Ninaishi na mtoto wa kike wa miaka 12, alikuwa anaishi kijijini na bibi yake na kwa sasa naishi nae huku mjini. Huyu mtoto kifupi kakulia mazingira magumu kimaisha na amedumaa pia, ana miaka 12 lakini nimempeleka shule wamemkubali darasa la kwanza. Tatizo lake ni kwamba ana sweat sana, yani usiku ile sehemu yote aliyolala inakuwa imeloa jasho. Halafu jasho lake si la kawaida kabisa, yani harufu yake ni kali sana kama ya kitu kilicho chacha. Naomba kujuzwa kama hili ni tatizo la kiafya au nini.
Nawakilisha.