JamiiForums ni kiboko, imenipa kazi mwenzenu

Mkuu kweli wewe ni mzee wa budget,...ila siku ukioa kumbuka kubadilika maake_mmmmmmh

Hahahahaa....wala sioni cha kubadilisha hapo, mbona cjibani?! Hebu angalia hapo kwenu kama kila wiki mnakula maini (joke)!!!! nikuambie mkuu, na-enjoy sana na hii lyf style. Nakumbuka ki2 kilichokuwa kinaniumiza sana sana ni vocha....unajua haya mambo ya simu nayo ni upuuzi mtupu, na mbaya zaidi nilikuwa nashindwa kujizuia....c unajua sie wengine toka familia maskini kila cku wa2 ni kutu-beep na wewe ndio upige. Nikajikuta kwa mwezi natumia hela nyingi sana. Mwanzo wa mwezi matumizi ya simu ndo yalikuwa makubwa sana coz' bado unakuwa na visenti...nikatafutia dawa. Nikajiunga na post paid ya tgo ya Sh. 20,000/=!! Unajua nini? hii ki2 imekuwa very helpful kwangu kuliko ambavyo nilitarajia. Airtime ninayowekewa (ya 20,000/-)huwa inaishia siku za mwisho mwisho wa mwezi ambapo huwa sina tena hela ya kuchezea hovyohovyo!!!
 

Hapo kwenye red, vipi kama hakuna umeme? Ila nimeipenda ile ya kula asubuhi kabla ya kwenda kazini. Nimeifanya sana hiyo. It saves you a lot of money na muda pia. Muda nikiwa na maana kuwa wakati wafanyakazi wengine wanaenda lunch, unaweza kuutumia huo muda kufanya mambo ya maana sana.

For me, nilikuwa nakula asubuhi kabla ya kwenda kazini, then muda wa lunch niliutumia kutafuta scholarships kwenye net na kwenda posta kutuma barua za maombi ambapo nilifanikiwa kupata scholarship ya kwenda kusoma nje ya nchi. Wengine walishangaa nimepataje hiyo scholarship mapema hivyo, wakahisi nilikuwa namjua mkubwa fulani hapo ofisini. But scholarship ilitoka huko huko majuu and no mkubwa was involved.

My strategy ilikuwa sio kuongeza kipato immediately bali kuongeza shule yangu ambayo ingenisaidia kuongeza kipato in future. Mtu mwingine anaweza kuwa na plan tofauti. Kama prospective entrepreneur anaweza kuutumia huo muda ku-design business plans, making contacts, etc. Au unaweza kuutumia huo muda kutafuta kazi ambayo inalipa zaidi. Ni muda mfupi, but you can do a lot kama ukijipanga vizuri. Ukirudi home jioni unajikuta uko free b'se mambo mengi ulishaya settle wakati wa lunch kazini.

Mleta hoja ameuliza kama 400,000 zinakidhi kwa maisha ya Dar. Lakini amesahau kuwa maisha yanatofautiana from one person to another. Sh. 400,000 inaweza kuwa nyingi sana kwa mtu mmoja na isitoshe kabisa kwa mtu mwingine. Maisha ya Dar are not the same kwa kila mtu. Kwa mfano, kuna watu watatu wanaishi maeneo ya Ufundi Kurasini na wanafanya kazi maeneo ya stesheni. Mmoja atapanda daladala kwenda na kurudi kazini, mwingine ataenda na kurudi kazini kwa miguu na mwingine atapanda daladala kwenda kazini lakini ataarudi kwa miguu.

So, maisha ya Dar ni jinsi unavyoyapangilia. Ukikubali tuu Dar ikupangie maisha lazima itakula kwako hasa kama kipato chako ni kidogo au cha wastani. Mkuu nafikiri wengi watafaidika na somo ulilotoa kwenye posts zako hapo juu. Kudos.
 

LABDA mbagala usiiwaingize mkenge wenzio wakaja kuvuliwa chupi sema unaishi wapi unalipa ngapi kama yuko anaitaji chumba mbagala ani pm sh 15 kwa mwezi analipa miezi sita tu maji 3000 umeemee 3000 si kalvari ya dunia njoo sinza uone kama ujaungana na wenzio pale afrikasana so kuonyesha sehemu inasaidia zaidi mpwa
 

mkuu ni pm nikupe vocha kila mwezi free usiogope mpwa nitumie namba yako
 
mkuu ni pm nikupe vocha kila mwezi free usiogope mpwa nitumie namba yako
Sijawahi kupata KITU KIKUBWA kama nilichokipata katka thread hii!! Jamani 400,000 ni kubwa sanaaaaaaaa!!!!!! Wengine huku tunalipwa 500,000 na bado lisaa limoja la lunch nakimbia shule ya JIRANI hapa napiga pindi kwa 250,000 kwa mwezi! kaza mkaka,life sio cheap hivyo!
 

Du..ukitembelewa na mshkaji wakati wa ushatandika meza lazima utanuna... tight budget.......girl friend akija wiki endi aje na pakti ya tambi...
 
Thats a start point. Wenzako tunatafuta kazi nzuri wakati tupo kazini na sio kutafuta wakati huna kazi. Kumbuka pia work history ni muhimu sana...

