SoC01 Jamii ya kidijitali;Kuna jambo halipo sawa

SoC01 Jamii ya kidijitali;Kuna jambo halipo sawa

Stories of Change - 2021 Competition

Apollo one spaceship

JF-Expert Member
Joined
Jan 28, 2021
Posts
245
Reaction score
457
Kijana wa kidijitali anaamka asubuhi na mapema.
Badala ya sala,kijana huyu anachukua simu yake na kuwasha data.
Hapa ndipo ratiba ya kijana huyu inapoanza.

[emoji3578]Anaingia Instagram.
Hapa anatumia masaa kadhaa kuangalia umbea wa siku hiyo.Atajiposti,atalike,atadislike,atafollow,atatafuta followers, atacomment matusi,atascroll hata kama hana lengo maalum ilimuradi tu anapekua.

[emoji3578] Baada ya insta ataingia WhatsApp
Hapa atatumia masaa kadhaa kuangalia status.Kisha ataingia kwenye magrupu ya ngono,mipira,urembo na mengine ya ajabu.Huku atasoma sms,atadownload video,picha nk.Kisha ataangalia sms alizotumiwa na marafiki,wapenzi wake.Hapa itamchukua masaa mengi tu.

[emoji3578]Kisha ataingia Facebook.
Huku atascroll,ataangalia posts za watu,atapost,atalike,atashare, atafollow,atacomment matusi.Kisha ataenda messenger kuangalia sms za mapenzi.Hii itaconsume time ya kutosha tu.Ataingia kwenye magrupu and so on and so forth.

[emoji3578]Kisha ataingia Twitter.
Huku atatamani stori za kina kigogo,kina Tundu Lissu,nk.Atascroll,atafuatilia vichekesho na upuuzi wa kina madenge, atascroll,atatamani kila taarifa isimpite,atatafuta followers, atafollow nk.

[emoji3578]Then Anaingia Jamii Forum
Huku kuna nyuzi za maana kama uchumi,sheria lakini kijana huyu atatumia masaa mengi kwenye kuangalia makalio kwenye nyuzi za warembo worldwide,atasimulia uzinzi na uasherati wake kwenye uzi wa kula kimasihara.Atazidi kuonesha ulimbukeni kwa kucomment matusi kwenye nyuzi za maana.

[emoji3578]Paap!!! Ataingia app ya photos kucheki picha zake za zamani,za warembo,ma-ex wake.atacheki short videos,atashare picha hizo fb,tssap,insta,twitter nk.That is time.

[emoji3578]Mbiooo ataenda telegram.
Huku ataangalia chats,atachek magrupu ya ngono,na vitu vingine vya kipuuzi.

[emoji3578]Kisha Tiktok.Atascroll,atachek picha za kijinga,video za hovyo,umbea, vichekesho vya hovyohovyo nk

[emoji3578] Huyooooooo Snapchat,atabinua makalio,atajifilter.Atarembua macho ya uzinzi,aisee!!!!!!

[emoji3578]Paap ataenda app ya normal message kucheki miamala ya kutuma na ya kutolea,atacheki sms za wenye vinokia tochi, Waganga wa kienyeji nk.


[emoji3578] Ataenda Camera app kupiga picha makalio na six pack zake.Aisee!!!!!


[emoji3578]Kisha ataenda sofascore,fotmob,goal-live then betpawa, sportpesa,betika, sportybet,mbet nk.Atatumia masaa mengi kuanaalyse kutupoa mikeka.


[emoji3578] Anaingia YouTube.
Huku atacheki video kwa masaa mengi.Atafollow,ata-upload,ata like,dislike nk

[emoji3578]Then ataenda Gmail kuangalia new email and spams.Atabonyeza vilink kadhaa nk.

[emoji3578]Then ataenda calls and contacts.Atapiga simu na kuongea umbea dkk au masaa.

[emoji3578]Bado hajaenda onlyfans, LinkedIn, Google,chrome,settings, notification bar ambazo zinaconsume muda mwingi tu

[emoji3578]Bado kijana anawaza mapenzi,anawaza utajiri,anawaza ma-ex,sehemu za starehe Kama beach, bar,kucheki mechi.

