 1 ni sawa na Centavos 100.

Santiago.jpg

Jijini Santiago ©Chile Travel

Mji mkuu wa Chile ni Santiago mji wenye kuhodhi shughuli za kiserikali, biashara na mji wenye maendeleo zaidi ndani ya Chile.

Valparaiso.jpg

Jijini Valparaíso ©ValparaísoEn

Miji mingine iliyokuwa bora ni Valparaíso, Concepción, La Serena, Iquique, Antofagasta, Punta Arenas, Valdívia, Talca, Puerto Montt, Coquimbo, Rancagua na Temuco.

Historia ya Kati ndani ya taifa

Chile iliyopitia misukosuko na machafuko mbalimbali sehemu yenye historia ya mapinduzi, mnamo miaka ya 1960 na 1970 vuguvugu zito lilipamba moto kutokana na Chile ya wakati huo kutokuwa na matumaini, furaha wala faraja baina ya WaChile walioathirika na ukiukwaji wa haki za binadamu, siasa za mlengo mmoja, rushwa, ukosefu wa ajira na hali duni ya maisha.

Salvador-Allende-1971.jpg

Salvador Allende ©Alpha History

Ilivyofika Septemba 11, 1973 nayo mapinduzi yakawadia, mapinduzi yaliyoongozwa na majeshi ya taifa, vikosi vya mataifa ya magharibi na wananchi. Mapinduzi yaliyomuondosha madarakani rais wa wakati huo Salvador Allende, kupitia mchakato huo naye Allende alijitoa uhai ndani ya ikulu iliyokuwa imezingirwa tayari.

Mapinduzi hayo yalifungua mlango na kuweka pazia, na pazia hii sio nyingine ni kiongozi wa kijeshi Bw. Augusto Pinochet aliyedhaniwa ndiye kumbe siye.

pinochet.jpg

Augusto Pinochet ©Alpha History

Katika utawala wa Augusto Pinochet aliyetambuliwa kama dikteta wa kijeshi alihakikisha hamna uhuru wa kutoa mawazo, kupeana wala kupashana habari, aliendeleza rushwa na ukiukwaji wa haki za binadamu, siasa za mlengo mmoja zilipaishwa na aliweza kuua, kupoteza au kuwaweka vifungoni jumla ya watu 3,000.

Uchumi, Biashara, Uwekezaji, Kilimo, Maendeleo na Utalii

Chile yenye uchumi imara na kiwango safi cha maisha inatambulika kama taifa lenye ushindani, kipato kikubwa, amani, uhuru wa kibiashara na kiwango kidogo cha rushwa.

Biashara, Uwekezaji na Kilimo ni chachu ya uchumi imara kwa Chile, ikiwa ni nyumbani kwa mgodi mkubwa wa shaba duniani ESCONDIDA. Huku uwekezaji ndani ya Chile ukichagizwa na viwanda vya saruji, vitambaa, mvinyo na bidhaa mbalimbali zenye soko kubwa katika mataifa ya Brasil, Japan, Uchina, Korea ya Kusini na Marekani.

Santiago-Chile-market.jpg

Vyakula katika soko la Las Vega, Concepción ©FromFarms

Kilimo kwa taifa ni moja ya sekta yenye kutoa ajira kwa asilimia 38% ya ajira zote, kilimo kikubwa ni chenye kulenga ngano, mahindi, viazi, maharage, vitunguu, mtama pamoja na ufugaji na uvuvi wa kisasa.

LATAM-Chile.jpeg

LATAM Chile (LATAM Airlines) ©Sam Chui

Maendeleo kwa Chile yameanza katika kila ngazi ya maisha huku miundombinu bora kuanzia barabara za rami, umeme, maji, reli na viwanja vya ndege. Chile yenye viwanja vya ndege nane vyenye hadhi ya kimataifa kuanzia Comodoro Arturo Marino Benítez Int. Airport (Santiago) nyumbani kwa Shirika la ndege la mataifa ya Latini ya Amerika (LATAM Airlines).

