SoC03 Jamii na isikie

SoC03 Jamii na isikie

Stories of Change - 2023 Competition

Mbwilo jr

New Member
Joined
Jun 28, 2023
Posts
2
Reaction score
1
Hii ni mara yangu ya kwanza kupanda katika jukwaa hili la story of change nia na madhumuni sio tu kushindana ila kupaza sauti kwa jamii.

Jamii ni nini? Isikie nini? Chanzo chake nini? Na nini kifanyike? Huu n mgawanyo wa story yangu katika shindano hili la story of change 2023.

Jamii ni nini?..
Jamii ni watu wanaokaa pamoja na kushirikiana kwa mambo mbalimbali, kwa mfano masuala ya afya, elimu na ulinzi: mambo hayo yanapowakutanisha watu hujenga kitu kinachoitwa jamii, jamii hujenga umoja na upendo baina ya watu husika.

Jamii bora inahitaji watu wenye upendo: watu wakipendana huweza kuishi na kujenga jamii bora, hivyo ni vyema watu wa sehemu husika wapendane ili waweze kujenga jamii ya namna hiyo.

Isikie nini?
Leo nataman jamii hii isikie huu ya mambo haya
1. Kumekua na ongezeko kubwa la watoto wa mitaani
2. Ukatili na unyasaji wa kijinsia unazidi kukua
3. Mambo mengi mabaya yanazidi kuongezeka kwa kasi mnoo.

Chanzo chake ni nini?
kama nilivyotangulia kusema hapo awali jamii inajumuisha upended na ushirikiano baina ya watu na watu hasa wanaoyuzunguka, lakini haipo hvyo tena tumezungukwa na watu tunochukiana nao wakati mwengine bila hata sababu hvyo nina thubutu kusema chanzo cha haya yote ni kukosa upendo, kushirikina na vitu vinavyoendana na hivyo.

Nini kifanyike.
Hatuwezi kutokomeza ukatili wa kijinsia kwa kufungana miaka 30 au hata maisha kama hatutoweza kupanda mbegu ya upendo tangu watoto wetu, zamani, desturi na mila zetu zilitufundisha maadili yaliyo safi kanla hatujaamua kuufuata ulimwengu.

Natamani jamii isikie juu ya kujaliana, kuwalea watoto wa watu wengne kama tunavyolea wa kwetu, wakiwa na maadil yenye kumcha na kumpendeza Mungu, hatuitaji Biblia wala Quran kuyatambua haya, jamii tubadilike.

JAMII NA ISIKIE 🙏
 
Upvote 1
Kura yangu unayooo, [emoji122][emoji122][emoji122]
 
Back
Top Bottom