JamiiTalks
JF Advocacy Team
- Aug 7, 2018
- 685
- 1,124
Taasisi za JamiiForums (JF) na Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC) zimeingia Makubaliano ya Ushirikiano (MoU) katika masuala anuai ikiwemo kuhakikisha uwepo wa Sera bora nchini; kuimarisha Haki za Kidijitali, Uwajibikaji, Utawala Bora, kuchochea Haki ya Utoaji na Upatikanaji wa Taarifa Sahihi kwa wakati na utetezi wa Haki za Binadamu
Ushirikiano huu unatarajiwa kuongeza ushiriki wa Wananchi katika Maendeleo ya Kisiasa, Kijamii, na Kiuchumi, Kidigitali kwa maarifa zaidi, huku ukikuza Majukwaa jumuishi na salama kwa Mijadala yenye tija kwa Umma na Taifa.
Makubaliano hayo yametiwa saini na Mkurugenzi Mtendaji wa JF, Ndg. Maxence Melo na Mkurugenzi Mtendaji wa LHRC, Dkt. Anna Henga.