Atacam Desert.jpg

Jangwa la Atacam ©Nacíonal DCI

Utalii kwa taifa unachagizwa na uwepo wa kisiwa cha Easter 'Easter Island' chenye historia ya enzi na enzi, jangwa la Atacam - jangwa kavu zaidi duniani likiwa sehemu ya majaribio ya magari ya tafiti (Rovers) za sayari ya Mars.

Analagbo Pool.jpg

Bwawa la Algarrobo ©Guinness

Bwawa kubwa zaidi duniani la kuogelea Algarrobo linalopatikana jijini Algarrobo. Pia jengo refu zaidi Amerika ya Kusini Costanera Gran Torre.

1-Santiago-Chile.jpg

Costanera Gran Torre ©Itsbest travel

Elimu

Elimu kwa taifa ni ya kiwango cha juu ikiwa na asilimia 96% ya raia wenye elimu ya kati na fani mbalimbali huku ikiwa imegawanywa katika msingi, upili na elimu ya juu.

Elimu ya upili imetengwa mara mbili ndani ya miaka minne (Miaka miwili ikiwa elimu ya nadharia na miaka miwili elimu yenye kuleta maana katika fani za Sanaa, Sayansi, Ufundi na Kazi zenye mlengo wa jamii.

Elimu ya juu hutolewa katika vyuo bora mifano ya University of Chile, University of Concepción, University of Talca, University of Antofagasta, Universidad Mayor, Universidad Finish Terrae na Universidad de los Andes.

Michezo, Muziki na Filamu

Mchezo wa kitaifa ni Rodeo huku mchezo wenye wafuasi wengi ni mpira wa miguu unaowakilishwa vyema na timu ya taifa ya Chile na vilabu vya Colo - Colo na Universidad de Chile.

C Centanario.jpg

Timu ya taifa ya Chile wakisherehekea kutwaa ubingwa wa Copa América Centanario ©Clara Hugo

Chile bingwa mara mbili mfululizo wa mashindano ya Copa América ( Copa América 15 na Copa América Centanario ) mashindano yaliyokimulika kizazi bora cha Chile kuwahi kutokea, kizazi kilichokuwa na talanta ya uchakataji wa aina.

Alexis Sanchez.jpg

Alexis Sanchez ©Clara Hugo

Shehena ya wachezaji nguli mfano wa Alexis Sánchez, Arturo Vidal, Eduardo Vargas, Mauricio Isla, Charles Aranguiz, José Pedro Fuenzalida, Gonzalo Jara, Claudio Bravo na Gary Medel kwa uchache.

Kampuni ya uandaaji, uzalishaji na usambazaji wa filamu Andes Films ni chapa ya Chile ikiwa na waongozaji Pablo Larrain na Marcela Said.

Paloma Mami2.jpg

Paloma Mami ©Postas

Muziki unatambulishwa vyema na tamasha la kimataifa la muziki Festival de Viña del Mar na mdada Paloma Mami aliyetamba na nyimbo “No Te Enamores” na “Goteo” huku wakiwepo wasanii Newen Afrobeat, Moral Distaída na Villa Cariño.

Hii ndio Jamhuri ya Chile 🇨🇱
 
Jamhuri ya Chile | Republic of Chile au República de Chile

Chile
ni taifa linalopatikana bara la Amerika Kusini likiwa na mipaka baina ya Ajentina, Bolivia, Peru, milima ya Andes na bahari ya Pasifiki.

View attachment 1507625
Bendera ya Jamhuri ya Chile

Taifa hili lenye ukubwa wa Kilomita za mraba 756,950 sawa na maili za mraba 292,260 ni nyumbani kwa watu takribani millioni 19,121,776 kufikia Julai 14, 2020.