Kula mzigo broda, acha za kuleta

 

Kwenye color hapo man, nilizani ulitaka kusema ni ngumu sana hiyo ki2!!! Ningeamrisha Green Guards waje kukuvua gwanda sasa hivi na kukupeleka pale Ofisi ndogo mtaa wa Lumumba ili ukapatiwe T-shirt na Cap za kijani na njano! lol
 
Reactions: EMT
Du..ukitembelewa na mshkaji wakati wa ushatandika meza lazima utanuna... tight budget.......girl friend akija wiki endi aje na pakti ya tambi...

Mgeni kwangu ruksa, asije na chochote mkononi, lakini vilevile ahakikishe anakuja kuanzia saa tisa na aondoke kabla ya saa moja!!!!
 
Chukua kazi hiyo
Mi nlianza na mshahara ambao net ilikuwa 170,000 nkatafuta chumba kwa mwezi nlikuwa nalipa 10,000.
Kazi moja huanzisha nyingine.
 
Kwenye color hapo man, nilizani ulitaka kusema ni ngumu sana hiyo ki2!!! Ningeamrisha Green Guards waje kukuvua gwanda sasa hivi na kukupeleka pale Ofisi ndogo mtaa wa Lumumba ili ukapatiwe T-shirt na Cap za kijani na njano! lol

Haha haa haaa. Mkuu vipi idea ya ku-pack lunch toka home na kwenda nayo kazini? Nimenote kwa wezetu wa nchi zilizoendelea wakienda kazini huwa wana-pack lunch zao toka nyumbani. Ofisi nyingi wametenga chumba kama dinning room, kuna fridge hapo, microwave na jagi la kuchemshia maji. Hivyo, ikifika walati wa lunch watu wanachukua lunch zao walizotokanazo home, wanapasha moto kidogo na kula hapo hapo ofisini wakati wakisoma kilichodhiri kwenye magazeti (sie tunasoma magazeti wakati wa kazi). Ni wachache sana wanaongozana kwenda hotelini kula. Watakaotoka nje sana sana wataenda kununua snacks and that is once in a while.

Lakini kwetu unakuta fridge or jagi la kuchemshia maji vyote viko kwa sekretari wa boss mkuu na ni kwa ajili ya boss na wageni wake special tuu. Kwetu hatutaki shida. Pia tunaona noma ku-pack lunch na kuja nayo kazini. Kwa vile boss huwa anatoka kwenda kula lunch, basi na secretari nae atataka kufanya hivyo. Hii ni moja ya sababu ya sababu ya kuenea kwa rushwa ndogo ndogo maofisini. Unaingia ofisi ya umma, ghafla unadaiwa pesa ya lunch. Wengine muda wa lunch wanautumia kukutana na nyumba ndogo au vigaloni. Unaonaje pia tutengeneze tabia ya kubeba viporo vyetu kazini for a lunch? Si tunaweza pia ku-save a lot of money? Halafu jinsi kiporo kilivyo kitamu.
 

tena kikiwa kiporo cha wali maharage,utakipenda mbona!
 

Dah! Umenikumbusha mkuu....hii ki2 nililuwa naifikiria sana 2!! Nilishawahi kuifanya wakati fulani wakati wa mfungo wa ramadhani!!! Wakati huo, nilikuwa naenda job saa 12 jioni. What i was doing, nilikuwa natoka gheto na lunch box yangu kwa ajili ya daku!! Ona wale waliokuwa wanaona noma kutembea na lunch box, walikuwa wanahangaika ile mbaya na matokeo yake mara nyingi ikawa inaishia kwenye ku-share the same msosi!! Afadhali umenikumbusha, wacha nikanunue empty lunch box za kutosha kwa ajili ya kutimba nazo kwa job!!

Halafu umeongea hilo la virushwa vidogo vidogo...mkuu, yaani ni aibu!! Nakumbuka wakati fulani nikiwa kwenye benki moja hapa town nalikuwa nasikitika sana kuona wamama watu wazima wanavyowanyenyekea baadhi ya wateja...hii sio kwamba ilikuwa ni customer care, la hasha...hiyo ilikuwa ni kwa ajili ya wateja waliokuwa na tabia ya kutoa kitu kidogo wanapohudumiwa (in short, huwa siwapendi wateja wa aina hii)!! Unakuta mama mtu mzima mwenye watoto na wajukuu, anaacha alichokuwa anafanya (wakati mwingine anamuacha mteja mchovu) na kumkimbilia mteja ambae anajua anapomuhudumia anamuachia sh.10,000/-!!! Nilikuwa najisikia aibu sana...Hili naliongea kwa uchungu !!! kuiendekeza njaa, ni ki2 mbaya sana....!!
 
Reactions: EMT
Chukulia kama ni sehemu ya kupatia uzoefu maana siyo rahisi kupata kazi nzuri bila ya kuwa na uzoefu.
 
Kwa kweli mmemshauri vizuri. Yaani nimesoma post moja moja. Zoote ni nzuri, na wamekupa namna ya kuishi/kufanya.
Wamekupa mpaka ushauri ambao utakusaidia kwa miaka 5 au 6 ijayo.
Mwenye macho, na aone.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…