USSR
JF-Expert Member
- Jul 15, 2015
- 10,904
- 26,184
Kutoka kona za ikulu asubuhi ya leo ni kuwa Mheshimiwa January Makamba atangaza kugombea uwenyekiti wa tume ya umoja wa Afrika (AU) kutoka nje ya Umoja wa Afrika Mashariki na SADC baada ya mgombea wa swali Raila Odinga kuamua kujiunga na Serikali ya Wiliam Ruto kama alivyotangaza wiki iliyopita kumsaidia Ruto.
Hapo awali Bwana Odinga aliomba nchi za ukanda wa Afrika Mashariki na kusini kumuunga mkono huku Tanzania ilikubali kabla ya January kutangaza kuwa Tanzania itasema baadaye.
Pia soma: Uteuzi na Utenguzi: Nape, January na Byabato out! Jerry Silaa ahamishiwa Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari
Kwa sasa Januari Makamba atapita kwenye kona za Ikulu za wakuu wa Afrika mashariki na SADC pia kwingineko Afrika na duniani kuomba kuungwa mkono kwa msaada wa Ikulu ya Tanzania.
Wengi walimuona Odinga kama mzee sana kitu kilicholeta ugumu na sasa kete za January inabebwa na diplomasia bora ya Tanzania, urafiki na harakati za ukombozi barani Afrika.
USSR