Japan alipigwa kwa nyuklia lakini ni rafiki mkubwa wa Marekani. Ni kwa sababu gani?

Webabu

JF-Expert Member
Joined
Apr 29, 2010
Posts
8,870
Reaction score
14,258
Katika vita vya pili vya dunia 1945 Japan ilipigwa kwa silaha mbaya ya nyulkia na Marekani na ikabidi isalimu amri.

Silaha hiyo ndiyo ilikuwa mara ya mwanzo kutumika kwenye visiwa vyake vya Hiroshima na Nagasaki.

Watu wake wengi kwa mamia walikufa papo hapo na athari za vita hivyo bado zinaendelea. Jambo la kushangaza baada ya tukio hilo Japan imekuwa bega kwa bega na Marekani na hata kuunda ushirika dhidi ya nchi nyengine.

Kuna faida Japan inayopata,ni woga wake au ni ukarimu tu wa watu wake.

1665659085358.png
 
Kuna faida Japan inayopata,ni woga wake au ni ukarimu tu wa watu wake.
Mkuu Japan 🇯🇵 Ilipopigwa kuanzia mwaka 1945-52 ilikaliwa kimabavu na Marekani kisha ilisainishwa mkataba wa amani uliokuwa na vipengele vingi, vichache kati ya hivyo ni;

Kulipa fidia (baadhi ya nchi zilisamehe), kuachia makoloni yake yote, kukubali makosa yote ya kivita iliyoshitakiwa kwayo na mahakama ya kijeshi, kuyapendelea mataifa ya ‘Allied Powers’ katika biashara n.k

Lakini Marekani ilibadili gia, ikaanza kukuza uchumi wa Japan 🇯🇵 lengo kuu ni kuzuia vimelea vya ukomunist kuota mizizi ndani ya Japan 🇯🇵.

Na baadae Marekani ikaunda mfumo kati ya nchi za New Zealand, Australia, Korea Kusini, Japan na Marekani wa kiulinzi na kibiashara wanaouita ‘San Francisco System’.

Leo hii Japan 🇯🇵 ni mshirika wa karibu sana wa Marekani kwa sababu hizo.

FAIDA AU UOGA?
Ni faida Mkuu, Japan 🇯🇵 inanufaika sana kiuchumi (ninaeleza hapa chini) na kiulinzi.
Lakini pia inapata hasara fulani fulani.

Sababu za kufufuka kwa Uchumi wa Japan 🇯🇵
Binafsi nitaziweka katika makundi mawili
1) Za ndani
2) Za nje

1) Za ndani - Kundi la kwanza nitaachana nalo ila kwa kifupi ni kuhusu sera za ndani kama vile kuhamasisha wanawake kufanya kazi.

2) Za nje - Hapa hoja kubwa na Vita vya Korea (1950-53).
Vita hivyo vilipoanza Marekani ilitumia ushawishi wake kuiingiza UN vitani kuilinda Korea Kusini, na kutokana na jiografia ya Korea ilivyo ambapo Magharibi ilipakana na China 🇨🇳 (Wakomunist), Kaskazini na Korea Kaskazini 🇰🇵 (Wakomunist) mashariki na Bahari ya Pasifiki na visiwa vya USSR (Wacomunist), Kusini na Bahari tena na Japan 🇯🇵 iliyodorora kiuchumi.

Kwa Marekani adui alikuwa ni Wakomunist hivyo kijeshi ilikua ni ‘logical’ wao kuiwezesha Japan Kiuchumi hasa kufufua viwanda ambavyo vilizalisha silaha na mahitaji ya kutosha kwaajili ya vikosi vya UN na Marekani huko Korea. Na kwa mpango huu Marekani 🇺🇸 Iliweza kufupisha ‘supply line’ hivyo kuiwezesha kupambana vizuri kwenye rasi ya Korea.

Mpango wa kufufua viwanda vya Japan 🇯🇵 uliisaidia sana Japan 🇯🇵 maana viwanda vyake vilizalisha bidhaa nyingi zikiwemo silaha na kupata soko la uhakika.

Kuanzia kipindi hiko wachumi wanaeleza 🇯🇵 Ilikuwa kwenye kipindi cha “Economic Boom” mpaka miaka ya 1970.

Nafikiri nimejibu swali lako.
 
.Hata kama kutakuwa na zaidi ya hayo na wewe umejitahidi kufafanua.
 