Kauli kuu ya taifa (Motto) ni “Kwa Haki au Nguvu” | “Por la razón o la fuerza”. Lugha rasmi ni Kihispaniola, pesa rasmi ni Peso ya Chile (CLP), Peso 1 ni sawa na Centavos 100.

View attachment 1507633
Jijini Santiago ©Chile Travel

Mji mkuu wa Chile ni Santiago mji wenye kuhodhi shughuli za kiserikali, biashara na mji wenye maendeleo zaidi ndani ya Chile.

View attachment 1507634
Jijini Valparaíso ©ValparaísoEn

Miji mingine iliyokuwa bora ni Valparaíso, Concepción, La Serena, Iquique, Antofagasta, Punta Arenas, Valdívia, Talca, Puerto Montt, Coquimbo, Rancagua na Temuco.

Historia ya Kati ndani ya taifa

Chile iliyopitia misukosuko na machafuko mbalimbali sehemu yenye historia ya mapinduzi, mnamo miaka ya 1960 na 1970 vuguvugu zito lilipamba moto kutokana na Chile ya wakati huo kutokuwa na matumaini, furaha wala faraja baina ya WaChile walioathirika na ukiukwaji wa haki za binadamu, siasa za mlengo mmoja, rushwa, ukosefu wa ajira na hali duni ya maisha.

View attachment 1507712
Salvador Allende ©Alpha History

Ilivyofika Septemba 11, 1973 nayo mapinduzi yakawadia, mapinduzi yaliyoongozwa na majeshi ya taifa, vikosi vya mataifa ya magharibi na wananchi. Mapinduzi yaliyomuondosha madarakani rais wa wakati huo Salvador Allende, kupitia mchakato huo naye Allende alijitoa uhai ndani ya ikulu iliyokuwa imezingirwa tayari.

Mapinduzi hayo yalifungua mlango na kuweka pazia, na pazia hii sio nyingine ni kiongozi wa kijeshi Bw. Augusto Pinochet aliyedhaniwa ndiye kumbe siye.

View attachment 1507710
Augusto Pinochet ©Alpha History

Katika utawala wa Augusto Pinochet aliyetambuliwa kama dikteta wa kijeshi alihakikisha hamna uhuru wa kutoa mawazo, kupeana wala kupashana habari, aliendeleza rushwa na ukiukwaji wa haki za binadamu, siasa za mlengo mmoja zilipaishwa na aliweza kuua, kupoteza au kuwaweka vifungoni jumla ya watu 3,000.

Uchumi, Biashara, Uwekezaji, Kilimo, Maendeleo na Utalii

Chile yenye uchumi imara na kiwango safi cha maisha inatambulika kama taifa lenye ushindani, kipato kikubwa, amani, uhuru wa kibiashara na kiwango kidogo cha rushwa.

Biashara, Uwekezaji na Kilimo ni chachu ya uchumi imara kwa Chile, ikiwa ni nyumbani kwa mgodi mkubwa wa shaba duniani ESCONDIDA. Huku uwekezaji ndani ya Chile ukichagizwa na viwanda vya saruji, vitambaa, mvinyo na bidhaa mbalimbali zenye soko kubwa katika mataifa ya Brasil, Japan, Uchina, Korea ya Kusini na Marekani.

View attachment 1507714
Vyakula katika soko la Las Vega, Concepción ©FromFarms

Kilimo kwa taifa ni moja ya sekta yenye kutoa ajira kwa asilimia 38% ya ajira zote, kilimo kikubwa ni chenye kulenga ngano, mahindi, viazi, maharage, vitunguu, mtama pamoja na ufugaji na uvuvi wa kisasa.

View attachment 1507715
LATAM Chile (LATAM Airlines) ©Sam Chui

Maendeleo kwa Chile yameanza katika kila ngazi ya maisha huku miundombinu bora kuanzia barabara za rami, umeme, maji, reli na viwanja vya ndege. Chile yenye viwanja vya ndege nane vyenye hadhi ya kimataifa kuanzia Comodoro Arturo Marino Benítez Int. Airport (Santiago) nyumbani kwa Shirika la ndege la mataifa ya Latini ya Amerika (LATAM Airlines).

