Japan yatengeneza app ya kushangilia ili wachezaji wasiwe wapweke viwanjani

Japan yatengeneza app ya kushangilia ili wachezaji wasiwe wapweke viwanjani

Analogia Malenga

JF-Expert Member
Joined
Feb 24, 2012
Posts
5,108
Reaction score
10,191
Kutokana na janga la #COVID19 watu hawataruhusiwa kuingia viwanjani kushangilia michezo mbalimbali itakayokuwa inaendelea

Yamaha wametengeneza ‘Application’ itakayosaidia kufanya michezo mbalimbali kuendelea kushangiliwa bila watu kuwepo uwanjani

Watakaokuwa wanafuatilia michezo watatumia ‘app’ hiyo na kubofya sauti wanayoitaka, iwe ni kuzomea, kupiga makofi au kushangilia na sauti zitatumwa kwenye spika zilizoko uwanjani kunakoendelea michezo

Hiromi Yanagihara, kutoka kwenye idara ya mikakati amesema aliwaza sana kuhusu wachezaji kuwa uwanjani bila shangwe za mashabiki na ndio sababu ya kufikiria kutengeneza ‘app’ hiyo

Tangazo la hali ya hatari limeondolewa Mei 25 na michezo inatarajiwa kuendelea, Julai 19 ligi ya baseball itaendelea na ligi za mpira wa miguu itafuata baadae

 
Back
Top Bottom