Jamii za Wafugaji wa Kisukuma, Mang'ati na Wengineo zimulikwe, wanaturudisha nyuma katika vita ya Unyanyasaji Wanawake,Watoto wanakosa haki za Msingi.

Jamii za Wafugaji wa Kisukuma, Mang'ati na Wengineo zimulikwe, wanaturudisha nyuma katika vita ya Unyanyasaji Wanawake,Watoto wanakosa haki za Msingi.

Bush Dokta

JF-Expert Member
Joined
Apr 11, 2023
Posts
24,831
Reaction score
45,154
Ni zile jamii za Wafugaji wa kuhama hama. Hawana makazi maalumu.

Leo wako mbeya kwesho wako Tanga.

Natoa wito kwa serikali, japo kila mtu ana haki ya kulinda, kutumza na kuishi kwa mujibu wa mila, desturi na utamaduni wake bado hatuwezi kuvumilia ikiwa mila hizo zinavunja heshima, utu, haki za watu wengine.

Katika baadhi jamii za wafugaji wa kuhama hama yaani Pastralists, hali ni mbaya sana.

Kutokana wao wameshazoea maisha hayo baadhi wanaona ni haki yak kuishi ktk giza na gereza la mateso yanayotokana na mila hizo mbovu zisizofaa.

Baadhi ya madhila yanayozikabiri jamii hizi ni kama vile

1. Watoto wadogo wa kike kati ya umri 10 hadi 14 kuozeshwa kwa wanaume wakubwa au wazee., Mimba za utotoni ni nyingi
2. Watoto kukosa fursa ya masomo
3. Vipigo na adhabu kali zinazotolewa dhidi ya wanawake na watoto kutoka kwa Viongozi wa familia hasa Wababa.
4. Hali duni ya maisha ya kukosa nyumba bora kwa ajili ya watoto na Familia kwa ujumla.

5. Watoto na wanawake kukosa fursa ya kupata huduma bora za kijamii kama bile Matibabu, USafiri, maji, umeme n.k
6. Vitendo vya kuharibu au kudhuri sehemu mbali mbali za mwili kwa wanawake hasa Ukeketaji, Kutoboa masikio tundu Pana, kuchora chora alama usoni na mahala pengine.

7. Mjane kurithiwa na Ndugu wa Mume, hii ni lazima hata kama hupendi.

8. Wanaume kuoa wanasake wengi bila kuwa na uwezo wa kuwahudumia na matatizo ya hapo jui hujitokeza zaidi
9. Wanawake kufanyishwa kazi za nguvu bila kupumzishwa.

Kutokana na uelewa mdogo wa maisha ktk nyanja mbali mbali Giza hili la unyanyasaji limeshakuwa sehemu ya maisha yao na wao huona kama hakuna tatizo.

hali hii inarudisha nyuma Jithada za serikali kuhakikisha kila mtanzania anaishi maisha bora, yenye kuheshimu utu, amani na maendeleo.

Salut! Bonne Soir. À Bientoť
 
Anza kwanza na watoto wa mjini kama magomen na mwembe yanga nao shule hawaend vile vile

Dar nzima imejaa watoto wala gundi nao ni wasukuma? Tena hawana hata pakulala wanalala mitaroni na kwenye madaraja
 
Hapo migo migo kuna mishoga kibao iliotokana na watoto ambao wazazi hawataki kutekeleza wajibu wao…!!
 
Hapo migo migo kuna mishoga kibao iliotokana na watoto ambao wazazi hawataki kutekeleza wajibu wao…!!
Vitoto vya miaka 16 vinaolewa na wazee wa miaka 70 huku uswahilini tena Ramadan hii ndo usiseme na ramadhan ikiisha wanaanza kuachana tena

Waache ujinga bhana
 
Mimi ni mtafiti nimeishi na jamii za wafugaji ,kuna kesi tuliishuhudia ya Baba kuua mtoto Kwa kumkomesha mkewe kisa kundi la ng'ombe limekula mazao ya Jirani.

Mke aliulizwa kwanini amewaacha ng'ombe hadi kuharibu mazao ya watu.

Akajibu,alikuwa ananyonyesha mtoto,ndipo mtoto aliposhikwa na jibaba lenye nguvu la kisukuma na kubamizwa kwenye mti,na kupelekea umauti wa mtoto wa miezi nane.
Akanyimwa haki yake ya kuishi.

