Hamza Nsiha
JF-Expert Member
- Jul 25, 2022
- 221
- 197
Leo nimeamua kutoa ya moyoni kuhusu, Manufaa niliyoyapata JamiiForums.
Kiukweli, nilibahatika kujiunga na JamiiForums mwezi wa saba~ mwaka huu mara baada ya kutumiwa tangazo linalohuso shindano la "STORIES OF CHANGE 2022" kutoka kwa rafiki yangu ambaye anadai aliliona kutoka kwenye mtandao wa Instagram.
Kabla ya hapo, nilikuwa nikisikia kuhusu "JamiiForums" lakini sikubahatika kuifuatilia kiundani hususani nilisikia baadhi ya marafiki zangu wakichangia mada mbalimbali za kisiasa huku wakianisha vyanzo mbalimbali vya habari ikiwemo JamiiForums.
Lakini, cha ajabu tangu nilipojiunga kama mwanachama wa JamiiForums, dhahiri nimegundua kuwa nilifanya makosa makubwa sana kutojiunga toka zamani_ kwa maana hivi sasa JamiiForums ndio mtandao wangu pendwa. Kila siku lazima niperuzi kuangalia mada mbalimbali zilizowekwa kikaangoni, pamoja na kusoma stori mbalimbali ni ukweli dhahiri kuwa JamiiForums imenikomboa katika mambo mbalimbali ambayo yamenifanya kuwa mchangia mada mkubwa katika stori na midahalo mbalimbali nje na JamiiForums.
Pia kitu kikubwa, ni kuwa nimeweza kuwashawishi baadhi ya rafiki zangu ambao walikuwa na fikra kama zangu za awali kuhusu JamiiForums. Lakini mpaka sasa wamefanikiwa kujiunga huku wakifurahishwa na Shindano la "STORIES OF CHANGE"
Pia ningependa kufahamu mwana JamiiForums mwenzangu, ilikuwaje mpaka ukaingia katika mtandao huu mzuri na wenye tija au na wewe uliingia kupitia rafiki yako?
Mwisho wa yote, japo si kwa ubaya _Ningependa kuwashukuru wana Jukwaa wenzangu ambao tumekuwa tukishea mawazo mbalimbali katika mada tofauti nilizowahi kuzipakia.
Pia mimi ni mshiriki wa "STORY OF CHANGES" nikiwa na mada inayohusu "VITA YA VIJANA DHIDI YA MAENDELEO YA SAYANSI NA TEKNOLOJIA"
hivyo si vibaya kama utapata muda wa kupitia ili kujifunza baadhi ya mawazo niliyoweza kuainisha pia ukipendezwa zaidi unaweza kunipatia kura yako.