SoC02 Jamii yetu

SoC02 Jamii yetu

Stories of Change - 2022 Competition

Willntoke

New Member
Joined
Sep 7, 2022
Posts
3
Reaction score
1
Wahusika,
■Njiwa.
■Kondakta.
■Dereva.
■Mama kuku.
■Miss Tausi.
■Mwewe.
■Kunguru.
■Bwana afya.
■Shangazi bata.

Ilikuwa siku ya alhamisi asubuhi katika jiji la Miamba(Mwanza) dala dala moja yenye usajil wa TLK 791 ikitoka Ilemela kuelekea kisesa dala dala ikitawaliwa na sauti ya redio iliyokuwa inarusha taarifa ya habari.

Dereva: anavunja ukimya kwa kusema daaah! kiukweli bei ya mafuta inazidi kukwea pipa sijui tutaishi vipi. kutwa nzima tunatafuta pesa ambayo asilimia kubwa inaishia kujaza mafuta kwenye gari.

Kondakta: Mmmh! sio poa ndugu bora wewe unaendesha kuliko mimi hapa kutwa nzima shingo imening'inia jua lote linaishia usoni naambulia kuwa mweusi kama mkaa halafu mfukoni fedha kiduchu.

Njiwa: Wanachi wenzangu mnafikiri viongozi wanafaidi sana huko ila kiukweli uongozi ni wito.

Pia wanajitolea sana kuhakikixha wananchi wao tunaishi maisha bora pekee yao hawawezi bila ushirikiano wetu kwa sababu sisi ndio mabosi zao.

Ila kwa upande wangu riziki naiona nisiwe muongo ndugu zangu mkono unaenda kinywani bila shida kabisa.

●Kunguru :sisi wengine kutwa juani kuzunguka huku na kule kutafuta chochote kitu lakini twambulia jasho lisilo na matumaini tukiwa na imani kesho itakuwa bora ya Leo na hatuna budi ya kusubiri asubuhi labda tuta fanikiwa halafu unadhifu wetu unaficha mengi sana laiti mngejua shida na sisi ni marafiki wasiotengana mngetuonea imani.

●Mwewe :Bora nyie ndugu zangu kwa upande wa vijana wetu mambo sio rahsi hivyo ina wa radhimu kufanya unyang'anyi ndio wapate chochote kitu sio kwamba wanapenda kuwa wakatili ila hawana cha kufanya zaidi ya hicho laiti kama kungekuwa na jitihada za kuwaelimisha na kuwapa mitaji ya kufanya biashara wangekuwa wadilifu katika nchi yao na kuwa walinzi wa mali za wananchi.

●Mama kuku:Bora nyie wanaume kwa upande wetu wa mama changamoto ni nyingi sana kama vile tatizo la maji, umbali mrefu kwenda kujifungua na kunyanyaswa kijinsia kama ningepata nafasi ya kutoa ushauri kwa viongozi wetu ningependa watazame haya matatizo kwa ukaribu zaidi pia elimu ya jinsia itolewe kwa mabinti zetu ili kuandaa kizazi kilicho bora hapo baadae .

●Miss Tausi:Hali sio shwali kwa sisi mabinti kabisa naomba kunukuu maneno ya mama ndege"elimu ya jinsia itolewe kwa mabinti zetu" nikweli kwa sababu rushwa ya ngono imekuwa kikwazo kikubwa katika kutimiza ndoto zetu kama wasichana.

●Bwana afya : kwanza kondakta asante ndugu yangu kwa rifti kwa sababu maisha yangu tu ni kichekesho kutwa kushinda majaralani kuokota chupa za plastiki sina mbele wala nyuma na nguvu nilizo nazo zote hazija nisaidia chochote katika jamii yangu je? nifanye nini kuondokana na hili tatizo sugu ndugu zangu.

●Shangazi bata: ujue nimewasikiliza mda mrefu sana na huu mjadala hauwezi kuisha Leo wala kexho naomba niumalize kwa kumuunga mkono mama kuku kwenye suala la elimu ambayo ndiyo siraha mojawapo ya kuteketeza umasikini na utegemezi na elimu sio lazima mpka itolewe shuleni tu bali hata wazazi tuna nafasi katika kuwapa elimu vijana wetu waweze kujiamini wao binafsi na kuwa na uwezo wa kujitambua, lakini nasisi watu wazima tufanye kazi kwa bidii ili kuwawezexha hawa vijana huku tukiamini katika mungu ambae ndiyo chanzo cha kila kitu na amini huyu. ADUI (umasikini ) hatapata nafasi tena katika maisha yetu.

Kwa pamoja walimsifu sana shangazi Bata kwa mazungumzo yaliyojaa matumaini na nguvu ya kupambana haijalishi changmoto ni nyingi kiasi gani.

●WAHUSIKA WALIVYOTUMIKA.
1.Njiwa=mtu tajiri.

2.Kunguru=mvuja jasho mwenye tumaini la kupata.

3.Mwewe=Mtetezi wa vijana.

4.Miss Tausi=Binti msomi mwenye ndoto kubwa.

5.Bwana afya=mlala hoi.

6.Shangazi bata=Mama anae amini katika mungu.

7.Mama kuku=Mama anaeishi maisha duni.

8.Dereva & Kondakta =waathirika wa mfumuko wa bei ya mafuta.
MWISHO
 
Upvote 2
Habari yako ndugu Willntoke.

Hongera kwa nakala nzuri yenye mawaidha na tija kwa jamii.

Kura yangu umepata!!

Nikiamini katika uchakataji wako wa mambo na uwezo wako wa fikra na ubunifu, naomba ukipendezwa, nipate mawazo yako au mapendekezo juu ya nakala ihusuyo


Ahsante!!
Kiukweli hongera kwa nakala muhimu kwa sababu bila afya bora Hakuna maendeleo uzima kwanza halafu upambanaji ndiyo unafatia Big up👊
 
Back
Top Bottom