JamiiForums ni kiboko, imenipa kazi mwenzenu


Sure watu tumeanza na sh 75,000/= graduate baada ya miaka 15 tunakula mamilioni.Kwanza tafuta uzoefu wa kuja kukupa kazi nzuri zaidi..Usijali ukiwa na kazi unapata kazi//////
 
Chezea mshahara usichezee kazi,ni ushauri tu!
 
ebwana weee jembe... Ngoja nifanyie kazi, ntaifanya my blue print kwenye matumizi yangu ya mwezi... Santaa..

Ccta hapo umetisha kinoma i neva thought dis, tanx nadhani kijana kakusoma
 
Wakuu mengi mmeyasema tena ya kufaa si kwa kijana wetu tu anayeanza maisha bali hata kwetu sisi ambao tumekwisha kuwa wakongwe katika maisha,mnaonaje kwa idhini ya mtoa mada tukaifunga mada hii ili kutoa nafasi ya kijana wetu ku incorporate huu ushauri uliuotolewa ili dogo achukue kandarsi yake na kuanza kupambana? together ninawakilisha.
 
Babake hongera sana kwa kupata kazi. Hata hiyo sio mbaya kuanzia maana mbuyu nao ulikuwa kama mchicha siku moja.
 


Du, nzuri sana ingawa hamna kidude cha kukupa "I like". Nilijiuliza maharage unapikaje bila mkaa nikakuta umeweka mafuta ya taa lita 6. Mnyumbulisho poa sana kwa bachela anayeanza maisha
 
Hongera kwa kupata kazi, nadhani wazoefu wa jiji wameshakupa hints, so nenda kafanye kazi
 
Du, nzuri sana ingawa hamna kidude cha kukupa "I like". Nilijiuliza maharage unapikaje bila mkaa nikakuta umeweka mafuta ya taa lita 6. Mnyumbulisho poa sana kwa bachela anayeanza maisha

I ril congratlat u! Nmekukbal sana! And nmejfunza alot and i'm goin 2work on it practically, 4that cas thr z no maisha magumu coz hata yule wa 150,000 anaweza kuish vzr! Gud.
 
Tatizo kubwa ninaloona kwa vijana ni kutengeneza daraja kabla hujaona mto,nina maana kuwa kama kweli unatafuta kazi ,kila kazi ina vigezo vyake na pia kuna mambo ya ujuzi hebu jiulize kwa hiyo 380,000 si umekuta kuna watu wako hapo wanafanya kazi,cha muhimu angalia malengo yako,mshahara ni nyongeza ya malengo yako,.
kwa mfano unaweza ukaa unapata mshahara mdogo lakini hapo hapo unajifunza mengi ambayo ulikuwa huyajui,tuchukulie umepata kazi ya masoko au benki huko utakutana na vitu vingi ambavyo hata waalimu wako hawajawahi kukufundisha au kama umefundishwa ilikuwa ni nadharia zaidi,muhimu kama hapo unapata ujuzi na si mshahara,kumbuka ukifanya kazi kwa muda unapata ujuzi sasa hapo ndipo utaanza kutafuta kazi nzuri kwa kutegemeana na kisomo na ujuzi ulionao na pia uzoefu.katika soko la ajira kuna mambo mengi wandugu ,mambo ya mshahara ni sehemu tu ya yote.Mimi naona ni muhimu zaidi kupata ujuzi kuliko kukimbilia mishahara minono,hiyo mishahara minono ina vigezo vingi kuipata.Hapa mjini watu wanapata laki 2 na wanaishi ,hata Roma haikujengwa kwa siku moja
 

heshma kwako mkuu wangu! Nimeipenda..
 
mkubwa nenda kapige kazi hiyo hata usiache coz hata wewe mwenyewe ulikuwa na expirience ya kutosha juu ya kutumia boom ambalo ulikuwa ukipewa 300000Tsh@mwezi na ukaweza kumaliza chuo vizuri Sasa itashindikana vipi kwa laki 4 ambayo unaipata kila mwezi bro?
 
Kijana chagua kazi yeyote katika hizo lkn consider sana kazi itakayokupa career development na sio salary ili uje weza kupata jo ya ukweli badae, kwa hizo salary uliosema zote ni kama sawa tu, mimi mwenzio nilipomaliza chuo nilikaa mkoa mwaka mzima bila job na nikapata kazi ya 350,000 dsm,nilikuja nikaanza kazi bila ya kujiuliza lkn nilijua kuwa kazi ndio huleta kazi, na kweli baada ya miezi isiyozidi sita tu nikapata job nyingine niliyokuwa nayo hadi sasa ambapo nakunja mkwanja wa ukweli.
Pia utakua mwendawazimu kama utaacha hiyo kazi then uendelee kukaa kwa ndugu.
 

Heshima kwako mkuu, Hii sred imekuwa ya miaka 50 ya uhuru kwa ubora, nadhani hata wale wanaosema posho ziongezwe wanaweza kujifunza kitu kutoka kwako, Hata hivyo nimegundua wewe siyo mvivu, kinachosumbua watu wengi ni uvivu. Huo uchambuzi wako hasa kupika asbh inahitaji moyo.

Hata hivyo hapo kwenye RED na Bluu kama kuna utata fulani, je ukinywa maji ya moto yenye soya si altenative ya chai? kwa hiyo chai unakunya ila hujasema unainywa kwa utaratibu gani.

Labda niongezee na kwa faida ya wana JF, Kunywa chai ya rangi siyo vema kabisa, majani ya chai yana cafein ambapo ukiizoea chai ya rangi hiyo cafein inakuongezea kuhisi njaa mara kwa mara hivyo kuwa mtu wa menu na kuongeza matumizi. Kwa hiyo bwana NasDaz anaweza kuhimili mlo wa asubuhi tu kwa kuwa hatumii majani ya chai, hivyo hawezi kuhisi njaa mapema. Ukitaka kufuata huu utaratibu wake lazima uachane na mwaswala ya chai ya rangi.

Kitu kingine, kwa faida ya dogo aliyepata kazi, Tumbo halina kioo, unaweza kula menu ya bei ndogo siku za mwanzoni huku ukitunisha kipato na kununua vitu vya msingi kwa ajili ya matumizi ya baadaye. Huo mshahara ni mkubwa unatosha kabisa kuanzia maisha, siye enzi hizo tulianza na 45,000/= lakini leo hii si haba.

Kaka NasDaz nimekukubali na nimedesa sredi yako kwa ajili ya dogo.
 
Nadhan sasa kijana ametuelewa na bila shaka ameshaanza kupiga mzigo,NASISITIZA TENA "chezea mshahara usichezee kazi"
 
We NasDazNundaz we si Unaishi Mafia... au Ushaachana na Uvuvi Umeamua kwenda Dar kuajiriwa Dah Totoz hupati kwa Mtaji Huu Umeamua hataMsosi Wajipikia Tena Alfajiri kama Wapika Maandazi....
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…