Habari wanajukwaa. Leo nimepigiwa simu kutoka namba +255673099097, mpigaji akijitambulisha kuwa anafanya kazi makao makuu ya vodacom. Nilivyosikia hivyo tu, nikajua matapeli hawa. Basi nikajifanya mjinga kwenda naye taratibu ili asishtuke.
Alisema kuwa kuna mtu katuma pesa kwenye account yangu ya voda kimakosa, na akataka kujua kama nimepata message yoyote. Mimi nikamwambia, akate simu kwanza niione message yenyewe. Hakutaka kunipa muda huo, badala yake akaniuliza kiasi cha pesa kilichopo katika account yangu. Aliposisitiza sana nikaamua kudanganya kwa kumtajia kiasi kikubwa. Bila hata kunipa fursa ya kutazama kama kuna message yoyote akaishia kunitukana tusi baya sana huku akisema haioni pesa hiyo.
Kiasi chenyewe nilichomtajia ni shs 250,000, ambazo kwakweli hazikuwemo. Alivyomaliza kutukana akakata simu.
Nimebaki na maswali kadhaa. La kwanza, namba aliyotumia kupiga nadhani ni ya mtandao wa Tigo, huku akijitambulisha kuwa yuko vodacom, sijui ni kwanini?
Pili, alijuaje kuwa kweli sina pesa yoyote kwenye account yangu ya mpesa?
Nawasilisha.