Japan imeanzisha ushirikiano mkubwa zaidi na Tanzania kibiashara na wekezaji

Japan imeanzisha ushirikiano mkubwa zaidi na Tanzania kibiashara na wekezaji

Herbalist Dr MziziMkavu

JF-Expert Member
Joined
Feb 3, 2009
Posts
42,872
Reaction score
34,363
Japan imeanzisha ushirikiano mkubwa zaidi na Tanzania kibiashara na wekezaji

10-aug-japan2.jpg




Japan imeanzisha ushirikiano mkubwa zaidi na Tanzania ambapo nchi hiyo itaifanya Tanzania kuwa kitovu cha biashara na uwekezaji katika Afrika kwa nia ya kuiwezesha kuwa na uchumi ulioimarika na wenye kuzalisha ajira nyingi kwa wananchi.

Uamuzi huo wa Japan ni matunda ya mazungumzo kati ya Rais Jakaya Kikwete na waziri mkuu wa Japan, Mh. Shinzo Abe yaliyofanyika Tokyo, Japan wakati rais Kikwete alipotembelea nchi hiyo Juni, mwaka huu, 2013. Msimamo mpya

wa Japan umetangazwa rasmi Agosti 10, 2013 na waziri wa uchumi, biashara na viwanda wa nchi hiyo, Mheshimiwa Toshimistu Motegi alipokutana na kufanya mazungumzo na rais Kikwete, Ikulu, Dar es Salaam.

Kwa upande wa Tanzania, mazungumzo hayo yamehudhuriwa na waziri wa nchi ofisi ya waziri mkuu uwekezaji na uwezeshaji Dr. Mary Nagu, waziri wa viwanda na biashara Dkt. Abdallah Kigoda na waziri wa uchukuzi Dkt. Harrison Mwakyembe.

Waziri Motegi amemwambia rais Kikwete kuwa ametumwa na waziri mkuu Abe kufuatilia mazungumzo kati yao na kutangaza rasmi kuwa Japan imeiteua Tanzania kuwa nchi lengwa na kitovu cha uwekezaji wa Japan katika Afrika mashariki na katika Afrika kwa jumla.

Waziri Motegi pia amemwambia rais Kikwete kuwa pia amekuja Tanzania kutoa taarifa kuwa Japan iko tayari kushiriki katika kuifanya ya kisasa zaidi reli ya kati kwa kujenga njia ya kimataifa badala ya njia nyembamba ya sasa. aidha,

Mheshimiwa Motegi ametangaza kuwa Japan itashiriki katika upanuzi na uboreshaji wa bandari ya Dar es Salaam kwa kuifanya ya kisasa zaidi.

Waziri Motegi amesema katika azma ya Japan ya kuifanya Tanzania nchi ya mfano katika Afrika katika uwekezaji na uchumi ulioimarika,amekuja na kundi la wafanya biashara wa Japan ambao wanaendelea kufanya mazungumzo na

wafanyabiashara wa Tanzania kuona jinsi gani wanavyoweza kusaidiana katika kuwekeza katika uchumi wa Tanzania.
Waziri huyo pia amesema moja ya malengo ya uamuzi huo wa Japan ni kuhakikisha kuwa bidhaa ambazo kwa sasa

zinanunuliwa moja kwa moja kutoka Japan zitazalishwa hapa nchini katika viwanda ambavyo vitajengwa na makampuni ya japan ambapo kwa kuanzia makampuni mawili ya honda na panasonic yamekubali kujenga viwanda nchini kimoja kwa ajili ya kutengeneza pikipiki za honda hapa hapa nchini na kingine kwa ajili ya kutengeneza vifaa vya umeme.



chanzo.
:: Japan Imeanzisha Ushirikiano Mkubwa Zaidi Na Tanzania Kibiashara Na Wekezaji

 
Last edited by a moderator:
Ujio huu ni jambo zuri sana kwa Tanzania; japan siyo wababishaji na wabinafsi sana kama Wachina. Unakumbuka miaka ya nyuma sana tulikuwa na Matsushita ikiwa inatengeza redio na betri za ubora wa juu sana hapa hapa Dar. Wakija kutengeza Piki piki za Honda, Consumer electronics pamoja na magari basi tutaneemeka sana, na tutakomboka kutoka kwenye unyanyasaji wa wachina.
 
Back
Top Bottom