Januari Makamba: Tanzania hatuna uhaba wa mafuta, tumeshaagiza mengine ya Mei, Juni 2022

Jamani tumsikilize nani sasa kila kukicha ni matamko tu. Nikajua Waziri sasa wewe unakuja kumaliza utata lkn umeishia tu kusema Mafuta yapo yakutosha basi, badala yakumalizia tu sentesi kuwa bei ya mafuta nii..........tujue.

Mnajifanya hamjui concern ya WANANCHI sio uwingi au uchache wa mafuta...Bali ni Bei yake ndio ilifanya Jana baadhi ya watu kujazana vituoni kuhitaji mafuta yakiwa ktk Bei Ile ya Kabla ya kupanda leo.
Ukimuuliza anaelimu gani utasikia Nina masters zaidi ya Moja hivi hizi elimu zenu Zina tusaidia vp wananchi hasa kwa nyinyi tulio wapa mamlaka ? Wananchi Wana lalamikia mfumuko wa bei wewe unakuja na hoja za uhaba wa mafuta namashaka na darasa lake sio Bure aisee.
 
Makamba kumpa wizara nyeti kama hii ni kumuonea bure bora apelekwe sanaa na utamaduni
 
Sasa kama hamna shida mbona yanapanda bei?
 
Ila hii nchi sijui tu hawa watu wamesoma wapi au wakiwa viongozi akili zao wanaziweka wapi kwani?? Ni aibu yani tuna viongozi kama hawa ni mawaziri kabisa dah inasikitisha sana nchi yangu.
 
Pigeni hela tu mtulie. Tuacheni sisi wa daraja la chini tuhangaike na kuteseka.
Mungu alishawapa.
 
aliyeshiba......
 
Ifike wakati, viongozi wa kitaifa waache kuzungumza mambo yasio na tija kwenye jambo la msingi kama hili na linalo gharimu maisha ya wengi.

Wajifunze/ waige nchi jirani kama Kenya na Rwanda jinsi walivyo manage suala la bei ya mafuta.
 
Mi naona Mhe. amefanya sawa tu kutoa tamko maana kulikuwa na tetesi kuwa mafuta nchini yapo machache na nchi inaenda kukosa mafuta...Hii ni ishu tofauti na ishu ya kupanda kwa bei. Hapa alikuwa anajaribu kuwatoa watu katika taharuki ya uhaba kwanza sio bei.
 
Hawa Mawaziri ambao ni mabaki ya Kikwete ni matatizo bei ya mafuta imepanda kutokana na uhaba,bado unajitokeza unasema hakuna uhaba.
Yani matumizi ya siku 27 kwa Nchi hii yote,nayo ni akiba ya kujitosheleza hadi kujigamba??
 
Tozo nyingi kwenda mafuta ni kutokana na Serikali kukosa vyanzo reliable vya kukusanya basi ili wapate fedha kiurahisi wanakimbilia kuweka tozo hizo.

Tanzania tutafute kiongozi atakaye tengeneza uchumi kwa kuongeza shughuli za uzalishaji,watu wazalishe kodi zipatikane haya ya kutegemea tozo za mafuta ya importation ni kuendelea kuua Uchumi wa Nchi.
 
Unadhani hayo malalamiko ya wananchi yeye hayajui?
 
Kimemshinda nini kuunganisha majibu ya hoja zote mbili? Uhaba na Bei?
 

Hilo sahau watu wavivu kama raisi wetu aumize kichww cha kutafuta chanzo cha kupata bajeti ya ya 2trion sahau hilo . Wao wakihitaji pesa wanaifikiria tenesco na hayo mafuta basi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…