View attachment 1507635
Jangwa la Atacam ©Nacíonal DCI

Utalii kwa taifa unachagizwa na uwepo wa kisiwa cha Easter 'Easter Island' chenye historia ya enzi na enzi, jangwa la Atacam - jangwa kavu zaidi duniani likiwa sehemu ya majaribio ya magari ya tafiti (Rovers) za sayari ya Mars.

View attachment 1507643
Bwawa la Algarrobo ©Guinness

Bwawa kubwa zaidi duniani la kuogelea Algarrobo linalopatikana jijini Algarrobo. Pia jengo refu zaidi Amerika ya Kusini Costanera Gran Torre.

View attachment 1507724
Costanera Gran Torre ©Itsbest travel

Elimu

Elimu kwa taifa ni ya kiwango cha juu ikiwa na asilimia 96% ya raia wenye elimu ya kati na fani mbalimbali huku ikiwa imegawanywa katika msingi, upili na elimu ya juu.

Elimu ya upili imetengwa mara mbili ndani ya miaka minne (Miaka miwili ikiwa elimu ya nadharia na miaka miwili elimu yenye kuleta maana katika fani za Sanaa, Sayansi, Ufundi na Kazi zenye mlengo wa jamii.

Elimu ya juu hutolewa katika vyuo bora mifano ya University of Chile, University of Concepción, University of Talca, University of Antofagasta, Universidad Mayor, Universidad Finish Terrae na Universidad de los Andes.

Michezo, Muziki na Filamu

Mchezo wa kitaifa ni Rodeo huku mchezo wenye wafuasi wengi ni mpira wa miguu unaowakilishwa vyema na timu ya taifa ya Chile na vilabu vya Colo - Colo na Universidad de Chile.

View attachment 1507716
Timu ya taifa ya Chile wakisherehekea kutwaa ubingwa wa Copa América Centanario ©Clara Hugo

Chile bingwa mara mbili mfululizo wa mashindano ya Copa América ( Copa América 15 na Copa América Centanario ) mashindano yaliyokimulika kizazi bora cha Chile kuwahi kutokea, kizazi kilichokuwa na talanta ya uchakataji wa aina.

View attachment 1507719
Alexis Sanchez ©Clara Hugo

Shehena ya wachezaji nguli mfano wa Alexis Sánchez, Arturo Vidal, Eduardo Vargas, Mauricio Isla, Charles Aranguiz, José Pedro Fuenzalida, Gonzalo Jara, Claudio Bravo na Gary Medel kwa uchache.

Kampuni ya uandaaji, uzalishaji na usambazaji wa filamu Andes Films ni chapa ya Chile ikiwa na waongozaji Pablo Larrain na Marcela Said.

View attachment 1507654
Paloma Mami ©Postas

Muziki unatambulishwa vyema na tamasha la kimataifa la muziki Festival de Viña del Mar na mdada Paloma Mami aliyetamba na nyimbo “No Te Enamores” na “Goteo” huku wakiwepo wasanii Newen Afrobeat, Moral Distaída na Villa Cariño.

Hii ndio Jamhuri ya Chile 🇨🇱
Mimi nitasema ninayo ndoto ya kuzunguka dunia nzima. Ila kwa America ya kusini ndoto yangu kuu ni kufika Colombia. Lakini kipindi nitakachotembelea Colombia basi Chile itanibidi nifike pia.

Jangwa la Atacama ni miongoni mwa majangwa ya ajabu zaidi duniani na research mbali mbali pia hufanyika huko
 
Natumai utafanikisha kutimiza malengo yako kwa Colombia na Chile. Colombia Virtual Tour Jamhuri ya Colombia | República de Colombia
-
Moja ya maajabu ya Atacama ni jua wakati mwingine kuonekana lenye rangi ya bluu.
 
Back
Top Bottom