BAKIIF Islamic
JF-Expert Member
- Jul 11, 2021
- 600
- 1,843
Ina idadi ya watu ya milioni kumi na moja na eneo la maili mraba 190,000. Ndio eneo pekee la peninsula hii linalopata mvua za monsuni, na kuifanya sehemu yenye rutba sana na yenye watu wengi.
Mlima mrefu sana wa Arabia, uitwao an-Nabi Shu’aib, uko Yemen na unafikia urefu wa futi 12,350.
Sana’a ndio makao makuu na mji mkubwa zaidi katika nchi hii. Upo katika muinuko wa futi 7200, na unafahamika kwa hali yake ya hewa ya kiafya nzuri.
Aden ndio mji mkuu wa kibiashara. Al-Mocha, Al-Huhaydah, Ta’izz na Mukalla ni miji mingine mikuu. Sayun na Shibam ni miji ambayo ni maarufu kwa magorofa yake marefu.