Jasusi Honda ndani ya mpango wa Congo

Kudo nakupa pongezi sana sana kwa story zako huwa uniangushi uko vizuri by Jasusi Honda
 
 

Mzigo umesisisma sema tu unatoka kidogo kidogo sana haikati KIU Kabisa
 
Ahsante Kudo hadithi nzuri sana,ila kuna mahali umechanganya badala ya Mtega Nyoka ukaandika Honda
Kweli aisee, ahsante kwa kuliona hilo nalifanyia kaz
 
Riwaya : mpango Congo

Sehemu ya kumi



Kilichofuata ni saluti kutoka kwa askari wale. Mtega nyoka hakujali saluti zao aligeuka na kujichanganya kwenye umati wa watu ulioanza kujikusanya tena huku kwa mbali akisikia king’ora cha gari la polisi kilisikika kikija eneo lile hivyo akajua askari wale watakuwa waliomba usaidizi makao makuu kwa kudhani wao ni wezi wakiwa wanapanga kuiba benki.

***
Dakika kumi badae Mtega nyoka alikuwa ndani ya nyumba ya kulala wageni ya D8,pembezoni kidogo mwa stendi ya mabasi ya Buzuruga.

Akilini mwake aliona mapicha ambayo hakujua yana mana gani.

Kwanza ni operesheni yake maalumu ya kuwatafuta wahandisi watatu waliohusika katika ujenzi wa jengo fulani, na kabla hajawafikia akakutana na maiti zao.

Nani alieua;? Hakumjua.

Pili ni wakati akijaribu kutafuta fununu za wahusika wa mauaji yale na kujua sababu za mauaji, mara anakutana na binti wa ajabu anaeandamwa na watu wa ajabu.

Lakini kilichomumiza zaidi ni kuwa wote wawili walijikuta ndani ya ofisi za Kasuku contractors huku wote wakimuulizia Malima.

“Kuna nini Kati ya Malima na yule dada?” alijiuliza huku akiwa anatizama uso wake kwenye kioo kikubwa kilichokuwa ndani ya chumba alichokuwamo.
Akavuta pumzi nyingi na kuzishusha kwa nguvu, hapo ndipo alipohisi maumivu katikati ya paji la uso alipopigwa ngumi na mtekaji.

Akatabasamu!!.

Jamaa anangumi kavu” akajisemea huku akitoka kujitazama na kwenda kukaa kitandani.

Mara wazo likamjia.

Haraka akanyanyuka na kuvaa nguo na kisha akavaa raba safi nyeusi ilioendana na rangi ya fulana nyeusi aliokuwa amevaa, kisha akavaa kofia Kaki iloendana na suruali aliokuwa amevaa kisha akajitazama kwenye kioo.

Akajicheka mwenyewe!.

Hakuwa amevaa mpangilio sahihi wa rangi za mavazi yake.

“Nianzie wapi sasa!” alijiuliza mara bada ya kuongezeka wazo la pili tofauti na la awali..

Hatimae akanyakua simu yake na kutaka kupiga hatua ili atoke nje.

Simu ikaita.

Alipotizama mpigaji, sura yake ikajikunja kwa fadhaa huku akilini akijishauri namna ya kumjibu mpigaji.

Hatimae akapokea.

“Kimya sana mtegaji!’” iliunguruma sauti ya Mzee Kinyonga.

“Hali tete Mzee, ila nipo njia moja” alisema Mtega nyoka.

Ukapita ukimya wa sekunde kadhaa.

“Hali imeshavuka Def Cond 0002” alisema Kinyonga.

Mtega nyoka akatumbua macho na asione alichokitumbulia.

Hii ilikuwa mpya kwake.

“ina maana ilishaanza Def Cond 0001 na sasa inavuka 0002?” aliuliza Mtega nyoka

“Lakini sio ile unayoijua wewe” alisema Mtega nyoka.

Hapo tena Mtega nyoka akakwama sauti kisha akamsikia Kinyonga akiendelea kuelezea…

“ Hii Def inaandaa Def cond 0008,na sio kama ni ya ndani; la hasha, hii ni ya kutokea nje ikihusisha watu wa ndani, hivyo basi kipimo changu kinasoma 0002 bado ni kimya kimya” alifafanua Mzee Kinyonga.


