Julai 26, 2024, JamiiForums ikishirikiana na The Collaboration on International ICT Policy for East and Southern Africa
(CIPESA) iliendesha Mafunzo ya Uhakiki wa Taarifa kwa Wadau wa Tasnia ya Habari kama sehemu ya kuwajengea uwezo katika kutekeleza majukumu yao.
Washiriki walifundishwa athari ya taarifa potofu hususan kwenye kipindi cha Uchaguzi, jinsi ya kutambua taarifa hizo na namna wanavyoweza kutumia ujuzi na nyenzo mbalimbali kuzihakiki.
Aidha, Washiriki hao walipata fursa ya kufafanuliwa jinsi JamiiForums inavyopambana na taarifa potofu kupitia Jukwaa lake mahususi la
JamiiCheck.com ambalo huwashirikisha Wananchi mchakato wa kuhakiki maudhui yanayopatikana ndani na nje ya Mtandao.