Janga la pombe kali na anguko la kizazi: Kilio cha wazazi na hatari kwa Taifa

Nilikuwa Msibani Mbahe Marangu kwenye msiba wa Mama wa rafiki yangu mkubwa sana,nakumbuka kama kumbukumbu zangu ziko sahihi ilikuwa September 2024,kuna mbunge wa viti maalum Kilimanjaro alikuwa pia ni rafiki wa familia na alichelewa kidogo kufika Msibani,alicho tueleza pale Msibani ni kwamba walikuwa wako Marangu mtoni kutoa elimu vijana waachane na urahibu wa visungura alisema baada ya presentation alitoa fursa ya kuwasiliza walio muambia sasa yani wakati huo sijui sasa,kuna vijana wengi sana wanalawitiwa kwa ajili ya kununuliwa visungura,malalamiko yake kwa wazazi wa kichaga ni kwamba nani kati ya hao walevi atakae endeleza kizazi,familia na ukoo kama vijana wenyewe ndio hawa,akasihi sana familia mbalimbali na koo zijikite kutoa mafunzo kwa vizazi vyao
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…