chinchilla coat
JF-Expert Member
- May 16, 2016
- 5,107
- 10,969
Mara nyingi naegemea Upinzani Ila leo nawapongeza CCM kwa walivyoanza kampeni zao. Hawajawashambulia Wapinzani kwa kejeli au matusi kama ilivyokuwa mwaka 2015 ambapo Lowassa alitukanwa sana kuhusu Afya yake, ambaye Sasa hivi wapo naye huko.
Lakini tangu waanze mpaka sasa naona Magufuli akielezea tu kazi alizofanya na kuahidi atakazofanya endapo atachaguliwa, wapambe wake wengi nao hawajajilita kushambulia Sana Wapinzani
Japokuwa kuna vijembe mara moja moja Ila sio mbaya Ila Kuna tatizo Huko Mara ambapo nimesika yupo mpiga kampeni kamtukana mgombea wa Upinzani m*alaya nadhani chama kitamkemea.
Nashauri Upinzani pia usijikite sana kumshambulia Magufuli, japo najua Ni lazima ashambuliwe sababu ndio mtendaji mkuu wa Serikali, lakini akosolewe kisera zaidi.
Ikiwa hivi kampeni zetu zitakuwa za kistaarabu kuliko za nchi nyingi Africa Mashariki na pengine nitapata pride ya kuwa Mtanzania tena.