[emoji3578]Halafu kijana huyu atalalamika uhaba wa ajira,ataombaomba wazazi ilhali ashakua

EWE KIJANA
[emoji120]If you don't stand for something, you will fall for everything.Huwezi ukajua vitu vyote duniani kwa siku moja,kubali Mambo mengine yakupite tu hasa umbea.Kuwa na msimamo kwa kuwa na kiasi kwenye matumizi ya mitandao ya kijamii.Kwenye maisha halisi ni sawa na kufanya kazi kupitiliza au kufanya kazi tofauti tofauti kwa papara na kwa muda mmoja bila lengo maalum
Hii inakula nguvu zako tu bila kutimiza chochote cha maana.

Application au software nyingi za simu au tarakilishi zinakudanganya kwa kuwa hauvuji jasho ukiwa unazitumia lakini zinaconsume plenty of time bila kunotice.

#Remember to be productive in social network NOT BUSY.

NB:Jinsi ya kuwa productive kwenye mitandao ya kijamii.
*Jifunze blogging, jifunze freelance,uza bidhaa online,fanya manunuzi, fuatilia taarifa za kiuchumi,masoko,soma educational documents.

Tuwe na kiasi kwenye mambo yote.

#Asanteni sana#
 
Upvote 3
Haya mambo wakati mwingine yanakuwa influenced na umri wa mtu, kwa under eighteen hasa wale waliomaliza form four wengi wanakuwa na tabia hizo, kwasababu wanaisikiliza zaidi miili yao na ndio inawaamrisha nini wafanye.

Kwasababu hawa wanakuwa chini ya utawala au himaya ya wazazi wao, wengi hujikuta wako idle muda mwingi hawana kazi maalum za kufanya, mfano wanasubiri matokeo ya mitihaninyao ya kumaliza shule, na hawana pressure ya kujitafutia riziki.

Hivyo automatically hujikuta wanageukia simu zao na bahati mbaya siku hizi smartphones zimekuwa nyingi zaidi ya vitochi baada ya kuondolewa kodi ya uingizaji nchini, na kuangalia kile ambacho miili yao inawatuma.

Kwa watu wazima wenye majukumu kufuatilia hayo mambo kupitiliza ni jambo la kusikitisha zaidi, hawa wanatakiwa kuelekeza muda wao mwingi kwenye uzalishaji kwa ajili ya kuzikimu familia zao.

Kwa kawaida binadamu anaongozwa na viwili, either mwili au roho, kutegemeana na malezi ya muhusika na vile alivyoamua kuchagua mtindo wa maisha yake aenende vipi.

Wapo watoto/watu wazima ambao wamekuzwa kwa misingi ya kiroho hawa hujikuta wanafuata njia za wazazi wao ambao kimsingi ni mafundisho ya kwenye vitabu vitakatifu, lakini pia wapo wale ambao hawajakuzwa kwa mtindo huo, hawa ndio huingia zaidi kwenye mtego ulioandika mleta mada.

What should be done simply to avoid this, pawepo na namna ya wazazi kuwafundisha malezi ya kiroho watoto wao, wamjue, kumpenda na kumuogopa Mungu, then after, baada ya hapo, wawatafutie watoto wao jambo la kufanya wanapomaliza masomo yao, ili wasikae mitaani na kujiingiza kwenye makundi yanayosababisha kuwabadili tabia zao.

Kwa wale ambao bado wako mashuleni, ningependa pawepo na muda maalum wa kumuacha mtoto amiliki simu, anapokuwa na simu na wakati mwingine huenda nazo shuleni, hii husababisha wafanye uliyoandika pale juu kwa urahisi zaidi.

Lakini kama watabanwa kwenye kumiliki simu, na wabanwe tena kwenye matumizi ya hizo simu, naamini kwa kiasi fulani itasaidia kupunguza tatizo na kuongeza viwango vyao vya ufaulu darasani.

Tabia ya kumaliza shule na kuzurura mtaani huwa ndio mtego mbaya zaidi, wengi hupata mimba zisizotarajiwa, wa kiume hujiingiza kwenye matendo ya uhalifu ikiwemo uvutaji unga na bangi, ambayo mwishowe huweza kuharibu future zao moja kwa moja.
 
KWENYE ANY SITUATION HUWA SITOKI KAPA .

NIMEJIFUNZA KITU KIKUBWA .

BUT UMEWAKUNA KUNAKO.
 
Back
Top Bottom