Janet Jackson Asilimu, Kufunga Ndoa na Bilionea wa Qatar

Janet Jackson Asilimu, Kufunga Ndoa na Bilionea wa Qatar

abdulahsaf

JF-Expert Member
Joined
Aug 31, 2010
Posts
858
Reaction score
130
[TABLE="width: 491"]
[TR]
[TD="colspan: 3"]Janet Jackson Asilimu, Kufunga Ndoa na Bilionea wa Qatar [/TD]
[/TR]
[TR="bgcolor: #E1E1E1"]
[TD]
4003020483.jpg

Janet Jackson na mpenzi wake bilionea wa Qatar, Wissam Al Mana[/TD]
[TD]Tuesday, November 13, 2012 3:00 PM
Nyota wa muziki wa Marekani na dada wa aliyekuwa mfalme wa muziki wa Pop, Janet Jackson amebadili dini kuwa muislamu na atafunga ndoa ya kifahari na mpenzi wake bilionea wa Qatar, kwa watakaohudhuria kila mmoja atapewa zawadi ya saa ya Milioni 20. [/TD]
[/TR]
[TR]
[TD="colspan: 3"]Dada yake Michael Jackson, Janet Jackson amesilimu kuwa muislamu na atafunga ndoa ya kiislamu na mpenzi wake bilionea wa Qatar, Wissam Al Mana mwanzoni mwa mwaka ujao.

Sherehe ya kukata na shoka ambayo inatarajiwa kufanyika kwenye mji wa Doha, Qatar inatarajiwa kugharimu mamilioni ya dola ambapo bilionea huyo wa Qatar anataka kuifanya harusi yake iingie kwenye historia ya harusi bora kuliko zote duniani.

Kwa mujibu wa taarifa za ndani zilizopatikana Janet na mchumba wake huyo wamepanga kutumia dola milioni 3 kwaajili ya kuwakodishia ndege za kuwaleta wageni wapatao 500 watakaohudhuria harusi hiyo.

Katika kuhakikisha kuwa wanaifanya harusi yao inakuwa ya kifahari zaidi, bilionea huyo wa Qatar amepanga kuwazawadia wageni wote watakaohudhuria sherehe hiyo saa ya kifahari aina ya Rolex yenye thamani zaidi Tsh, milioni 20. Kila mgeni atapata saa hiyo kama shukurani ya kutumia muda wake kuhudhuria harusi hiyo.

"Itakuwa ni harusi ya karne, Wissam amepanga kumwaga pesa kuifanya harusi yake na Janet iwe ya kipekee", alisema mtu mmoja wa karibu na wapenzi hao.

Janet mwenye umri wa miaka 46 alikutana na Wissam ambaye ni mdogo kwa miaka takribani 10 mnamo mwaka 2009 wakati Janet alipotembelea nchi za Mashariki ya kati na kufanya shoo maalumu kwenye nchi hizo.

Janet na Wissam walianza mapenzi yao mnamo mwaka 2010 na walivalishana pete za uchumba mwaka jana ambapo Wissam alimvalisha Janet pete ya uchumba ya almasi yenye carat 15.

"Mama yangu alitulea na kutufundisha tuamini kuwa umri ni namba tu", alisema Janet wakati alipoulizwa kuhusiana na umri wake mkubwa kulinganisha na Wissam.[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD="colspan: 3, align: center"][/TD]
[/TR]
[TR]
[TD="colspan: 3"][/TD]
[/TR]
[/TABLE]
 
This is what Arabs can do with their money!

But well, at least watajifunza kuvaa nguo kutoka kwa Janet (Gold Digger) Jackson.
 
hapa bongo mastar watatu wa kike wa Bongo Movie ndani ya wiki 1 walibadilisha dini na kuolewa uarabuni na ndani ya mwezi wawili kati yao wamesharudi bongo wanaendelea na ufuska na bangi zao baada ya kwenda kuliwa Tigo ya kutosha na kula pesa za bureeee!! likely naye anafuata pesa.
 
The Dude has money to blow,15 carats for da bitch and 500 Rolexs to give it out.
 
Kimsingi hapo hakuna ndoa, zaidi ya kutaka kuweka records. Yes maisha ni mafupi duniani. Ukiacha record ya uhakika unaweza kumbukwa hadi miaka 500 ijayo. Na hiki ndicho watu wanakitafuta
 
hapa bongo mastar watatu wa kike wa Bongo Movie ndani ya wiki 1 walibadilisha dini na kuolewa uarabuni na ndani ya mwezi wawili kati yao wamesharudi bongo wanaendelea na ufuska na bangi zao baada ya kwenda kuliwa Tigo ya kutosha na kula pesa za bureeee!! likely naye anafuata pesa.

una hakika wamefanyiwa hivyo?? una ushahidi... usiseme tu mambo
 
This is what Arabs can do with their money!

But well, at least watajifunza kuvaa nguo kutoka kwa Janet (Gold Digger) Jackson.

so, unachosema janet amefuata pesa kwa huyo jamaa na siyo love?? dude kama ashakuwa muislamu, mavazi tena ya uovu ata achana nayo, inshallah mungu atamsaidia.. ama labda abadili dini kama jina na asifuate uislamu unavyotaka.. hapo itakuwa mtihani.. ila sidhani kama familia ya huyo jamaa kama itakubali


BUT WHAT IS HER NEW NAME??
 
acheni uswahili nyinyi,janet jackson ana 150$ million dollar, and uyo mshkaji ana 200 million dollars,so that proof their relation actually isn't for money kivile,lakini wakuu nakubali point ya kuweka record that all! Follow link hii utajua all thinGs Janet Jackson Net Worth | Celebrity Net Worth
 
Tamaa ya pesa hakuna lolote. Atayaweza maisha ya waarabu? Akat kila siku mother f*cker nying??
 
Back
Top Bottom