Waligeuka na kuwa marafiki baada ya kuwa na itikadi moja ya kibepari

Nchi za Ulaya wao bifu yao ipo katika itikadi tu hata kama mlipigana

Mfano Ujerumani na Ulaya Magharibi (Uingereza, Ufaransa, Ubelgiji, Poland n.k) hizi nchi zilikuwa maadui wakubwa kipindi cha WW2 ila sasa ni marafiki wakubwa wapo wote kwenye EU sababu wana itikadi inayofanana

Marekani na China na Urusi walikuwa upande mmoja wakati wa WW2 na Marekani alimsaidia China kumpiga Japan ambaye alikuwa adui wake mkubwa, ila sasa Marekani, China na Urusi ni mahasimu sababu ni hiyo hiyo itikadi
 
Mkuu Japan 🇯🇵 Ilipopigwa kuanzia mwaka 1945-52 ilikaliwa kimabavu na Marekani kisha ilisainishwa mkataba wa amani uliokuwa na vipengele vingi, vichache kati ya hivyo ni;

Kulipa fidia (baadhi ya nchi zilisamehe), kuachia makoloni yake yote, kukubali makosa yote ya kivita iliyoshitakiwa kwayo na mahakama ya kijeshi, kuyapendelea mataifa ya ‘Allied Powers’ katika biashara n.k

Lakini Marekani ilibadili gia, ikaanza kukuza uchumi wa Japan 🇯🇵 lengo kuu ni kuzuia vimelea vya ukomunist kuota mizizi ndani ya Japan 🇯🇵.

Na baadae Marekani ikaunda mfumo kati ya nchi za New Zealand, Australia, Korea Kusini, Japan na Marekani wa kiulinzi na kibiashara wanaouita ‘San Francisco System’.

Leo hii Japan 🇯🇵 ni mshirika wa karibu sana wa Marekani kwa sababu hizo.

FAIDA AU UOGA?
Ni faida Mkuu, Japan 🇯🇵 inanufaika sana kiuchumi (ninaeleza hapa chini) na kiulinzi.
Lakini pia inapata hasara fulani fulani.

Sababu za kufufuka kwa Uchumi wa Japan 🇯🇵
Binafsi nitaziweka katika makundi mawili
1) Za ndani
2) Za nje

1) Za ndani - Kundi la kwanza nitaachana nalo ila kwa kifupi ni kuhusu sera za ndani kama vile kuhamasisha wanawake kufanya kazi.

2) Za nje - Hapa hoja kubwa na Vita vya Korea (1950-53).
Vita hivyo vilipoanza Marekani ilitumia ushawishi wake kuiingiza UN vitani kuilinda Korea Kusini, na kutokana na jiografia ya Korea ilivyo ambapo Magharibi ilipakana na China 🇨🇳 (Wakomunist), Kaskazini na Korea Kaskazini 🇰🇵 (Wakomunist) mashariki na Bahari ya Pasifiki na visiwa vya USSR (Wacomunist), Kusini na Bahari tena na Japan 🇯🇵 iliyodorora kiuchumi.

Kwa Marekani adui alikuwa ni Wakomunist hivyo kijeshi ilikua ni ‘logical’ wao kuiwezesha Japan Kiuchumi hasa kufufua viwanda ambavyo vilizalisha silaha na mahitaji ya kutosha kwaajili ya vikosi vya UN na Marekani huko Korea. Na kwa mpango huu Marekani 🇺🇸 Iliweza kufupisha ‘supply line’ hivyo kuiwezesha kupambana vizuri kwenye rasi ya Korea.

Mpango wa kufufua viwanda vya Japan 🇯🇵 uliisaidia sana Japan 🇯🇵 maana viwanda vyake vilizalisha bidhaa nyingi zikiwemo silaha na kupata soko la uhakika.

Kuanzia kipindi hiko wachumi wanaeleza 🇯🇵 Ilikuwa kwenye kipindi cha “Economic Boom” mpaka miaka ya 1970.

Nafikiri nimejibu swali lako.
Tena Marekani ndio alimsaidia China kuipiga Japan ambayo ilikuwa katili sana kwa China
Na kuisadia Urusi kumpiga Hitler aliyeua Warusi Milioni 20
 
Nikuibie tu siri kuwa kamwe Mjapani na Mmarekani hawajawahi kuiva na hawataiva chungu kimoja.

Niliwahi kuwaona wakiwa kwenye apartment flani hapa DAR walikuwa hawasalimiani na wakati mwingine walikuwa wakielekea kugongana kwenye njia 1 mmojawapo alikuwa akidiriki kuhama njia kabisa wakiwa wamenuniana.
 
Katika vita vya pili vya dunia 1945 Japan ilipigwa kwa silaha mbaya ya nyulkia na Marekani na ikabidi isalimu amri.

Silaha hiyo ndiyo ilikuwa mara ya mwanzo kutumika kwenye visiwa vyake vya Hiroshima na Nagasaki.

