Shayu
Platinum Member
- May 24, 2011
- 608
- 1,655
Viongozi wetu ni muhimu sana kujiepusha na kufanya biashara kama wanataka kuongoza taifa hili vyema, huwezi kuviweka vitu hivi pamoja na vikafanya kazi katika ufanisi wa hali ya juu. (Uongozi + biashara).
Hutaepuka kuwa fisadi, hutaweza kusimamia haki kwa watu. Asili ya biashara ni (uroho) wa kupata faida, na ukiwa madarakani na wakati huo huo unafanya biashara kuna hatari ya kufisadi taifa.
Viongozi wetu ni muhimu sana wasiwe wafanyabiashara na wategemee mishahara tu wanayopewa na taifa na mafao baada ya kustaafu kwao, wakitoka kwenye uongozi wawe huru kufanya wanachotaka, kuna hatari kubwa sana kama viongozi wetu watakuwa wafanyabiashara nchi yetu itaharibika na kupoteza mwelekeo wake. kwasababu asili ya biashara ni uroho wa faida na serikali itaweza kuwasimamia ikiwa tu, wakiwa nje ya siasa na uongozi, na ikiwa viongozi wetu wakiwa sio wafanyabiashara.
Viongozi wetu wakiwa wafanyabiashara hakuna haki itakayosimamiwa. Wafanyabiashara lazima wakae nje ya siasa, wakiwa ndani ya siasa wananchi wa taifa hili hawatoweza kuwa huru. Wataendelea kuwa watumwa tu na watu wa kutumika kwa maslahi ya wachache.
Uhuru wa watu wetu utakuwepo ikiwa wafanyabiashara wakiwa nje ya siasa. Jiulize kwanini mfanyabiashara atake kuwa kiongozi?? Mfanyabiashara hawezi kuwa kiongozi na kamwe hatoweza kuangalia watu wa chini na maskini. Tabia yake ni kujikusanyia kadiri anavyoweza na mtu huyu (Mfanyabiashara) anatakiwa kusimamiwa na serikali ya watu wasio wafanyabiashara ili kudhibiti uroho wake.
Jamii ambayo viongozi wake ni wafanyabiashara ni jamii ambayo ni corrupt ambayo haiangalii utu bali faida ya mali. Kwahiyo ni muhimu kwa wafanyabiashara kuwekwa nje ya siasa na watu wakawaida waongoze Taifa. Madaraka wapewe watu wa kawaida. watu wa kawaida wenye maadili ya kutosha ya kuongoza watu. watu waliotosheka na wasio walafi.
Kuna watu wanafikiri watu matajiri na wenye pesa hawatoiba ukiwapa uongozi, na maskini kwakuwa hawana kitu wataiba, hii sio kweli. Chanzo cha kuiba ni uroho na kutotosheka. Mtu mroho hatosheki na alichonacho hata awe na kiasi gani, hata umpe dunia nzima hatotosheka. Uroho hauna mipaka. Kuiba au kutokuiba kunategemea maadili ya mtu. Kuna maskini lakini wanaishi maisha ya uaminifu. Kwahiyo tunapochagua kiongozi wetu ni lazima na ni muhimu kufikiria mambo mengi sana.
Tunahitaji mtu mwenye maadili ya kutosha kutuongoza. Maadili yetu kama mtu mmoja mmoja na kama taifa yanategemea sana aina ya kiongozi tutakayemweka madarakani. Mtu mwenye maadili atachagua baraza la mawaziri lenye maadili na watu waliomzunguka kuwa wenye maadili, na mtu mwovu hivyo hivyo. Kumbukeni nuru na giza haviwezi kukaa pamoja. Kwahiyo tukichagua kiongozi mwovu tutegemee taifa la watu waovu. Mpera hauwezi kuzaa maembe. That is impossible.
