Mkalukungone mwamba
JF-Expert Member
- Aug 29, 2022
- 862
- 1,755
Hatimaye alikuwa kimya sana tangu ameteguliwa lakini sasa January Makamba ameibuka kwenye kampeni za kuwanadi wagombea wa chama chake CCM
=====================
Mbunge wa Jimbo la Bumbuli ambaye pia ni Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Taifa, January Makamba amesema chama hicho kinajivunia ubora wa wagombea wake, sera bora, na rekodi nzuri ya uongozi, vitu ambavyo vinakipa chama hicho nafasi kubwa ya kushinda katika uchaguzi wa serikali za mitaa utakaofanyika Novemba 27, 2024.
Akizungumza wakati wa kuwafanyia kampeni wagombea wa CCM Jimboni Bumbuli mkoani Tanga, Makamba ameeleza kuwa mchakato wa upatikanaji wa wagombea ndani ya chama umejikita katika kuhakikisha wanachaguliwa viongozi bora kupitia mchujo wa kina.
Soma Pia: Special Thread: Orodha ya Mijadala ya Mikoa yote Tanzania Bara inayoshiriki katika Uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2024
"Sisi CCM tunaamini kwamba kwenye Chama Cha Mapinduzi tunazo turufu kadhaa ambazo zinatubeba kuhakikisha kwamba tunashinda. Moja ni ubora wa wagombea. Sisi tuna namna ambavyo tunawapata wagombea wetu, kwanza wanapigiwa kura, pili wanapitishwa na vikao, na kikao cha mwisho kabisa ni Halmashauri Kuu ya Wilaya, ambayo ina watu wengi. Kwahiyo, mkimkuta mgombea hapa labda anayegombea uenyekiti wa kijiji, amepitishwa na watu wengi zaidi, amepitishwa kwenye mchujo zaidi, kwahiyo mnakuwa na uhakika kuwa yeye ni bora. Kwa hiyo tunajivunia na ubora wa wagombea," amesema Makamba.
Ameongeza kuwa sera za CCM zimeendelea kuwashawishi wananchi kwa kuwa zinahusu moja kwa moja maisha yao ya kila siku, hasa kupitia programu za maendeleo vijijini.
"Tunajivunia na sera nzuri. Tunawaeleza wananchi nini tutafanya, na sisi Chama Cha Mapinduzi tuna programu yetu ya maendeleo ya watu katika vijiji vyetu. Kwahiyo ni rahisi zaidi kuwaeleza na kuwashawishi kwa sababu ni mambo yanayowahusu," amesisitiza na kuongeza,
"Tunayo rekodi nzuri ya kuwa na wagombea tayari ambao wameongoza vizuri,"