Watu wake wengi kwa mamia walikufa papo hapo na athari za vita hivyo bado zinaendelea. Jambo la kushangaza baada ya tukio hilo Japan imekuwa bega kwa bega na Marekani na hata kuunda ushirika dhidi ya nchi nyengine.

Kuna faida Japan inayopata,ni woga wake au ni ukarimu tu wa watu wake.

View attachment 2385825
Shukrani Sana mkuu
 
Unasahau alienza kumpiga america alikuwa ni nani? pearl harbour attack?
Ile ilikuwa retaliation ya america kwa japan.. na vile walitaka irohito ajiuzulu kwa namna yoyote ile.

Both zili agree kutokurudia kile kitu. Wamekuwa wakisaka amani tu
 
Marekani ndio imemfundisha Japan mambo mengi ambayo imefanya Japan ifike hapo ilipo leo.

Technology nyingi anayotumia mjapani ameitoa Marekani na ndio msingi wa uswahiba wao mkubwa na ni hivyo hivyo kwa Israel, Germany, Uingereza, Ufaransa, South Korea na hata China.
 
Shortly and clear baada ya maangamizi marekani alitoa fidia ya kusomesha technology ya kuunda magari kupewa soko kwenye taasisi za UN,na baadhi ya nchi ukipata msaada kama kuna budget ya magari unaelekezwa Japan kwa lazima
Mfano Nyerere alipowasaidia wengine kupata Uhuru angewaingiza mikataba ya kununua hata vitumbua na maandazi kutoka Tanzania...lakini sasa nothing, nonsense.....
 
Rekebisha hapo Japan hakuwahi kupigwa na Nuclear na hakuna nchi iliyo wahi kupigwa na Nuclear.
Japan ilipigwa na Atomic bomb sasa hapo kasome mambo ya urutubisha wa madini ya Uranium.
Samahani lakini sina muda wa kutosha kukuelezea.
Atomic bomb ni nuclear bomb hiyo fanya tafiti uone .
 
Waswahili wanasema if you can't beat them join them. Baada ya little boy na fat man kuangushwa Japan alilegea hakuwa na nguvu tena ya kupambana nao ila kujiunga nao
 
Shortly and clear baada ya maangamizi marekani alitoa fidia ya kusomesha technology ya kuunda magari kupewa soko kwenye taasisi za UN,na baadhi ya nchi ukipata msaada kama kuna fungi LA magari unaelekezwa Japan kwa lazima
Mfano Nyerere alipowasaidia wengine kupata Uhuru angewaingiza mikataba ya kununua hata vitumbua na maandazi kutoka Tanzania...lakini sasa nothing, nonsense.....

[emoji23][emoji23][emoji23] mkuu leo ni Nyerere Day punguza hasira kidogo
 
Katika vita vya pili vya dunia 1945 Japan ilipigwa kwa silaha mbaya ya nyulkia na Marekani na ikabidi isalimu amri.

Silaha hiyo ndiyo ilikuwa mara ya mwanzo kutumika kwenye visiwa vyake vya Hiroshima na Nagasaki.

Watu wake wengi kwa mamia walikufa papo hapo na athari za vita hivyo bado zinaendelea. Jambo la kushangaza baada ya tukio hilo Japan imekuwa bega kwa bega na Marekani na hata kuunda ushirika dhidi ya nchi nyengine.

Kuna faida Japan inayopata,ni woga wake au ni ukarimu tu wa watu wake.

View attachment 2385825
Historia inasema Japan ndie alie anzisha vita na ndie alie anza kumpiga mwenzake baada ya kuonywa sana Marekani akataka maliza vita ndio vile vi twin akadondoshewa. Ila baada ya Vita kila mtu akubali makosa na Marekani skatengeneza ushirika mtakatofu na Japan. Ushirika huwo umeifanya Japan kuwa na moja ya products huwezi zipata nchi yeyote na moja wapo ni mauzo ya magari ktk dunia. Nenda popote Japan ni number one china atasubiri sana mpaka miaka 200
 
Katika vita vya pili vya dunia 1945 Japan ilipigwa kwa silaha mbaya ya nyulkia na Marekani na ikabidi isalimu amri.

Silaha hiyo ndiyo ilikuwa mara ya mwanzo kutumika kwenye visiwa vyake vya Hiroshima na Nagasaki.

Watu wake wengi kwa mamia walikufa papo hapo na athari za vita hivyo bado zinaendelea. Jambo la kushangaza baada ya tukio hilo Japan imekuwa bega kwa bega na Marekani na hata kuunda ushirika dhidi ya nchi nyengine.

Kuna faida Japan inayopata,ni woga wake au ni ukarimu tu wa watu wake.

View attachment 2385825
hakunaga ujanja mbele ya shida
 
Back
Top Bottom