mambo vipi waungwana naombeni munisaidie nitampataje mpenzi wa kweli
nipo katiaka harakati za kumtafuta mchumba nisaidieni:flypig:
Swali zuri Mwanangu, Angalia sana na uombe Mungu akutangulie katika kuchagua. Jua kwamba, unakwenda kuchagua mtu ambaye utaishi naye kwa maisha yako yote yaliyosalia hapa duniani. Hivyo umakini mkubwa unahitajika, pamoja na kumtanguliza Mungu katika kuchagua. Wengi wamefanya makosa katika hatua hii muhimu, na baadaye kuishia kujilaumu. Baadhi ya Vigezo katika kuchagua mwenzi wako wa maisha, jaribu kuzingatia yafuatayo:-
A-Age:- Mwanaume lazima awe na umri mkubwa kuliko mwanamke. Hii ni kwa sababu akili ya mwanamke hukomaa mapema kabla ya akili ya mwanaume. Iwapo watakuwa na umri sawa, mwanamke atakuwa ana akilipevu mbele ya mwanaume na hivyo hawataendena hii itapelekea ugomvi kutatokea. Nakushauri mwanaume amzidi mwanamke kwa miaka si chini ya 5 na si zaidi ya 15.
B- Beaut:- Haiba: Hii hushauriwi wala kushawishiwa na mtu. kaa na chunguza kama mwenzi wako anakupendeza machoni kiasi kuwa hutamwonea haya kumtambulisha kwa ndugu,jamaa na marafiki zako. Wapo watu wanaona aibu hata kutembea barabarani na wenzi wao, kwa kuwa wanaona haiba zao haziendani. Hii inafanya kujuta katika ndoa.
C- Charming:-Uchangamfu:- Mwanamke ana sifa ya kuwa mkaribishaji wa wageni katika nyumba. zipo baadhi ya nyumba ambazo wageni wanapofika, baba huhangaika kukaribisha wageni wakati mama amekaa, kanuna, kama vile kala sumu. Hii ni tatizo katika familia
D- Diseases:- Chagua mwenzi ambaye hana sifa za kuugua mara kwa mara. Kuugua ni kawaida, lakini wapo watu ambao mwezi hauishi bila kulazwa hospitali. Achana na hao.
E- Education:-Mwanaume anatakiwa awe na Elimu ya juu kuliko mwanamke: Ingawa haitakiwi wazidiane sana. Kama mwanaume ana Masters, basi mwanamke awe na Bachelor. Hii itasaidia kuwa na mtazamo angalau unao shabihiana. nyumba nyingi zimepata matatizo kwa kuwa na wanandoa wenye wigo mpana wa elimu
F - Family welfare:-Tafuta mwenzi, ambaye hali ya maisha ya nyumbani hayatofautiani sana. Hii ni kwa sababu ndoa huunganisha familia mbili. hivyo familia hizi zisipo fanana, taabu hutokea
G- Genetic diseases:- Chunguza magonjwa ya kurithi, kama vile Albinism, circle cell etc.
Naomba niishie hapo kwa leo, na kama utakuwa interrested, nijuze niendelee.