sijui nini
JF-Expert Member
- Sep 29, 2010
- 2,553
- 1,291
MGOMBEA urais kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Jakaya Kikwete, jana alilazimika kukusanya watu kwa mabasi kutoka Arusha mjini kwenda wilayani Karatu kwa ajili ya kuhudhuria mkutano wake wa kampeni.
Habari za kuaminika kutoka Karatu zinasema hali hiyo inatokana na Karatu kuwa ngome ya mgombea urais kwa tiketi ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Dk. Willibrod Slaa.
Dk. Slaa ambaye amekuwa mbunge wa jimbo hilo kwa kipindi cha miaka 15, anaonekana kuliteka jimbo kwa shughuli mbalimbali za maendeleo ambazo amekuwa akizianzisha.
Huwezi kuamini, jana hapa Karatu yaliingia mabasi matano kutoka Arusha yakishusha wafuasi wa CCM kwa ajili ya kuja kujaza watu wa kumsikiliza Kikwete, unajua hapa ni ngome ya CHADEMA ndugu yangu sasa inawezekana walihofu kukosa watu, kilisema chanzo chetu cha habari.
Aidha, chanzo hicho kimesema uongozi wa CCM Mkoa wa Arusha, uliagiza kila mgombea ubunge katika majimbo yote ya mkoa huo kuhakikisha anasafirisha watu kama alivyoagizwa ili waweze kuhudhuria mkutano huo.
Huwezi kuamini mpaka jana nyumba za kulala wageni zilikuwa zimefurika ndugu yangu, utadhani kuna ugeni wa kitaifa hawa jamaa hapa hawakubaliki kabisa, kilisema chanzo chetu.
Katika hatua nyingine, Waziri Mkuu mstaafu, Frederick Sumaye, amekuwa kiongozi kwa kwanza mstaafu kujitokeza hadharani kumnadi Kikwete mbele ya wananchi, tangu kampeni hizo zilipozinduliwa Agosti 21, mwaka huu.
Sumaye aliwataka wananchi wa Karatu kumchagua tena Kikwete ili aweze kutekeleza ahadi ambazo amezitoa kwa ajili ya faida ya taifa.
Mko tayari kumchagua Kikwete Oktoba 31, mwaka huu? Mchagueni ili atimize ahadi alizotoa kwa ajili ya maendeleo ya taifa letu, alisema Sumaye kabla hajapanda jukwaani kumuombea kura Kikwete.
Source: Tanzania Diama
My Take: huyu jamaa bado hajaacha tu hii tabia!???