“ooh Sawa nimeelewa, kwa hiyo, kwa huo mkia umeonekana au kichwa ndo kimeonekana” aliuliza Mtega nyoka.

“aaah Mtega nyoka!!; kwani lini umeanza kuniuliza habari za kina nyoka mimi Kinyonga?” alilalama Mzee kinyonga.

Mtega nyoka, aliamua kukaa kimya mana alijua jukumu bado ni lake yeye kapewa tu fununu.

Na kikubwa aliwaza uzito wa kipimo alichodokezewa yani Def cond.
Def cond(defence control) ni kipimo cha migogoro ndani ya serikali huku kikianza na 1-8,sasa Mtega nyoka alikuwa ameambiwa hii Def cond sio anayoijua, hivyo basi katika uelewa wake alijua ya kuwa kuna mipango ya usaliti inafanyika kuiangusha serikali, mana def ilikadiriwa kuelekea def cond 0008 kumaanisha huko kunafukuta Vita kamili.
Lakini pia aliambiwa yakuwa kuna watu ndani na nje katika mipango hiyo na yeye ndo anapaswa kuwatafuta.

Akatabasamu hasa alipokumbuka vifo vya wahandisi, siku moja iliopita.

Fumbo!!

Hiyo ilimaanisha kuna fumbo lipo ndani ya kampuni ya Kasuku contractors lakini swali likabaki kwake.

Kwa nini Kasuku?

Na lilikuwa swali la msingi yeye kujiuliza kwa sababu Kasuku wanahusika na uchoraji na ujenzi wa majengo, lakini hata jengo lililojengwa nao lililomhusisha Mtega nyoka wao wajengaji hawakujua ni la nini lakini pia ramani ya jengo hawakuwa nayo yote.

Sasa ni vipi Kasuku wahusike na sakata gumu vile?

Mtego!!

Akajiwazia huku akipiga hatua kutoka ndani ya chumba alichokuwamo.

***

Safari yake ilimfikisha hadi soko dogo la machinjioni Mandu, kisha huko akaungana na wasafiri wengine kupanda daladala za kwenda kisasa kulikokuwa na mazishi ya mmoja wahandisi wa kampuni ya Kasuku.

Alichagua kwenda hapa, sababu wengine walisafirishwa mikoani kwao kwa ajili ya maziko.

Alifika mazishini na kushuhudia umati wa watu wengi sana ukiwa umejuimuika pamoja huku baadhi ya watu wakiwa wamejitenga huku na huko.

Msiba ulikuwa umepokea watu wa kila aina huku magari ya kifahari yakiwa yametapakaa kila sehemu hii ilimaanisha aliefariki alikuwa ni mtu wa watu lakini pia alikuwa ni mwenye kujiweza kifedha..

Roho ilimuuma mtega nyoka hasa aliposikia sauti za akina mama wakiomboleza.

“kwanini waluwawa watu hawa?” alijiuliza mtega nyoka bila kupata majibu.

“mtuhumiwa wa kwanza yupo kwetu au yupo ndani ya Kasuku” alizidi kuwaza mtega nyoka huku akipepesa macho huku na huko na hapo akaona vijana wa usalama kadhaa wakiwa katika majukumu yao ya kufuatilia kesi ile.

Akaachana nao na macho yake yakagota kwa kijana mmoja mtanashati akiwa amekaa na vijana wengine wawili wakijadili jambo huku mara kadhaa wakionekana kufurahia walichokuwa wanakijadili.

Lakini wakiwa katikati ya majadiliano mara akaja binti mmoja na kumuita yule kijana mtanashati alietizamwa na Mtega nyoka.

Yule kijana akaenda kumsikiliza yule binti, huku maongezi yao yakionekana kuwa ya utata upande mmoja kwani binti aliongea kwa kubabaika ama kuchanganywa na jambo huku kijana wa kiume akiwa makini kusikiliza.

Mtega nyoka akavuta hatua kujipitisha karibu yao, lakini kabla hajawafikia tayari walikuwa wamekwisha kuongozana kutoka eneo lile.

“una nini Malima!!” alijisemea Mtega nyoka huku akiangaza huku na huko ili aone kama kulikuwa kuna mtu mwingine aliekuwa anafuatilia nyendo za kijana yule.

Alimuona!!
 
shukrani mkuu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…