Jasusi la kitanzania lilivyowatoka wanajeshi Uganda

Naam, NAKULABYE (maana yake Nimekuona). Iko karibu na Kasubi,, makao ya Kabaka (ukiwa kwenye kilima cha Nakulabye, unakuwa unaikabili Ikulu ya Mfalme, ndo maana ya nimekuona Kabaka). Bombo iko karibu na Namirembe (Makao Makuu ya Kanisa Anglikana Uganda). Neno hili lina maanisha HURUMA za MUNGU. Kanisa hili (Cathedral)liko Kusini mwa Chuo Kikuu cha Makelele (kilicho eneo la Wandegeya).....
 

MKUU UMETOKA SEHEMU YA 4 UMEENDA SEHEMU YA 6 NAOMBA NIWEKEE SEHEMU YA 5 PLEASE
 
Hadithi nzuri, ya kutunga of course, fiction. Mtunzi amejitahidi kuwianisha na historia, mfano ametaja kwa usahihi kuwa mkuu wa SRB alikuwa Col Farouk Minowa. Lakini amekosea vitu vingine vya kihistoria ambavyo angepatia hii hadithi ingekuwa na uhalisia zaidi. Mifano:
  1. Pesa aliyopewa ya uhamisho kutoka Dar shilingi laki tatu. Mwaka 1978 sh laki tatu ilikuwa pesa nyingi za kutisha. Mwaka huo nilikuwa shule ya msingi darasa la nne, na ninakumbuka kaka yangu alianza kazi mwaka huo alikuja nyumbani akaomba misa ya shukrani kwa kupata kazi yenye mshahara mzuri wa shilingi 750 kwa mwezi. Haiwezekani kwa mwaka huo mtu alipwe fedha za uhamisho ambazo ni sawa na mishahara ya karibu miaka 3! Mtunzi akarekebishe historia hapo.
  2. Mtunzi ametaja mtaa wa Luwum kule Kampala. Mtaa huo ulipewa jina hilo baada ya Iddi Amin kuondoka madarakani, kwa kumuenzi Askofu wa kianglikana Janan Luwum aliyeuawa na Amin. Kwa kuwa hadithi ni ya kipindi cha Amin, mtaa huo haupaswi kutajwa kwa jina hilo, anapaswa afanye utafiti ajue jina lililokuwa likitumika wakati huo.
  3. Matumizi ya simu. Mtunzi anasema huyo mwanamke aliyemrubuni na kwenda naye kwake alipopigiwa simu aliondoka nayo eti akazungumzie mbali. Kifupi mtunzi anataka kutuaminisha kuwa hiyo ilikuwa simu ya kiganjani. Mwaka 1978 simu za kiganjani hazikuwepo, simu zote zilikuwa za mezani, zile za kuzungusha tarakimu.
Licha ya makosa hayo ya kihistoria, mtunzi ana makosa ya kumbukumbu pia. Anatusimulia kuwa huyu mhusika mkuu alipigwa risasi ya bega alipokuwa anawatoroka SRB, eti akatibiwa na padre wiki moja, halafu akawa mzima kabisa hadi anafukuzia mademu, anaoga kwenye bathtub na jeraha lake la risasi begani!
 
Nilinunua copy moja ya kitabu cha huyu jamaa nahisi hela yangu haikutendewa haki.
 
Good observation mkuu, nami nilikuwa nahubiri nikimaliza nicorment hivyohivyo, pia maji ya chupa mwaka 78 hayakuwepo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…