SYLLOGIST!
JF-Expert Member
- Dec 28, 2007
- 8,189
- 7,853
Ndugu zangu...
Sio Leo, wala Jana, au Juzi wala Majuzi tumekuwa tunasoma Lugha zenye utata katika baadhi ya nyuzi na maudhui yanayo ambatana nayo...mfano mzuri ni kama zile za mambo ya ndoa, nywele za wanawake n.k Kiujumla ni zile zinazotoa wosia kwa Jamii kwa ujumla. Wakati nyuma yake unakuta lengo ni kukejeli aina fulani ya watu au ngozi.
Vilevile, tunasoma na kuona lugha zilizo na uashiria wa Ukimbari, ubaguzi(languages with Racist Connotation) kutoka kwa baadhi ya wanahudhuri na hata viongozi wa kitaifa, mfano Robert Heriel() au Naibu Waziri wa Afya Mh. Mollel .
Lugha na misamiati wanayotumia ni ile ya unyanyasaji, kejeli na hata kudumaza.
Je, tunajibu vipi kwa hoja, lugha zilizojaa maneno au misamiati hiyo tunapokutana nayo?
Hakika, maneno yao yanaweza kuchukuliwa kama matusi.... Je, tuwatusi au kuwa tukana wale wenye kauli zilizo na uashiria wa ukimbari, ubaguzii yaani pale inapotokea hivyo? au Tunawakemea kwa Ustaha?
Hainiingii akilini kusikia Wanahudhuri au Viongozi wenye dhamana za kulinda na kudumisha Afya na Ustawi wa Jamii, wakijikita kutoa kauli kinzani na hasi dhidi yake!
Ni dhahiri wanachangia kwa namna moja au nyingine katika kuchochea na uchagizaji wa lugha hasi kwa jamii yetu, kwani kauli zao, zinapo rudiwa na kutumiwa kama silaha kwa uhasama mkubwa, kukejeli, kubeza,na kudumaza yaani kubomoa Jamii wanayodai wanataka kuijenga.... wanabomoa tu.
Nyuzi nyingi zimekuwa za Kibaguzi baguzi yaani kuna mabaguzi humu, bigoted people wanoendesha kile ninachoweza kukiita ni Ugaidi, na maudhui yaliyojaa Hisia kali na chanya dhidi ya makundi fulani ya kijamii.... maudhui na makomenti yenye madhara makubwa, yanayoweza kuathiri Afya ya Jamii kisaikilojia.....
Madhara ambayo athari zake katika Tamaduni na Maadili yetu yanaweza kuwa makubwa na kupimika!
Je, tukae kimya na kutizama Tamaduni na maadili ya Mtanzania yakigaragazwa na kubomolewa ilimradi tuna "Uhuru" -wa kuongea? 'Uhuru wa Habari'? Wapi tunaweka kikomo? Where do we draw the line?
Je, Tunaweza kujenga Jamii kwa Kubomoa?