Pre GE2025 January Makamba: Kura za CCM uchaguzi Mkuu kuwa zaidi ya 90%

Pre GE2025 January Makamba: Kura za CCM uchaguzi Mkuu kuwa zaidi ya 90%

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)

Chachu Ombara

JF-Expert Member
Joined
Dec 11, 2012
Posts
6,067
Reaction score
10,938
Akizungumza leo, Jumatatu, Februari 24, 2025, katika mkutano wa hadhara wilayani Lushoto, Makamba amesema kuwa uzinduzi wa jengo la Halmashauri la Bumbuli ni kielelezo cha shukrani na mapenzi ya wananchi wa Bumbuli kwa Rais Samia na Serikali yake.

"Umeona umati mkubwa wa watu waliokusanyika hapa leo. Hii ni ishara ya jinsi ambavyo wananchi wa Bumbuli wanavyothamini kazi yako na jinsi ambavyo maendeleo yaliyofanyika katika kipindi cha miaka minne ya uongozi wako yameinua maisha ya watu wetu," alisema Makamba, akisisitiza kuwa miradi ya maendeleo pekee imeweza kuboresha miundombinu na kuongeza fursa za kiuchumi katika mkoa wa Tanga.

Vilevile Makamba amekumbusha kuwa kwa miaka 20, wananchi wa Bumbuli walikuwa wakililia ujenzi wa barabara ya Soni–Bumbuli–Dindira–Korogwe, na kwamba hivi karibuni Serikali ilikubali ujenzi wa barabara hiyo kwa kiwango cha lami, hatua ambayo itarahisisha usafiri na kukuza uchumi wa eneo hilo.

"Kwa miaka mingi, barabara hii ilikuwa ni changamoto kubwa kwetu. Lakini juzi, takribani wiki tatu zilizopita, tumepokea taarifa kuwa barabara hii itajengwa kwa kiwango cha lami. Hii ni habari njema kwa wananchi wa Bumbuli na kwa wananchi wa Lushoto kwa ujumla. Utakuwa umeacha historia kubwa sana katika milima hii ya Usambara," alisema Makamba.

Akielezea mabadiliko yaliyoletwa na uongozi wa Rais Samia, Makamba alikumbusha historia ya matokeo ya uchaguzi wa Rais, akisema kuwa tangu mwaka 1995, kura za urais kwa mgombea wa CCM zimekuwa juu, na hivyo ataendelea kushikilia nafasi hiyo kwa asilimia kubwa katika uchaguzi ujao kutokana na mafanikio ya Serikali ya Rais Samia. "Milima hii ni milima ya CCM, na mwaka huu hatutashuka chini ya asilimia 90 kwa kura za CCM," alisema Makamba, akitaja mafanikio ya Rais Samia kama motisha kwa wananchi kuendelea kumchagua.

Pia soma: Pre GE2025 - Rais Samia: Nilimpiga kikofi January leo namrudisha kwa mama

Pia, Makamba alitumia fursa hiyo kumshukuru Rais Samia kwa kumteua kushika nafasi muhimu katika Serikali, akitaja nafasi ya Waziri wa Nishati na baadaye Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, akisema kuwa uzoefu alioupata katika nafasi hizo umejenga uwezo wake kama kiongozi.

"Umejenga uwezo wangu katika utumishi wa umma, na hii ni heshima kubwa ambayo nitabaki nayo maisha yangu yote," aliongeza Makamba.
 
Back
Top Bottom