Mulokozi GG
Member
- Jul 14, 2021
- 34
- 44
Ni muda sasa tangu Taifa letu lianze kulalamika juu ya ukosefu wa ajira kwa vijana na wanajamii nzima kwa ujumla.
Tatizo hili linaonekana kuwa changamoto inayo ongezeka kwa kasi, siyo tu ndani ya Taifa la Tanzania bali ulimwenguni kote japo katika viwango tofauti tofauti.
Ukosefu wa ajira kwa kiwango kikubwa kiasi hiki ni matokeo ya kile jamii yetu inacho kifanya, hasa hasa kile kinacho fundishwa katika mifumo yetu ya elimu.
Kwa kiasi kikubwa changamoto hii imeongeza na inaongeza hali ya utegemezi, malalamiko juu ya mifumo ya uongozi(baadhi wakionesha shaka juu ya uwezo wa Viongozi wenyewe), kasi ya maendeleo isiyo endana na rasimali zilizopo na kuna uwezekano changamoto hii ya ukosefu wa ajira isipo fanyiwa ufumbuzi wa haraka inaweza kusababisha ongezeko la migogoro na uhalifu ndani ya jamii.
Makundi mengi na watu walio wengi wanao jaribu na kujitahidi kutatua changamoto hii wanajikita zaidi katika kupambana na matokeo kama kutoa ajira au kusisitiza kuwa watu wajiajiri bila kuonesha na kutoa ujuzi watakao tumia watu kujiajiri.
Hivyo hivyo serikali na taasisi za kijamii zinajaribu kukabiliana na changamoto hii, kwa kutoa ajira kadri zinavyohitajika na inavyo wezekana. Pia kwa kuweka mafunzo ya kiuzalishajimali kama mada au shughuli za ziada katika mitaala. Ni dhahili kupitia njia hizi zinazo tumika kukabiliana na hii changamoto hazitoleta matotekeo chanya kama inavyo kusudiwa.
Hatua hizi na nyingine zinazo elekeana na hizi, ni hatua za zima moto. Kinachosahaulika ni ukweli kuwa ujasiriamali au akili ya kimaendeleo na ufumbuzi siyo kitu kinacho fanywa mara moja bali ni tabia anayo paswa kuwa nayo mtu husika.
Tafiti za saikolojia zimetusaidia tunajua kuwa tabia ni matokeo ya kufanya kitu mara kwa mara. Hivyo kukabiliana na changamoto ya ukosefu wa ajira ni lazima utatuzi uanzie katika ngazi za chini hadi ngazi za juu kabisa kwenye mifumo yetu ya elimu kufundisha na kuwajengea wanafunzi tabia zitakazo wasaidia kutumia uwezo walio nao na kujitegemea.
Hivyo somo la uzalishaji mali/ujasiriamali katika mitaala liwekwe kama somo la kujitegemea. Vile vile lianzishwe somo la elimu ya kujitambua(self determination), katika somo hili mwanafunzi afundishwe uwezo halisi alio nao binaadamu na jinsi anavyo weza kuitumia kwa manufaa na masilahi ya jamii nzima kwa ujumla, kulingana na maarifa yaliyopo katika jamii tofauti tofauti.
Ni ukweli usiofichika kuwa ukosefu wa ajira siyo tatizo hata kidogo, tatizo ni elimu na elimu siyo tatizo hata kidogo, tatizo ni aina ya elimu.
Tusiiaminishe jamii yetu kuwa kutoa ajira kutaondoa tatizo la ukosefu wa ajira. Tatizo lipo ndani ya akili, mitazamo na Imani wanazo jengewa wanafunzi na jamii kwa ujumla.
Ni dhahili walimu na wakufunzi wengi waliopo ni matokeo ya mfumo ule ule uliopungukiwa ufanisi kutokana na maendeleo na mabadiliko katika dunia ya sasa. Mafunzo yatolewe na watu walio ndani ya fani husika, wenye uwezo na uzoefu wa fani husika pia.
Mafunzo haya yaanze kutolewa katika taasisi na shule chache kama sehemu ya majaribio kabla ya kuanza kutumika ndani ya Taifa zima kuweka urahisi katika kuyatekeleza haya mafunzo kwa ufanisi mkubwa. Ili kila atakaye ingia katika mfumo wa elimu, awe anajua fika kuwa anatafuta ujuzi atakao utumia maishani mwake yeye kama yeye kwa manufaa yake na ya jamii yake. Atakayeajiriwa iwe ni matokeo na siyo lengo kuu la mfumo wa elimu kwa jamii nzima

Upvote
1