January Makamba anaongea kwa vitendo, umeme watengamaa

sasa ulitaka mvua zisinyeshe ? nyie ndiyo huwa mnasababisha mvua zisinyeshe kumbe tushawajuwa
Hujaelewa nilichoandika,na siyo wewe tu bali wengi hawataelewa.Kwanza unaelewa kuwa suala la mvua kunyesha linapaswa kuwa ni mipango ya binadamu na wala siyo kudra?Pia unaelewa kuwa Taifa haliwezi kuendelea kwa kutegemea kudra?
 
Tuwe wakweli hapa. Tatizo la kukatika kwa umeme lilianza alipoingia yeye uongozini. Kuhalalisha tatizo akasema tatizo ni la mwendazake. Sasa imekuwaje achukue sifa za kuutengemeza tena?
Bwala la JHPP likamilke hata kama hataki. Halafu ndio zianze hizi hadithi nyingine
 
Bila shaka mtoa maada unafanya utafiti kwa namna ya kumsifia waziri ili ufahamu tatizo la umeme kukatika katika kama bado lipo. Mimi nakujibu tu kwa ufupi. TATIZO LIZOELEKA SAIZI
 
HUU NI UONGO WA KIWANGO CHA LAMI UMEME BADO UNAKATIKA SANA TU HALAFU HAWATOI HATA TAARIFA UNASHANGAA MARA PAAAP.

NAWAKANYA TANESCO MKIUNGUZA VITU TUNAPELEKANA MAHAKAMANI.
 
Alidai Mashine ziliwashwa mfululizo bila kuzimwa for routine maintenance so mitambo ikawa worn out.

Umeme ulikatika katika sababu ya ukame na hizo scheduled maintenance.

Solution ilikia utilization ya mabwawa yaliyobakia na kuongeza vituo vya umeme wa gesi.

Sasa umeme umeanza kutengemaa taratibu bado mnakejeli? Ameomba muda subirini walau mpaka january ndio mumkosoe. Mtu hana hata siku 100 tayari kukatishana tamaa!!

We are not being fair
 
Reactions: Tui
Nafikiri huku kuimba sifa hewa ni upungufu wa maadili na heshima kwa waTanzania bila sababu; hivi unathubutuje kusema hivyo wakati Mbeya na Iringa kila baada ya nusu saa umeme unakatika bado unaleta kelele za sifa za ovyo kwenda kwa mtu ambaye hana uwezo wa kutatua tatizo zaidi ya siasa zenye maslahi?
 

Dah huku niliko wameacha kukata.....makamba ameanza vizuri
 
Hakuna fairness mzee sisi tunataka umeme sio porojo. Na kazi zenye weledi na kujari maslahi mapana ya nchi
 
Kelele zeru ndiyo zimesaidia.

Hakuna bwawa lililokuwa limekauka. Mvua zilinyesha mfurulizo tena kwa kiwango cha juu hivyo kwa hicho kipindi kifupi mabwawa yasingekauka.

Kelele zetu zimezima ndoto za. January
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…