Jamii inakuwa na mategemeo makubwa sana kwa kijana mwenye digrii kiasi cha kumfanya abague baadhi ya kazi

Jamii inakuwa na mategemeo makubwa sana kwa kijana mwenye digrii kiasi cha kumfanya abague baadhi ya kazi

Attack

JF-Expert Member
Joined
Jun 29, 2022
Posts
894
Reaction score
1,608
Habari,

Je, hii ni sawa kwamba Baba Yako ameuza mchicha na kuni na wewe graduate uuze maji na kuni? Moja ya changamoto ya jamii nyingi zinapelekea vijana wengi kuwa na msongo Kwa sababu Kila anachofanya msomi unasikia, eti mtu ana degree anauza mchicha? Mtu ana degree anafanya hivi? Guys? Acheni hii tabia!

Katika upande wa pili wa shilingi Kuna familia Moja kwenye kitabu Cha RICH DAD AND POOR DAD, imenivutia sana kuitafakari;

Story Iko ivi ,Kuna familia Moja ROBERT KIYOSAKI ANAISIMULIA, kwamba kulikuwa na baba wa familia hiyo ambae alikuwa anauza maji, basi Kwa kupitia maji kasomesha watoto hadi vyuo , ila watoto walipokuwa wanakuja likizo aliwahimiza kwamba wasombe maji ya kuuza Kwa sababu yeye umri unaenda badae huo mradi utakuwa wao.

- Watoto walionekana kutokufurahishwa na mradi wa baba Yao wa kusomba maji Kwa kichwa kuisambazia jamii kama biashara, Mzee alisisitiza sana wajitume wasije kuuwa mradi.

Basi siku Moja Kijiji kikatoa zabuni Kwa atakae weza kusambaza maji kijijini, Basi Mzee nae aliomba hiyo nafasi akidai kwamba ataweka sehemu tank halafu atasomba yeye na familia yake isipokuwa wikendi na watu watachota, kulingana na yeye ni mzoefu wa kazi, wanakijiji hawaamini kama Kuna njia mmbadala walipiga makofi.

- Badae kijana msomi akapewa nafasi na yeye akasema ,yeye ameandaa business plan amepata wadhamini atasambaza mabomba ya maji Kwa Kila familia na Kila mtu atapata maji masaa 24 Kwa ghalama ndogo kuliko mzee, watu wakasema hii ndo Bora zaidi.

Turudi kwenye swali je jamii inataka kijana msomi aje na mbinu mpya ya biashara kuliko walizozizoea? Kama ni ndiyo mashirika ya watu binafsi, serikali dhaminini hawa vijana.
 
Turudi kwenye swali je jamii inataka kijana msomi aje na mbinu mpya ya biashara kuliko walizozizoea? Kama ni ndiyo mashirika ya watu binafsi, serikali dhaminini hawa vijana.
Hii ni yetu vijana tuandae business plans kama hatuna mitaji ( mwenye wazo na asie na wazo ila anapesa tuungane kutimiza kile kilicho cha muhimu kama alivyo sema SHIGONG'O katika kitabu cha jinsi ya kutoka katika umasikini hadi mafanikio)
 
😂😂😂 umenichekesha sana. Kama ilivyoada, tunategemea elimu kuwa ni investment (na ndio maana wazazi wakawasomeasha watoto wao). Dhana ya kuondoa Ujinga na kupanuka kifikra pia ipo. Lakini hadi ngazi ya Degree ujue ushapoteza kati ya Miaka 17 mpaka 20. Hili jambo hulioni?

Kumbuka pia elimu kwa mnajili wake ni mahususi kuwaandaa vijana kuwa (skilled labour). Sio kumfanya awe mfanyabiashara, na ukimsoma huyo huyo Kiyosaki atakueleza vyema ni kwa jinsi Gani hili Tabaka la waajiriwa linavyokamuliwa vilivyo.

Lakini tatu, tukumbuke kuwa kuuza mchicha sio dhambi, lakini usilikuze jambo, nikimaanisha sio lazima wote wakubali kuwa wafanyabiashara Wadogo, Hilo si lengo la Kila mtu, wengine wanataka kuspecialize kwenye jambo waliolotumia karibia sudusi ya maisha yao katika kuisaka hiyo elimu. Usifanye elimu kuwa cheap (huu ni mtazamo wako)

Wote tunaweza kuwa na kazi, lakini wote hatuwezi kuwa wafanyabiashara
 
Back
Top Bottom