Mama mtu alilia hakuwa na pakusemea lakini inteligensia Kali ilibaini lile na wahusika kusema ukweli.

Swali,

Ni watu wangapi wanafanyiwa ukatili wa kutisha na hawana pa kusemea?

Yapo mengi nitakuja na simulizi kabisa kuhusu ubaguzi wakikabila na kikanda,unyanyasaji,Mila potofu ,ubabe wa kishamba,dhuluma na mauaji ya nje nje .Ama kweli Dunia haina usawa.
 
Anza kwanza na watoto wa mjini kama magomen na mwembe yanga nao shule hawaend vile vile

Dar nzima imejaa watoto wala gundi nao ni wasukuma? Tena hawana hata pakulala wanalala mitaroni na kwenye madaraja
Tujikite kwenye kujadili Solution. Acha masimango
 
Mimi ni mtafiti nimeishi na jamii za wafugaji ,kuna kesi tuliishuhudia ya Baba kuua mtoto Kwa kumkomesha mkewe kisa kundi la ng'ombe limekula mazao ya Jirani.

Mke aliulizwa kwanini amewaacha ng'ombe hadi kuharibu mazao ya watu.

Akajibu,alikuwa ananyonyesha mtoto,ndipo mtoto aliposhikwa na jibaba lenye nguvu la kisukuma na kubamizwa kwenye mti,na kupelekea umauti wa mtoto wa miezi nane.
Akanyimwa haki yake ya kuishi.

Mama mtu alilia hakuwa na pakusemea lakini inteligensia Kali ilibaini lile na wahusika kusema ukweli.

Swali,

Ni watu wangapi wanafanyiwa ukatili wa kutisha na hawana pa kusemea?

Yapo mengi nitakuja na simulizi kabisa kuhusu ubaguzi wakikabila na kikanda,unyanyasaji,Mila potofu ,ubabe wa kishamba,dhuluma na mauaji ya nje nje .Ama kweli Dunia haina usawa.
Hali ni mbaya mno huko vijijini na maporini wanakoishi. Na hawana pakukimbilia wala wakuwatetea
 
Mkuu we acha tu hali si nzuri haswa Kwa vibarua wanaofanya kazi za kuchunga Kwa hawa jamaa
Navibarua pia wanapata cha moto? Angalau huyo akiona vipi anasepa lakini kwa Mwanafamilia sio rahisi.
 
Vitoto vya miaka 16 vinaolewa na wazee wa miaka 70 huku uswahilini tena Ramadan hii ndo usiseme na ramadhan ikiisha wanaanza kuachana tena

Waache ujinga bhana
Si kweli labda urudi kusoma ...Ukibisha nakuletea takwimu hapa ...Watu wa pwani tuna miili midogo sio ndoa z utotoni.
 
Kwa nini tusimulike mafisadi wanaokifilisi Taifa na kuliacha na madeni mazito tuhangaike na jamii ya wafugaji wanaopambania Mila zao zisizo na madhara yoyote?
 
Katika makabira ambayo wanasifa wahaya wanasubiri ni wasukuma wa sasa pro max.
Kwanza wanaona sifa kupenda ngono na kuwa na wake wengi ambao mwisho wa siku matunzo yana washinda.
 
Kwanza wanaona sifa kupenda ngono na kuwa na wake wengi ambao mwisho wa siku matunzo yana washinda.
Matunzo ni hafifu sana. Atleast wale wanaoishi Mijini. Hawa wa kufunga kilimo cha kuhama hama hali mi mbaya mno.
Its a tragedy
 
Kwa nini tusimulike mafisadi wanaokifilisi Taifa na kuliacha na madeni mazito tuhangaike na jamii ya wafugaji wanaopambania Mila zao zisizo na madhara yoyote?
Hao Mafisadi kaka Hatuwawezi, Mungu mwenyewe amewawezesha kuwa na nguvu na akili za kuiba. Harafu ukitaka kuona mafisadi wanabarikiwa tazama wanaishi muda mrefu sana hawafi chini ya miaka 70. Ikitokea ni bahati mbaya sana.

Wanabarikiwa mno. Ifike mahala wizi, ufisadi, uporaji, ushoga tuviweke kwenye kundi la Baraka. Tuache kupingana na ukweli
 
Back
Top Bottom