Motheojohn
New Member
- Aug 22, 2022
- 1
- 0
JANGA LA NJAA MPWAPWA
Mpwapwa ni wilaya inayopatikana mkoani Dodoma nchini Tanzania , ni wilaya yenye ardhi iinayosifika zaidi Kwa kilimo kikubwa Cha mazao ya biashata na chakula . Baadhi ya mazao yanayopatikana wilayani humo ni kama Mahindi ,Kkaranga,, mtama, alizeti, ufuta, viazi mviringo na maharage .
Licha ya ardhi hiyo kusifika Kwa kilimo Cha mazao mengi lakini ni wilaya qmbayo Kwa miaka ya hivi karibuni (2018-2022) inasumbuliwa na balaa la njaa Kali inayosababishwa na mabadiliko ya hali ya hewa ambayo Kwa kiasi kikubwa wachangiaji wa mabadiliko hayo ni wananchi wa eneo hilo.
Baadhi ya sababu zinazochangia njaa hiyo ni kama zifuatazo
Ukataji ovyo wa miti, hii ni sababu inayopelekea wilaya hiyo kukosa mvua za kutosha kutokana na uharibifu wa kuchoma misitu na kukata miti ovyo katika maeneo ya milima inayopatikana katika maeneo hayo ikiwa milima hiyo ndiyo chanzo kikubwa Cha mvua . Baadhi ya vijiji ambavyo milima yake imaathirika Kwa kiasi kikubwa ni kama vijiji vya kingiti, lukole, mzase, kibakwe, belege , chamtumile na vingine vingi ambavyo hawapati faida tena inayotokana na misitu.
Elimu duni ya kilimo na mazingira , kukosekana Kwa elimu Kwa wananchi au wakulima wa maeneo hayo kunatokana na uchache wa wataalamu wa kilimo na uzembe wa kuhakikisha wanatoa elimu kabla ya msimu wa kilimo , wataalamu wamekuwa wakikagua tu mazao na sio kuwaelekeza wakulima mazao gani yanatakiwa Kutokana na utabili wa Hali ya hewa hivyo wakulima wanalima Kwa uzoefu na sio Kwa mabadiliko ya hali ya hewa lakini pia kutoa elimu kuhusiana na mazingira Kwa ujumla.
Rushwa ,katika wilaya hiyo vitendo vya rushwa vimeshamili baina ya viongozi wa serikali za vijiji pamoja na waharibifu wa mazingira kwani maeneo yaliyo athiriwa yanaonekana Kwa ukaribu lakini pia mara kadhaa misitu imekuwa ikiwaka moto na hakuna hatua zozote zinatoka katika serikali hizo kuhakikisha waharifu wanapelekwa katika mikono ya Sheria , viongozi wamekuwa ni wamiliki wa maeneo hayo yaliyo chomwa moto na kukatwa miti wakiyatumia kama mashamba .
Bei kubwa ya mazao, baada ya kukosekana Kwa mvua nyingi ambazo asilimia 90% ya wananchi wa mpwapwa wanazitegemea zaidi katika kilimo hivyo Bei ya mazao hasa yale ya chakula imekuwa kubwa sana kulingana na uchumi wa wananchi Kwa kipindi hiki Cha njaa kali ambapo Mahindi ya chakula Kwa kilo 20 ni shilingi elfu 20 bei ambayo ni kubwa zaidi Kwa wananchi hao.
Hatua zinazoweza kuchukuliwa Ili kuweza kusaidia wananchi wa wilayani mpwapwa.
Uwajibikaji chanya wa kamati ya mazingira ya wilaya , kamati inatakiwa kuwajibika ipasavyo kwani hakuna tamko lolote ambalo limewahi kutolewa kutoka katika ngazi ya wilaya ambayo inaelimisha wananchi Kwa ujumla pamoja na viongozi wa vijiji husika lakini pia kutembelea mazingira yaliyo athirika Ili kuwasaidia wananchi wa eneo Hilo.
Itolewe elimu ya kutosha ya kilimo kwa wananchi, wakulima wa mpwapwa wangekuwa wanatambua namna ya kuendana na Hali ya hewa wasingejikuta katika balaa hivyo ni lazima wataalamu wa kilimo wahakikishe wanatoa elimu unapofika msimu wa kilimo Ili wakuliwa wajue ni aina gani ya mazao wanapaswa kuyapanda.
Endapo hatua hizi na zingine nyingi ziatafuatwa zitaweza kuwasaidia Kwa kiasi kikubwa wakazi wa wilaya ya mpwapwa kutokana na hiki wanachokipitia , pia itakuwa ni muda muafaka Kwa wakulima hao kujikwamua kiuchumi Kutokana na njaa iliyoshamili Kwa zaidi ya miaka miwili Sasa .

Upvote
0