Jamhuri ya Wapambanaji FC

Jamhuri ya Wapambanaji FC

MwanaWA Ebrania

JF-Expert Member
Joined
Oct 6, 2017
Posts
939
Reaction score
1,147
CLUB YETU YA JAMUHURI YA WAPAMBANAJI FC INAYOUNDWA NA WATOTO PAMOJA NA VIJANA WAISHIO MAZINGIRA HATARISHI (MTAANI) IKIWA MAZOEZINI KWENYE UWANJA WAKE WA NYUMBANI MAKONGO JUU, WILAYA YA KINONDONI - DAR ES SALAAM. LENGO KUU LA CLUB HIYO KUTOA ELIMU YA MALEZI BORA KUANZIA NGAZI YA FAMILIA ILI KUMALIZA ONGEZEKO LA WATOTO WAISHIO MITAANI.... CLUB HIYO INAUHITAJI WA SALE/JEZI PAMOJA NA MIPIRA YA KUCHEZEA...

Mipango ya Club ni mingi sana, ikiwemo kuwajengea uwezo wa kuyachukia maisha ya mtaani, wengi wao wanabadilika na kuomba kuunganishwa na familia zao, maana kuna baadhi ya watoto waliondoka kwa wazazi /walezi wao kwa sababu mbalimbali Wengine Umaskini, wengine vipigo na manyanyaso, wengine hofu na vitisho hasa baada ya kujihisi wametenda makosa ambayo wanajua wazazi / walezi wao watawaadhibu pamoja na mengine mengi kama hayo ikiwemo kutupwa kama mimi nilivyotupwa nikiwa mchanga wa siku moja.

Watoto wengine tunawaunganisha na Makao za kulelea watoto na wale watoto wenye vipaji tunawaendeleza ili waviishi vipaji wslivyonavyo. Kwa muda mfupi tu tangu tumeanza harakati za maswala ya kuupinga Ukatili wanaofanyiwa watoto waishio mitaani kwa kushirikiana na maafisa Ustawi wa Jamii, Tumefanikiwa kupunguza sana ongezeko la watoto waishio Mitaani kwa mkoa wetu wa Dar Es Salaam.

Kama wewe ni mzoefu jiji la Dar Es Salaam utakuwa unajua hilo, Miaka Miwili iliyopita, ukishuka pale Posta Mpya, Kisutu, CBE, IFM, Ferry, Station, Kisutu, utapokelewa na kundi kubwa la watoto wanaokuzunguka kwa ajili ya kuomba-omba uwape chochote, kwa sasa nafikiri unaona lile kundi lote halipo, mjini kuko shwari. Hiyo ndio kitu tunakifanya ili kuwasaidia watoto hao.

Karibuni sana wapenzi wa sports kuangalia vipaji vipya vya Soccer kutoka kwa vijana wanaoishi mazingira magumu.

View attachment 2557404

DSC_2880.JPG
 
Back
Top Bottom