JATU ni Mr Kuku mwingine, ni swala la muda tu

DSE walikuwa na hali mbaya sana kipindi Cha Magufuli na Corona kwahiyo ilibiidi wamkubalie kila mtu kuingia lakini ukweli Jatu imeingia pre mature. Mtawapata sana wale wa Kilimo Cha PDF, ambao na Mr Kuku aliwapata. Lakini kwa mtu aliyewahi kulima gharama zetu ni kubwa mno na faida kiduchu.
 
Binafsi naomba niwaeleze watanzania na wengine wenye nia ya kujiunga na hii kampuni. Nimefanya nao kilimo kuanzia mwaka 2020/2021. Mavuno yalipaswa kuwa 2021. Nimeweka pesa nyingi kwao, nadhani kati ya wakulima 10 na mimi nimo.

Kwanza customer care yao sio nzuri. Yaani unasumbuka sana kufanya kitu cha kawaida. Wanapenda sana pesa ila unapohitaji huduma wanakusumbua sana. Kwa siku unaweza kuongea na watu kama 10 bila mafanikio.

Pili, kuna kila dalili za uongo kwenye kilimo chao. Mfano CEO wa hiyo kampuni anakaa anabadilisha simu. Yaani unaweza kuongea naye leo, kesho akawa na namba nyingine ya simu. Hii ni dalili ya kukwepa watu. Anaweza akawa anakwepa watu hili kuepuka usumbufu wa maswali ya ujinga lakini pia anaweza kuwa anakwepa watu sababu hana majibu.

Nimeongea na manager, CEO...hawa wote mtindo wao wa kukwepa watu ni mmoja tu. Hawawezi kukupa jibu lolote. Hii inaonesha kampuni yao ipo kupiga watu na si kilimo kama wanavyotangaza.

Mavuno ya mwaka huu 2021 yamefanyika ila hawakutangaza maharage wamepata nini...eti mpaka mwezi wa kumi. Sasa jipimie mwenyewe. Yaani unalima kitu kwa mwaka mmoja...pengine hutapata pesa yako mpaka baada ya miaka miwili. Ni nani huwa analima hivyo?

Sasa hivi wametangaza mazao yaliyopatikana kwenye mchele na mahindi. Cha ajabu sasa, wanakwepa simu za watu...yaani huwezi kupiga simu ukaulizia kwamba unataka kuuza mazao yako wakapokea au wakakwambia kitu chochote. Hi ni kuanzia kwa CEO (huyu huwezi kumpata), manager (huyu nadhani anadanganya tu) na wafanyakazi wa kawaida (hawa ndo basi)...yaani management ikiisha sasa wafanyakazi wafanye nini?

Kwa ufupi uhusiano wao na wewe ni pale unapopeleka pesa tu. Hakuna mahusiano zaidi ya hapo. Baada ya hapo huwapati tena. Manager huwa anadai yupo busy kwenye mikutano. Sasa swali ni kwamba, unafanya mikutano na kina nani kama unawakwepa wawekezaji wako?

Serikali ya Magufuli ilikuwa imeanza kuwachunguza. Ilidhani wanauzia watu mashamba ya maharage ambayo hawana. Kwa kuogopa walikuwa wamestisha kuwauzia watu. Baada ya Rais Magufuli kufariki, wakaaza kuwauzia tena watu. Nina wasi wasi kama kweli wana hekari za kutosha za maharage na inaonekana ndio maana hawakutangaza kiasi walichopata.

Kampuni ina kila adalili za ubabaishaji. Wewe hata usiende mbali. Mtafute manager wao..ongea naye kwa week 1. Utajua! Akishajua wamechukua pesa zako anakukwepa.

Nitaendelea kufatilia zaidi na kutoa update kadri ntakavyowasoma. Kwa sasa sitashauri watu wasiwekeze kwao. Ntasema tu watu wawe makini. Kama kuna kitu chochote ntakachojifunza zaidi chenye kunionesha mambo tofauti na haya niloandika ntakisema hapa. Ila kwa sasa, haya ndo nimeona. Hakuna kampuni duniani haithamini wawekezaji. Ukiona kampuni ya hivyo, ni dalili za uhuni.
 
Unachoongea ni kweli kuna dada alinishawishi sana kujiunga nao lakini kila nikimpiga maswali anakimbia nikaona dalili za upigaji
 
Mr. Kuku alikua anafanya hivyo hivyo
 
Nimepiga kambi hapa
 
Na kwenye kuuza hisa za buku 5 make naona wamajitahid kupromote
 

[emoji120][emoji120]
 
duh naona kuna kenge wameanza kutoka damu maskioni! poleni sana wadanganyika !
 
kuna kampuni nyingine inajihusisha na kilimo cha vanilla ni harufu ya utapeli
Hawa watu wa Vanilla Village wa hapo Njombe nao ni hao hao. Kuna wastaafu fulani wamewekeza na hawa Vanilla Village kwa kuingia nao mkataba wa kuwalimia vanilla kwa njia ya Greenhouse, mkataba wa thamani ya Shs.33mi/-; LAKINI kitu cha ajabu ni kuwa hawawapi huduma sitahiki, ni ubabaishaji tu hata zile huduma basic kama kufungia na kunyweshea hiyo miche hawafanyi! Pia nimebahatika kuuona huo mkataba ni wa kunufaisha upande mmoja tu - wa Vanilla Village International, kama wanavyo jiita!

Naandika haya kwani nami nilihamasika sana na huu mradi hasa hiyo bei ya Shilingi Milioni moja kwa KILO YA VANILLA! Hivyo nikafanya utafiti kwa kuwatumia rafiki zangu wa huko huko ambao walikwenda hadi kijiji zilipo ofisi ndogo na mashamba vanilla hapo Vanill Village na kugundua uongo na ujanja ujanja mwingi sana. Kwa haya machache, sisemi msiwekeze nao, bali fanyeni utafiti na mjiridhishe na hayo wasemayo na wayatangazayo siku hizi!
 
Na hapo inatakiwa ununue bidhaa zao kima cha chini ni Tsh 30,000/=. mwisbo wa siku na wewe unakuwa myeja wa bishaa zako au zenu.
 
Mwezi ukiisha na IPO inaisha hizo 500 per zinarudi pale zilipokuwa 1200 per share. Uzi usiishie hapa njoo mtoe madini tena
Mkuu hivi nikienda pale kwenye listed companies za DSE nitajuaje kama company hii ipo kwenye IPO period.
 
Mkuu hivi nikienda pale kwenye listed companies za DSE nitajuaje kama company hii ipo kwenye IPO period.
Hakuna faida kuwekeza DSE, kwa lugha rahisi tuambizane ukweli. DSE wenyewe ni madarali wanapost hata clip za Mr. Liquid anaipigia kampeni Jatu. Kampuni kuwa IPO ndio kwanza inaingia soko la hisa ukiwa unafatilia taarifa hizi kupitia DSE na kwingine utajua. Ni kama mashabiki wa mpira wanavyojua mkataba wa fulani unaisha msimu huu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…