saidoo25
JF-Expert Member
- Jul 4, 2022
- 624
- 1,456
Tumeona siku za karibuni Makamba badala ya kujitika kutatua matatizo makubwa yaliyoko kwenye Wizara yake yanayolalamikiwa wa wananchi kila mahali ikiwemo tatizo la kukatika kwa umeme, kuchelewa kwa miradi ya Rea, lakini ameanza kuwapiga fitna mawaziri wenzake ili waonekane hawafanyi kazi.
Mfano ni tukio la juzi kitendo cha Makamba kumtaka Waziri wa Kilimo Bashe kutolea ufafanuzi suala la Bei ya mbolea wakati suala hilo lilishazungumzwa bungeni na baadae Waziri mwenyewe Bashe akiwa Kilosa alitolea ufafanuzi wote kuhusiana na hatua anazochukua.
Bashe aliweka wazi hatua inazochukua ikiwemo kurudisha mfumo wa unununuzi wa mbolea kwa pamoja, kurejesha utaratibu wa kuweka bei elekezi na kurejesha utaratibu wa usimamizi wa karibu wa Serikali kwenye mbolea ili kuondoa uholela wa wafanyabiashara kuwaumiza wakulima.
Sasa nini kinachomfanya Makamba kuwatengenezea fitina mawaziri wenzake kwa Rais ili waonekane hawafanyi kazi ikiwa yeye wizara yake ndio inaongoza kwa usimamizi mbovu wa Miradi hadi Makamu wa Rais Dk. Philip Mpango aliinyooshea kidole wizara hiyo alipokuwa ziarani Mkoa wa Katavi.