Jamii yetu imepoteza uwezo wa kufikiri kwa kina

Jamii yetu imepoteza uwezo wa kufikiri kwa kina

nandembako

JF-Expert Member
Joined
Jun 16, 2013
Posts
655
Reaction score
526
Leo nilikuwa nikijaribu kureview baadhi ya mambo kwa kina, mambo mengi tu lakini niliangalia sana mambo yanayoizunguka jamii kwa sasa.

IMANI:-

Nina imani kubwa watu wengi sana wanatafsiri tofauti ya maana halisi ya dini na imani,hadi nimeamua kuandika ni research ya muda mrefu.

Ipo hivi, watu wengi wamekuwa wakihusisha imani zao na maisha ya kawaida si jambo baya,ila kwa baadhi yao imekuwa na athari kubwa na mbaya tena kwa asilimia kubwa kwenye jamii yetu.

Inafikia wakati mtu imani yake ilivyomteka hata akiona mjusi au kitu cha kawaida kabisa kimetokea utaona anahusianisha na nguvu za giza. Mfano wiki iliyopita nilimtembelea bibi yangu kijijini. Iwas there siku kama tano hivi nilijifunza mambo mengi jamii ile inavyoyatafsiri, mojawapo ni kudhani jambo baya haliwezi kufanyika bila kuwa na ushirikina ndani yake.

Siku ya pili tangu nilipofika pale kuna takataka zilimwaga nje kwenye shamba lake, for me ningesema mtu mmoja asiye mstaarabu amemwaga takataka shambani kwangu. Ona sasa tafsiri ya wenyeji "hawa watakuwa wachawi wanafanya mambo yao". Sasa ikapelekea eneo lile likashindwa kufanyiwa kazi kwa mawazo tu hasi.

Hii inatokea kwenye jamii nyingi za kiafrika, yapo mambo mengi ya kawaida yanapelekea mambo mengi ya msingi yasifanyike kwa kuamini vitu visivyo na maana,niliwahi kuambiwa uwoga wako ndio umaskini wako now narealize kupitia hili suala la imani na jamii yetu.

DINI:-

Watu hawana tafsiri halisi ya dini. Dini haikupaswa kuchukua muda wako mwingi kuliko muda wako wa kufikiria how to survive. Ndio maana sielewi lile neno la tafuteni mtapata, bisheni mtafunguliwa na ombeni mtapewa halikulenga watu wapoteze muda mwingi makanisani na kushadadia dini kuliko kufanya maisha yao ila kwa njia halali wakifuata sheria za Mungu.

Dunia ya leo tunatukuza wachungaji kuliko kazi zetu, tunaheshimu kwenda ibadani hadi week days kuliko kufanya kazi. Halafu maisha yakiwa magumu tunasema tunarogwa, mmesahau kufanya kazi ni ibada pia. Mambo mengine tunajitakia wenyewe bwana
 
Back
Top Bottom