BigTall
JF-Expert Member
- Mar 9, 2022
- 525
- 1,257
Jamii imetakiwa kujikinga magonjwa ya mlipuko ikiwepo kufuata miongozo na elimu inayotolewa kwa umma katika kuongeza uelewa na kujenga utayari wa kukabiliana na magonjwa ya mlipuko.
Hayo yamesemwa Aprili 15, 2022 na Mratibu wa Elimu kwa Umma na Ushirikishaji Jamii wakati wa dharura Dkt. Tumaini Haonga wakati wa kikao kazi kinachofanyika Mkoani Morogoro.
Kikao kazi hicho kinahusu uandaaji wa mwongozo wa elimu kwa umma, uhamasishaji na ushirikishaji jamii wakati wa kukabiliana na magonjwa ya mlipuko.
"Tunatarajia baada ya mwongozo kukamilika, tutaboresha uratibu na kuainisha afua za kipaumbele kutekelezwa kwa ngazi mbalimbali, uhamasishaji na utoaji elimu kwa umma katika kujiandaa na kukabiliana na magonjwa mbalimbali ya mlipuko ikiwemo UVIKO-19 na Kipindupindu" Amesema Dkt. Haonga
Pia, Dkt. Haonga amesema wanatarajia kuona ushiriki wa wadau, sekta binafsi, viongozi wa serikali na ngazi ya jamii, watu mashuhuri pamoja na makundi ya kijamii kuendelea kutoa elimu kwa umma juu ya magonjwa ya mlipuko hususan kuongeza kasi ya utoaji wa chanjo dhidi ya UVIKO-19.
Kikao kazi hicho kimekutanisha Wataalamu mbalimbali kutoka Wizara ya Afya Kitengo cha Elimu ya Afya kwa Umma, Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, OR - TAMISEMI, Taasisi za Elimu, Ofisi ya Mganga Mkuu Mkoa wa Morogoro pamoja na wawakilishi wa makundi ya kijamii.