Dalili mbaya gani sasa kwani wamefungwa?
Hivi mechi ya Jumatano uliangalia kweli wewe?(Yanga 3 - 1 Mtibwa) Au kwa kua umeona wametoka droo leo na Azam ndo unajua kua Yanga mbovu
Yanga huwa haina mbwembwe waache waongoze ligi Yanga wao ni kuchukua kombe (ushindi) full stop
Yanga inamapungufu katika kiungo.. Toka Haruna kiwango kishuke tunastruggle... Kamusoko ni holding midfielder tunahitaji namba nane mtundu wa kuweza kuwachezesha wakina Ngoma.. Kuna yule dogo ufudu wa kagera sugar nilikuwa namfuatilia toka yuko mgambo ni mzuri sana hata juzi mechi na simba mkude alipata wakati mgumu....Hakuna mchawi Yanga December tafuteni viungo wawili wa kati timu bado nzuri
Kambale fc...hv mzee mzimba Yu wapi?,maana kimbinenga yake na Mzee akilimali ilikuwa balaa,Hawa wazee wameitafuna Sana hela ya manji,wanakinusha harafu wanaelewana na Manji wanayamaliza kiutu uzima...sasa dili la kukodisha timu hajawahusisha mzee Akilimali akakinukisha...