JATU ni Mr Kuku mwingine, ni swala la muda tu

JATU Plc imefikia leo tar 9 Sep 2021 Shs 940 kwa hisa moja. Kutokea ile bei waliotumia kufanya listing ya Shs 500 kwa hisa.

Kwa ufupi, kama ulikuwa na Shs 20,000,000 benki imetulia mwezi wa 6 au wa 7. Ukajipiga kununua shares 40,000 kwa Shs 500. Leo ukiamua kuziuza unapata cash money Shs 37,600,000 (yani 40,000 x Shs 940).

Profit yako ni Shs 17,600,000 ambayo hujaitolea hata tone la jasho. Ni balaa tupu.


 
Wanunuzi kwa bei hiyo wanatoka wapi
 
Wanakulazimisha kununua mazao kilo 100 hadi 200. Ukishamaliza kununua, wakivuna mazao huwezi kulipwa hata ufanyeje. Watakuzungusha mpaka utachoka.

Taratibu zao, wao pekee ndo wanajiuzia mazao kwa bei ya kutupwa. Wakishanunua kwako, wanakulazimisha kukuuzia kwa bei karibu mara mbili ya ile walonunua kwako.

Wakigundua kwamba unahitaji pesa zako hili utoke, faida yako wanaikata asilimia 70. Watakudanganya kwamba kuna gharama za kilimo ziliongezeka kila ekari. Kumbuka mwanzoni wameishakutoa gharama kubwa sana za kulima ekari moja.

Pia wanakutoa gharama nyingine za ajabu. Yaani faida yako kama ni millioni moja, wanaweza kukupa laki mbili.
Viongozi wa hiyo kampuni ni waongo haswaa. Wakati wa kudai pesa, hakuna mtu atakayeongea na wewe mule ndani. Wote watajifanya hawafanyi kazi hapo.

Kwa ufupi sijui ni kitu gani kile. For sure sio kampuni. Operation zake ni kama upatu. Yaani hawa wanalipa hawa wanalipwa. Wasipolipa hawa, kila kitu kinakufa. Mfumo wao upo hivo hivo. Nina wasi wasi kama mashamba wanayosema yapo kweli. Inawezekana kuna ekari 20 za mahindi ila wao wanasema ekari 2000. Hawajali wateja hata kidogo. Naandaa report yao yenye data zao zote na maneno yao. Kwa wanaofatilia mtashangaa.

Kama unapenda kulima, jilimie mwenyewe. Hawa watakupotezea muda wako na akili yako. Wamekaa kama either hawajui wanafanya nini au wapo hili kupiga pesa yako.
 
Tuletee ripoti boss.
 
Tatizo linakuja nani atanunua ukitaka kuuza
 
By t
By the way, nimemsikia JATU kesha ingia naye kwenye Soko la Hisa la Dar-es-Salaam (Dar-es-Salaam Stock Exchange)! Inaewzekana mambo yake yakawa safi huko!
 
Nilikutana na Lundo la Watu Benki moja ya NMB wakinunua hisa za JATU
 
Nakushauri andika hiyo ripoti ili iwafunue macho wengine. Kwa kufanyahivyo utakuwa umewasaidia sana wengine.
 
Jatu Kawa listed lkn kwenye DSE km hii ilikua fraud schemes nadhani DSE wasingeiweka
 
Walianzaga Deci, wakaja kina Ontario, Mr. kuku n.k itafikia mwisho watu watashtuka wenyewe lakini kwa utaratibu wa kuwaambia namna hii utaitwa majina mengi
Biashara ya utapeli huwa ni ya milele coz kila siku Wajinga wapya wanaongezeka..

Ni bonge la investment endapo kama hutaishia kwenye nondo
 
Hatimaye unabii umetimia.
 
Reactions: Lee
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…