Kwahiyo integrity ya nchi hii itategemea watu tutakaowaweka madarakani. Nawaambia haya kwasababu tunaelekea katika uchaguzi na nchi yetu imegubikwa na mambo mengi sana ambayo si sahihi. Taswira ya nchi yetu imeharibika kwa mauaji ya albino. Kuna mgawanyiko kwenye taifa letu ambao unahitaji mtu makini mwenye uwezo wa kuleta taifa hili pamoja na kuunda upya maadili ya taifa letu.
Hatuwezi kuunda taifa bila maadili. Kwahiyo ni muhimu taifa letu kurudi katika mstari wa maadili hatuwezi kuendelea pasipo maadili. Turudishe upya utawala wa sheria na order katika taifa letu. Turudishe upya nidhamu. Tunahitaji kuhuisha upya taifa letu na kuleta matumaini mapya na umoja kwa watu wetu wote.
Ubinafsi ambao umemea ndani kabisa ya moyo wa taifa letu ni lazima ukomeshwe tulete kutumikia kwa taifa letu. Kuna matumaini makubwa kama tutabadilika na amani ya kweli itapatikana kama tukizingatia haya mambo. Amani na utulivu wa moyo sio ya kutokuwepo na vita tu.
Ni muhimu sana kutenganisha biashara na uongozi ili tupate mwelekeo kama taifa. Uongozi hauhitaji mtu anayeingia madarakani kupata faida, unahitaji mtu anayeingia madarakani kutumikia. Mfanyabiashara hawezi kutetea maskini anaangalia maslahi yake. kwahiyo wafanyabiashara wakiingia kwenye siasa tegemea maadili ya taifa kuyumba. Ni watu wanaotakiwa kukaa nje ya siasa na kudhibitiwa na serikali.
Matatizo haya yameikumba CCM ambayo ilikuwa inajinadi ni chama cha wakulima na wafanyakazi kilianza vizuri na sasa inaharibu, sababu ya kuchanganya biashara na siasa. Kwasababu ya kuwakumbatia wafanyabiashara na kuwadharau common people.
Pale ambapo watu wengi ambao ni maskini wanapodharauliwa na kuwakumbatia matajiri, kuna hatari kubwa. Lazima kuwe na balance katika nchi kati ya maskini na matajiri pamoja na watu wa kipato cha kati. Kadiri muda unavyokwenda na maisha yanavyoendelea kuwa magumu na uwiano kati ya maskini na matajiri unavyoongezeka ndivyo CCM itakavyoendelea kupata tabu.
Serikali yeyote inaposahau kuangalia watu na kujikita katika kujilimbikizia mali inakosa ushawishi kwa wananchi na ni hatua moja kubwa ya kuifanya serikali hiyo kuwa ya ukandamizaji.
Kwahiyo ni dhahiri kwamba serikali ya CCM ikiendelea na tabia hii huenda tukawa na chama cha kikandamizaji na cha kidikteta. Kiongozi hapaswi kujilimbikizia mali atasahau haki za raia na kuwakandamiza. Ndio haya tunayo yaona katika CCM. Hawaonyeshi mfano wa maadili kwa watu wa taifa hili. Tulitegemea wao wawe mfano. Wananchi wa taifa hili hawapaswi ku support chama ambacho kimekosa maadili. Chama ambacho hakilei vijana katika maadili bora ambayo yatasababisha taifa hili kuendelea. Iangalie CCM ilivyo sasa hivi !
''Siku hizi kuna wao na sisi'' Tabaka la viongozi na walalahoi! Hawajali elimu kwa watu maskini, watoto wao hawasomi katika shule wanazosimamia! Back to your senses CCM! Ulaghai mnaofanya kwa kuzunguka nchi nzima kulinda maslahi yenu na sio ya taifa hausaidii. Wananchi wanajua kinana anachofanya ni usanii wanajua kinana sio miongoni mwao na hata hajui wanavyotaabika, yeye ni watabaka jingine. Tabaka la watu walio juu ya sheria. Tubuni mtapona usanii hausaidii.