watanzania waliotengenezwa na nyerere sio waliozalishwa na mfumo wa mwinyi, mkapa na kikwete, vizazi vitatu hivi wana hasira na wizi unaotendeka ndani ya nchi yao. usijidanganye eti sio watanzania, labda wanyarqwanda wanahusika kufanikisha upatikanani wa armaments tu, lakini uchoraji wa ramani na utekelezaji ni kizazi cha Mwinyi, Mkapa na Mrisho
Ndiyo bwana!!Natamani wangefanikiwa kuiba tu.. angalau na sisi huku mitaani tungenusa kidogo hiyo hela
Uchoyo wa nini Mkuu?Hali ya hewa imetulia kidogo na shuguli za kumtumikia kaburu zimeanza mnamo 1330hrs, kwa ujumla kulikuwa na vitofali 34 vya dhahabu ( kila kitofali kina 24KG) vilivyo pona pona kutembea (ila nawalaumu hawa ma intruders kwa uchoyo wao!)
kwa ujumla kulikuwa na vitofali 34 vya dhahabu ( kila kitofali kina 24KG) vilivyo pona pona kutembea ( ila nawalaumu hawa ma intruders kwa uchoyo wao!)
hii habari ni mpya na inaibua mawazo mapya pia!
Kwani katika tafsiri na uelewa wa kawaida, kati ya hawa wawili nani hasa ni mwizi!?
Na kama upande 'ulioshindwa' ni waliotaka kuzuia madini yasisafirishwe nje ya nchi ili wayafaidi wao, basi ni wapi Watz wengi wataegemea!?
Mkuu wee acha tu, hata mimi sielewi mwizi ni nani hapa, maana kama mtu ana uwezo wa kuruka na ndege kuanzia mgodini hadi huko aendako na hakuna ukaguzi wowote mahali popote hii haingii akilini kabisa. Juzi nilikua nimetoka safari na viroba vinne vya mkaa na kitanda kimoja nilipofika kibiti nikasimiamamishwa na kuanza kukaguliwa eti nilipie ushuru....pumbafu kabisa, wachukue tu kwanza tuwaite Majasiri na mashujaa wa taifa hili hao waliojaribu. Halafu nione kijitu kinasimama kwenye Luninga na kujifanya kuua majambazi.
siku moja nilikuwa naongea na injinia wa mgodini, nMtanzania mwenye mapozi hivi, aisee! anakubaliana na wizi wa madini yetu, halafu anapotosha ukweli eti madini hayawezi kutuinua kwenye tope la umaskini, wangekalenga kenyewe kwanza kafie mbali
Wadau,nasikia GGM kunawaka moto sasa hivi,majambazi wamevamia mgodini na hivi sasa nasikia wanapambana na polisi pamoja na walinzi wa mgodi.Wamevizia msafara wa kusafirisha dhahabu, mtu mmoja ameuwawa na mwingine amejeruhiwa vibaya na hali bado haijakaa sawa.Nitawajuza zaidi endapo waliopo mgodini watanipa taarifa mapema.