Congo inahitaji mtu kama Abiy Ahmed wa Ethiopia
View attachment 2504230 Unajua nchi zetu hizi za Afrika ni ngumu kupata sampuli kama yake. Viongozi waandamizi huchaguliwa wenye uwezo mdogo au wa wastani wasimzidi Rais, ikitokea kiongozi mwandamizi ana uwezo zaidi anaonekana tishio au kiherehere. Ndio yale ya Mrema akiwa Internal Minister anamzidi Mwinyi kuogopwa na kufanya maamuzi magumu.
Sasa Felix Tshisekedi kabebwa kwa kiasi kidogo na baba yake, Etiene. Etiene alikaa serikalini na kuwa Waziri Mkuu mara tatu na kabla alikuwa mpinzani tangu enzi za Mobutu. Etiene aliijua vizuri serikali, Felix alikijua chama chake sio serikali. Felix ndio Rais wa Congo kuchaguliwa kwa halali tangu wapate uhuru, chaguzi nyingine kunakuwepo na compromise, ingawa hata yeye kulikuwa na factions na inasemekana hakushinda uchaguzi ila alisaidiwa na team Kabila (kuliko Rais awe Martin Fayulu ambaye ni hardliner, bora awe Felix hana shida). Na kanisa inasemekana lilimtaka Felix. Bahati nzuri waliyokuwa nayo Congo ndio hii tu sidhani kama future wataipata.
Tofauti na Congo, pale Ethiopia Abiy Ahmed alikuwa mkuu wa usalama wa taifa kabla ya kuwa kiongozi wa nchi. Alipokuja alianza reforms mwaka uleule maana akitokea serikalini hivyo hakuanza kujifunza. Akapata na Nobel Peace Prize ila baadae akaona mageuzi aliyofanya yanamgeuka, mfano aliwafungulia maelfu ya wafungwa wa kisiasa ili nchi ipate reconciliation ila yale mafungwa yalipofunguliwa yakaanza chokochoko za kikabila tena.
Akaona sasa huu ujinga akaanza kuwaua na kuwaondoa kwenye nyadhifa nyeti za serikali wale wapuuzi. Pale Ethiopia kuna ukabila mkubwa sana ila Abiy amechanganya damu ya makabila mawili makuu na hasimu (hii ilimpa point kuwa mkuu wa nchi), ila bado makabila hayo kila moja linataka alipendelee. Mwishoni ikatokea vita kali Tigray na imeua watu wengi. Ethiopia ingejichanganya ikachagua mzembe tofauti na yeye sasahivi tungekuwa na Eritrea kama mbili za ziada. Na bahati yao wameitumia vizuri, kiongozi kijana in his 40s, katoka serikalini kidogo na ni smart hajabebwa.
Naona nchi nyingi huongozwa na vilaza, na sina imani na viongozi wazee kuanzia 65+ uko kwa nchi zetu zenye shida hizi. Na siamini kwenye viongozi waliokulia serikalini miaka zaidi ya 30 huwa hawana akili ila hawajui tu, hawana mawazo mapya. Na bado siamini mkuu wa nchi kutokea nje ya serikali kabisa kabisa yaani hajawahi ongoza hata mkoa au katoka jeshi. Huyo atapoteza miaka kujifunza kwanza au hatokuwa na busara au shida yoyote nyingine. Pale Marekani tumemuona Trump mfanyabiashara aliyeibukia Urais, ila sio lazima iwe hivyo maana Zelensky pale Ukraine kaonyesha ukomavu.