Jaribio la kutaka kuiangusha serikali ya Nyerere 1982/1983

Asante kwa kumbukumbu nzuri. Cocabs zilikuwa ni taxi zikipaki kwa wingi pale Kilimanjaro Hotels miaka ile ya 1980 mwanzoni.
 
Aiseee nimependa andiko lako la historia hii. Kudos!!
 
Je huyu Hatibu Gandhi aka Hatty MacGhee alikuwa ni mmarekani ama?
 
Je huyu Hatibu Gandhi aka Hatty MacGhee alikuwa ni mmarekani ama?
Hapana, alikuwa mtanzania. Inasemekana amekulia kariakoo, had tukio lile linatendeka wazazi wake na ndugu zake walikuwa bado wanaishi kariakoo, pia inasemekana chimbuko lake ni muheza - Tanga
 
Hapana, alikuwa mtanzania. Inasemekana amekulia kariakoo, had tukio lile linatendeka wazazi wake na ndugu zake walikuwa bado wanaishi kariakoo, pia inasemekana chimbuko lake ni muheza - Tanga
Hilo jina Hatty MacGhee sio la kiswahili kabisa
 
Kama Nyerere alinusurika kupinduliwa mara kadhaa , basi yawezekana kung'atuka kwake hakukutoka moyoni Bali yawezekana alishauriwa tu na waungwana kwamba mzee a step off The throne kuepuka aibu ya kupinduliwa au pia kuuawa you never know. Dunia Ina mengi.
 
Yote yanawezekana.

Ila wachambuzi wa mambo wanadai mzee aliona anapoelekea na fikra & misimamo yake anakwenda kuwauwa wananchi wake ilihali hawez kukubali sera za magharibi upande wa pili. Akaona Bora ang'atuke Ili ajae ndio akubali sera za magharibi ila sii yeye.


NB; kipindi hicho umaskin ulikuwa umeshamiri kupita maelezo
 
Masharti ya IMF na World Bank, yale ya Structural Adjustment Programme. Alimuachia sakata Mwinyi alicheze rumba.
 
Naam, japo inasemekana kuwa mastermind alikuwa yeye mwenyewe - angalau ajioshe mikono yake
 
Baadhi yetu tulikuwepo na tumeyapitia mengi tu, mpaka ya kufanya maandamano kupinga sera za IMF na kujiuzulu kwa Mzee Mtei.
Dah, nikikumbuka zile enzi naona safari ya maendeleo taifa liliyo ipiga ni kubwa sana.

Ajabu kuna watu tz ya Leo wanasema hakuna maendeleo!!
 
Sio kweli, nadhani huyo jamaa wa Simba kwa sababu ni maarufu ndio anajulika lakini naamini kuna wengine baadhi watakuwepo wapo japo siwajui.
P.
acha uongo.
washtakiwa wa Uhaini 1982 walishakufa wote.
the most recent ni Hans Pope, boss wako wa zamani wakati umeajiriwa Part-Time "Radio One"
 
acha uongo.
washtakiwa wa Uhaini 1982 walishakufa wote.
the most recent ni Hans Pope, boss wako wa zamani wakati umeajiriwa Part-Time "Radio One"
Mkuu Afande Macha, heshima kitu cha bure, huku kuitana waongo kwa kitu ambacho huna uhakika nacho, sio kunitendea haki!. Jee wewe unawajua washitakiwa wote 46 na unauhakika wote wamekufa?.
P
 
Kila mtu atakufa.

Na hao wahaini wangefanikiw anchi ingekuwa ya ovyo sana.

Tumeweza kuukata Ujamaa polepole bila mapinduzi ya nguvu.
 

This was my Sunday reading
Very well presented.
Excellent!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…