Japo ni mtoto wa kike, Nataka nijiajiri kwa kuendesha bajaj

Blues1

JF-Expert Member
Joined
Feb 14, 2015
Posts
663
Reaction score
1,412
Habari wakuu
Rejea kichwa cha uzi hapo juu.

Mimi msichana nimemaliza chuo ambapo mpaka dakika hii ajira zimekuwa ngumu kiasi kwamba nmekata tamaa ya kutimiza ndoto zangu za kuajiriwa.

Kinachoniuma zaidi baba yangu ana bajaj nne ambazo ameajiri watu ambao wanaendesha familia kwa kazi hiyo. Kutokana na mimi kuwa msimamizi wa biashara zake nimekumbana na mfanyakaz ambae ni msumbufu asiethamini ajira yake kiasi kwamba napata hasira maana kazi anayo ila anaichezea.wakati wengine tunahangaika kutafuta usiku na mchana.
Hilo jambo limenifanya nifikirie kwenda kuchukua course fupi ya udereva ili nichukue bajaj niiendeshe mwenyewe huku mzazi wangu akijipatia kipato chake kama kawaida maana nina uhakika hii kazi inalipa vizuri.

Nimeshaongea na baba japo ananionea huruma kama mzazi ila maamuzi makubwa yapo kwangu mwenyewe.

Kinachonikwamisha ni hali ya hii industry kutawaliwa na wanaume pekee.
Je sitaonekana mtu wa ajabu mtoto wa kike kuendesha bajaj?
Naombeni ushauri
 
unaweza ukaifanya ila uwe makini sana na njia unazoenda.. na saa 12 jion paki ukalale.. wanawake rahisi kudanganyika na mna mioyo laini mtu anaweza akatumia hiyo advantage kukuibia bajaj .. angalau wanaume machale machale mengi..
 
Habari wakuu
Rejea kichwa cha uzi hapo juu.
Mimi msichana nimemaliza chuo ambapo mpaka dakika hii ajira zimekuwa ngumu kiasi kwamba nmekata tamaa ya kutimiza ndoto zangu za kuajiriwa.
Kinachoniuma zaidi baba yangu ana bajaj nne ambazo ameajiri watu ambao wanaendesha familia kwa kazi hiyo. Kutokana na mimi kuwa msimamizi wa biashara zake nimekumbana na mfanyakaz ambae ni msumbufu asiethamini ajira yake kiasi kwamba napata hasira maana kazi anayo ila wanaichezea.wakati wengine tunahangaika kutafuta usiku na mchana.
Hilo jambo limenifanya nifikirie kwenda kuchukua course fupi ya udereva ili nichukue bajaj niiendeshe mwenyewe huku mzazi wangu akijipatia kipato chake kama kawaida maana nina uhakika hii kazi inalipa vizuri.
Nimeshaongea na baba japo ananionea huruma kama mzazi ila maamuzi makubwa yapo kwangu mwenyewe.
Kinachonikwamisha ni hali ya hii industry kutawaliwa na wanaume pekee.
Je sitaonekana mtu wa ajabu mtoto wa kike kuendesha bajaj?
Naombeni ushauri
Acha uoga,Dodoma nimeona wawili wakifanya hiyo kazi tena ilikuwa ni usiku...
 
Dodoma nishakutana nao kama wawili au watatu
Kilimanjaro (bomang'ombe ) m ishakutana nae mmoja
Kwahio ww sio first au last , kuna wanaosukuma semi za mizigo mpk Congo kwahio acha uoga.
Kuna wengine ni makonga nilimkuta moshi mjini.
Na mwingine ni dereva wa haice nilimkuta arusha
 
Habari wakuu
Rejea kichwa cha uzi hapo juu.

Mimi msichana nimemaliza chuo ambapo mpaka dakika hii ajira zimekuwa ngumu kiasi kwamba nmekata tamaa ya kutimiza ndoto zangu za kuajiriwa.

Kinachoniuma zaidi baba yangu ana bajaj nne ambazo ameajiri watu ambao wanaendesha familia kwa kazi hiyo. Kutokana na mimi kuwa msimamizi wa biashara zake nimekumbana na mfanyakaz ambae ni msumbufu asiethamini ajira yake kiasi kwamba napata hasira maana kazi anayo ila anaichezea.wakati wengine tunahangaika kutafuta usiku na mchana.
Hilo jambo limenifanya nifikirie kwenda kuchukua course fupi ya udereva ili nichukue bajaj niiendeshe mwenyewe huku mzazi wangu akijipatia kipato chake kama kawaida maana nina uhakika hii kazi inalipa vizuri.

Nimeshaongea na baba japo ananionea huruma kama mzazi ila maamuzi makubwa yapo kwangu mwenyewe.

Kinachonikwamisha ni hali ya hii industry kutawaliwa na wanaume pekee.
Je sitaonekana mtu wa ajabu mtoto wa kike kuendesha bajaj?
Naombeni ushauri

Hapana, kitu kikubwa ni ujue kuendesha kwanza ili uwe unaendesha kwa umakini, na uwe na lugha nzuri kwa wenzako na wateja. Nina imani utafanikiwa sana kwenye hii biashara, hongera na fanya kama utakavyo.
 
Kila la heri mamy
Mungu akutangulie
Uwe makini tu
Kupelekwa mbali mahali usipopajua na kutembea usiku usijaribu
 
Back
Top Bottom