Jamii za Tanzania zinawakilisha makundi yote makuu manne ya lugha barani Afrika

Jamii za Tanzania zinawakilisha makundi yote makuu manne ya lugha barani Afrika

Kasomi

JF-Expert Member
Joined
Sep 3, 2014
Posts
11,030
Reaction score
20,391
Nchini Tanzania Kuna makabila Zaidi ya 120 (125 hivi)

Lakini kuna Makabila yenye watu zaidi ya milioni moja makabila hayo ni Wasukuma, Wanyamwezi, Wachaga, Waha, Wagogo, Wahaya, Wajaluo na Wamakonde.

Jambo la pekee kuhusu jamii zilizoishi na zinazoendelea kuishi Tanzania ni kwamba wakazi asili wanawakilisha makundi yote makuu manne ya lugha barani Afrika.

1. Idadi kubwa sana ya Watanzania ni wa jamii ya Wabantu (k.m. Wasukuma, Wazaramo, Wapare na Wapogoro).

2. Nje ya hao, kuna Waniloti, kwa mfano Wamasai na Wajaluo ambao wengi wao zaidi wanaishi Kenya.

3. Kundi lingine ni makabila ya Wakushi wanaoishi kaskazini mwa Tanzania; hao ni makabila ya Wairaqw, Wafiome, Wasi na Waburunge.

4. Kuna kundi la Wakhoisan wanaofanana na makabila ya Botswana na Namibia; wanaitwa Wasandawe .

Hatimaye kuna Wahadzabe wachache ambao utafiti wa DNA umeonyesha hivi karibuni wana uhusiano wa asili na Watwa wa nchi za Afrika ya Kati.

Pia kuna asilimia ndogo ya watu wenye asili ya nje ya bara la Afrika, kwa mfano Wahindi, Waarabu, Waindochina, Wafarsi, Wachina, Wagiriki na Waingereza. Hii ilisababishwa na karne za mchanganyiko wa mahitaji ya biashara yaliyofanywa na mabara ya Ulaya na Asia hapo Afrika.
 
una agenda ya siri mkuu
umeshindwa kutaja wakurya hata kidogo
Kuna Zaid ya makabila 120 (125 hivi) kama kwenye mada ilivyo elezwa.

Hivyo nikisema niwataje wakurya na wajita watasema niwataje hivyo hivyo na wazinza.

Kwa kusema hivyo itoshe kuwataja walio wakilisha hapo.
 
Ungeorodhesha makabila yote na kuyaingiza kwenye hayo makundi yako manne
 
Uzi pumba huu...ina maana .....Waha ni wengi kuliko ....wahehe ... wanyakyusa
 
Ungeorodhesha makabila yote na kuyaingiza kwenye hayo makundi yako manne
Kuanza kuya tenganisha yote shughuli ipo hapo nimefanya sampling.

Ila orodha ya makabila ipo ipo hapa
 
Back
Top Bottom