Jaribio la kuiba dhahabu katika mgodi wa Geita (GGM) lazimwa

papason

JF-Expert Member
Joined
Sep 14, 2010
Posts
5,119
Reaction score
5,698
Jaribio la kutaka kuiba kiasi kikubwa sana cha dhahabu ktk mgodi wa Geita mchana huu mida ya 11:30hrs na watu wenye silaha nzito za kivitaa limezimwa na walinzi wa mgodi (snipers & quick respond unit force wakishilikiana na makomandoo walinzi wa ndege inayosafirisha dhahabu) mpaka mida hii imethibitika watu 2 wamepoteza maisha.

Jaribio hilo limefanyika Ktk airport ya mgodini wakati dhahabu hiyo ikipakiwa ktk ka ndege special tayari kwa kusafirishwa kwenda South Africa, hadi mida hii wana Geita bado tunasikia milio ya risasi zikilindima maporini na ving'ora vya ambulance za mgodini zikiwabeba majeruhi wengi wao ni walinzi wa wa mgodi, polisi walitarifiwa mapema kabisa lakini bado wanajipanga namna ya kufika eneo la tukio!


Tutazidi kuajuza kadri nitavyo pata habari zaidi.

UPDATE:
Polisi wamefika eneo la tukio na kwa sasa wanawakamata wakata mbao, wachungaji na wachoma mkaa wakiwatuhumu kwa ‘ujambazi' wakati wapiga deal halisi wameisha sepa , walinzi 8 wa mgodini ( wa kitanzania) wameahidiwa 10,000 USD kila mmoja kwa kuweza kulinda mali ya ' mwekezaji', huku mlinzi mzungu akisafilishwa kurudi RZA kwa matibabu ( huyu jamaa amepigwa kama risasi 3 mkononi na mguuni, na huyu ndio aliyeuwa jambazi baada ya kukabiliana naye uso kwa uso).

Polisi wamekabidhiwa sub machine gun 3, mabomu ya mkono 9 ( moja lilirushwa lakini halikulipuka vizuri) magazine zaidi ya 5 zikiwa na risasi zaidi 100, bullet proof vest 2.

Polisi wanasomeshwa wakubali kuwa wao ndio waliopambana na ku uwa majambazi ili hawa jamaa wanakwepa lawama za mauaji kimtindo, Mwili wa jambazi (kipande cha jibaba lenye asili ya kisomali inaaminiki ndiye alikuwa kiongozi wa uvamizi) umepelekwa mortuary, nikifanikiwa nita upload picha ya maiti yake.

Hali ya hewa imetulia kidogo na shuguli za kumtumikia kaburu zimeanza mnamo 1330hrs, kwa ujumla kulikuwa na vitofali 34 vya dhahabu ( kila kitofali kina 24KG) vilivyo pona pona kutembea ( ila nawalaumu hawa ma intruders kwa uchoyo wao!)

KUTOKA FIKRAPEVU:



PICHA ZAIDI kwa hisani ya
kanta (JF member):


 
ayallaaa ndili limezimwa ,ulizia utakuta kuna MKUBWA anahusika hapo,maana ndo Makada wa Magamba huko mikoani,mtu anatoa msaada wa milioni 500 ametoa wapi?Uchumi huu hu wa tanzania?
 
GOOD ATTEMPT. Kama waliofanikisha kulizima sakata hilo ni WATANZANIA, KIFO HALALI YAO. Nategemea waliohusika kuzima watanzania kuchukua MADINI YAO kuwa ni wazungu tu, kwani wanapeleka kwao
 
Natamani wangefanikiwa kuiba tu.. angalau na sisi huku mitaani tungenusa kidogo hiyo hela
siku moja nilikuwa naongea na injinia wa mgodini, nMtanzania mwenye mapozi hivi, aisee! anakubaliana na wizi wa madini yetu, halafu anapotosha ukweli eti madini hayawezi kutuinua kwenye tope la umaskini, wangekalenga kenyewe kwanza kafie mbali
 
Lakini wangevuta subira wakalipua hata ndege, halafu wananchi wakawa wa kwanza kufika eneo la tukio kuokota dhahabu.
 
HAO WEZI walikosea stepu gani aisee?
 
Wadau,nasikia GGM kunawaka moto sasa hivi,majambazi wamevamia mgodini na hivi sasa nasikia wanapambana na polisi pamoja na walinzi wa mgodi.Wamevizia msafara wa kusafirisha dhahabu, mtu mmoja ameuwawa na mwingine amejeruhiwa vibaya na hali bado haijakaa sawa.Nitawajuza zaidi endapo waliopo mgodini watanipa taarifa mapema.
 
Hawa watakuwa wanyarwanda.......watanzania hawawezi mikiki hii

watanzania waliotengenezwa na nyerere sio waliozalishwa na mfumo wa mwinyi, mkapa na kikwete, vizazi vitatu hivi wana hasira na wizi unaotendeka ndani ya nchi yao. usijidanganye eti sio watanzania, labda wanyarqwanda wanahusika kufanikisha upatikanani wa armaments tu, lakini uchoraji wa ramani na utekelezaji ni kizazi cha Mwinyi, Mkapa na Mrisho
 
Ni kweli kuna majambazi yamevamia escort ya Gold Shiftment mapambano yanaendelea lkn cjapata taarifa za watu kufa tusubiri tutawajuza
 
Si deal ingetik tu asee... Kama vipi walipue hiyo ndege inayopeleka zawadi zetu kwa makaburu.
 

Mkuu tunasubiri updates,Geita home aiseeee
 
hiyo dhahabu ingechukuliwa angalau tungenufaika kidogo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…