Janny Sikazwe (aliyezaliwa Mei 26, 1979 Kapiri Mposhi) ni mwamuzi wa soka wa kimataifa wa Zambia.
Safari yake ya mafanikio ya uamuzi aliianza kwenye mashindano ya COSAFA U20 mwaka 2008 wakati alipopewa nafasi hiyo baada ya mwamuzi mmojawapo kushindwa kufaulu mtihani wa Fitness.
Kuanzia hapo amekuwa mmoja wa Waamuzi bora kutoka Bara la Afrika. Anajulikana kwa kuruhusu mpira uchezwe zaidi na sio mtoaji wa kadi za hovyo hovyo.
Mnamo tarehe 20 Novemba 2018, alisimamishwa kwa muda mfupi na Bodi ya Ushauri ya CAF juu ya mashaka ya rushwa baada ya Timu ya Angola ya C.D. Primeiro de Agosto kulalamika, baada ya kupewa kichapo cha mabao 4-2 na Esperance de Tunis katika mchezo wa nusu fainali CAF Champions League.
Hata hivyo baada ya uchunguzi wa CAF ulibaini madai hayo hayana ukweli wowote, Janny Sikazwe aliruhusiwa kuendelea na kazi yake ya Uwamuzi.
Mwamuzi huyu ndiye aliyechezesha mechi ya fainali ya Kombe la dunia la Vilabu kati ya Real Madrid na Kashima Antlers mwaka 2016.
Aliteuliwa kuchezesha mechi za kombe la Dunia mwaka 2018 huko Russia. Mechi alizochezesha ni kati ya Belgium VS Panama (Group G) mechi ilichezwa 18 June, 2018.
Pia alichezesha mechi kati ya Japan VS Poland mechi iliyochezwa 8 June, 2018.
Pia alikuwa mmojawapo wa waamuzi waliochezesha kombe la mataifa ya Afrika mwaka 2015 na 2017.
Ndiye muamuzi pekee aliyeandika historia kutoka nchi ya Zambia kuchezesha mechi za michuano ya kombe la Dunia.
Mbali na uamuzi wa mpira wa miguu, Taaluma yake nyingine ni Mwalimu.
NB: Mwaka 2013 CAF ilibadilisha Mwamuzi wa mchezo kati ya Taifa Stars na Uganda kwa sababu za kiufundi. Mwamuzi aliyeondolewa alikuwa Jean Claude Birumushahu(Burundi) na nafasi yake ikachukuliwa na Herve Kakunze.
Mechi hiyo ilikuwa ni ya mchujo ya kusaka tiketi ya Fainali za Afrika kwa wachezaji wa ligi ya Ndani (CHAN) iliyopigwa Tanzania. Uganda hawakulalamika na Tanzania hawakulalamika. Ni kawaida.