KENYAMONTA
New Member
- Sep 23, 2021
- 1
- 0
TAFAKARI NAMI KATIKA MAKALA HII
Kumekuwa na kelele nyingi zinazohusu usawa wa kijinsia, kauli mbiu ikiwa ''Hamsini kwa Hamsini ifikapo 2025''. Kumekuwa na nadharia kuwa wanaume wamekuwa wanawakandamiza wanamke, Tumeshuhudia katika kipindi miaka kumi iliyopita kumekuwa na ongezeko kubwa la wanawake katika nafasi mbali mbali za kiutawala na kitendaji katika serikali na sekta binafsi kwa ujumla amabalo ni jambo zuri kwa usitawi na maendeleo ya nchi yetu, shida yangu kubwa ipo kwenye hamsini kwa hamsini. Mimi binafsi ni muumini mkubwa wa usawa wa kijinsia, lakini usawa nao ufikiria sio wa hamsini kwa hamsini kama watu wengi wanavyodai.
Kimsingi kuna usawa wa aina mbili, namba moja ni usawa wa fursa ambio wazungu huita ''equality of opportunity'' na namba mbili ni usawa wa matokeo ambao ni ''equality of outcome''. Usawa wa fursa unalenga kutengenza mazingira sawa kwa kila mmoja katika jamii bila kujali jinsia yake aweze kunufaika na fursa zilizo katika jamii, kwa mfano kama kuna fursa kumi za ajira basi kuwepo na mazingira rafiki kwa jinsia zote kufikia fursa hizo, usawa wa fursa haulengi kwamba fursa hizo zitaenda kwa nani bali kuna mazingira ambayo ni rafiki kwa jinsia zote kufikia fursa hizo. Lakini upande wa pili amabao ni usawa wa matokeo unalenga katika matokeo zaidi, kwa mfano kama kuna fursa kumi katika jamii basi nafasi tano ziende kwa wanawake na tano ziende kwa wanaume iwe hamsini kwa hamsini.
Naamini wanawake wanakutana na changamoto na vikwazo vingi hasa katika nchi zetu za kiafrika ambapo bado tuna tamaduni ambazo kimsingi kwa hali ya maisha ya sasa hazina uhalisia, lakini je njia bora ya kuondoa changamoto na vikwazo hivi ni hamsini kwa hamsini?. Sidhani kama lengo la hamsini kwa hamsini litafikiwa katika kila sekta, ni rahisi kufikia lengo hili katika siasa kwa sababu chama kinaweza kusimamisha wagombea wake kwa kutumia kigezo cha jinsia kwa malengo ya kisiasa zaidi. Japo sifikirii siku itafika jeshini itakuwa hamsini kwa hamsini au waendesha bodaboda itakuwa hamsini kwa hamsini.
Usawa wa matokeo ambao kimsingi ndio viongozi wetu wanao uhubiri anapelekea kuajiri watu ambao hawana sifa sitahiki kwa kigezo tu cha jinsia tu. Ni vyema serikali ikajikita kakita kujenga usawa wa fursa ambapo jinsia zote zitengenezewe mazingira sawa yakupata fursa zilizopo, kama mtu atateuliwa kuwa uwaziri basi kuteuliwa kwake kuwe ni matokeo ya vigezo alivyo navyo na si sababu ya kutimiza lengo la serikali la hamsini kwa hamsini.
karibu utafakari nami

Upvote
1